mimi si daktari, lakini through experience tunafahamu mtoto anatakiwa anyonye maziwa ya mama si chini ya miaka 1.5-2.
Ila kuanzia miezi 6 mtoto inabidi aanzishiwe vyakula vya ziada "supplimentary foods" hii ni kwa sababu katika umri huu mahitaji ya chakula kwa mwili wa mtoto yanakuwa yameongezeka sana na pia ubora na wingi wa maziwa ya mama unakuwa umepungua.
Ni kawaida kwa mara ya kwanza mtoto atakataa vyakula hivi vya ziada kutokana na kutokuvizoea ila inabidi utengeze chakula laini hasa "uji laini" na umuanzishie kidogo kidogo.