acha uongo na upotoshaji
Mtu wa jinsia ya kiume atakuwa ametenda kosa la kubaka kama
atakuwa amefanya tendo la ndoa na msichana au mwanamke chini ya
mazingira ambayo yanadondokea kwenye maelezo yafutayo:
(a) ambaye si mke wake, au awe mke wake ambaye ametengana
nae bila ridhaa yake wakati wa tendo la ndoa;
(b) kwa ridhaa yake, pale ambapo ridha yake imepatikana kwa
kutumia nguvu, vitisho, au kwa kumuogopesha au kumtishia
kumuua au kumuumiza au akiwa amezuiliwa isivyo halali;
(c) kwa ridhaa yake pale ambapo ridhaa yake imepatikana wakati
ambao alikutwa hana akili timamu au akiwa amelewa kwa
kushawishiwa na madawa ya kulevya, kitu au vitu ambavyo
amepewa na mtu au watu wengine isipokuwa ikithibitika kuwa
kulikuwa na ridhaa mwanzoni kati yao wawili;
(d) kwa ridhaa yake pale ambapo mwanamume alijua kuwa yeye si
mume wake, na kuwa ridhaa ilitolewa kwa sababu alifanywa
kuamini kuwa yeye ni mwanamume mwingine, ambaye yeye
mwenyewe, anaamini kuwa ameolewa nae kihalali;
(e) kwa ridhaa au bila ya ridhaa akiwa chini ya umri wa miaka
kumi na nane isipokuwa kama mwanamke ni mke wake
ambaye ana umri wa miaka kumi na tano au zaidi na
hajatengana na mumewe.
(3) Mtu yeyote-
(a) akiwa mtu wa mamlaka, kuchukulia kigezo cha nafasi yake ya
mamlaka, na anatenda kosa la kubaka kwa msichana au
mwanamke wa mahusiano ya kiofisi au kwa kukosea anamzuia
na kumbaka msichana au mwanamke;
(b) akiwa kwenye uongozi au kuwa miongoni mwa wafanyakazi wa
mahabusu au sehemu nyingine yeyote ya uangalizi, iliyoundwa
kisheria au kwa taasisi ya wanawake au watoto kwa kuchukulia
kigezo cha nafasi yake na kutenda kosa la kubaka msichana
yeyote au mwanamke mfanyakazi mwenzie wa magereza,
sehemu ya matunzo au taasisi.
(c) akiwa kwenye uongozi au mfanyakazi wa hospitali, kuchukulia
kigezo cha nafasi yake na kutenda kosa la kubaka msichana au
mwanamke;
(d) akiwa mganga wa kienyeji kuchukulia kigezo cha nafasi yake
na anatenda kosa la kubaka msichana au mwanamke ambaye ni
mteja wake kwa nia ya kupata uponyaji;
(e) akiwa kiongozi wa dini kuchukulia kigezo cha nafasi yake na
kutenda kosa la kubaka msichana au mwanamke.