Nikimuwaza Harmonize namkumbuka Kizzy Daniel

Nikimuwaza Harmonize namkumbuka Kizzy Daniel

herman joshua

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
1,967
Reaction score
3,212
Sijajua zaidi ni yapi yaliyomsibu Kizzy Daniel kuachana na management yake aliyokuwa nayo ila naona ni kama visa vinafanana na cha Harmonize.

Sitaki kujaribu kusema Harmonize atashuka ila najaribu kuangalia ukubwa aliokuwa nao Kizzy Daniel kipindi akiwa na management iliyomfikisha alipokuwepo na sasa alipo.

Kizzy Daniel alikuwa ni mkubwa tofauti na sasa ameshuka sana sijajua ni nini tatizo. Yote kwa yote Harmonize awe makini tu na atakachokuwa akifanya ili abaki kuwa juu.

Ni hayo tu nimejaribu kuwaza kwa sauti
 
Hata me naona harmo atapata tabu Sana ukubwa aliyoupata akiwa wasafi hataupata Tena ndomaana sasa hiv anatumia nguvu kubwa kupata support ya raia kwa kugawa chakula lakini namwambia watu chakula chako watakula na support kubwa hatapata.
 
Kabla ya kutoka management alikuwa akiitwa kiss daniel baada ya kupigwa ban ambayo ilihusisha nyimbo zote alizorekodi akiwa hapo hadi jina lake la kisanii akaamua ili asianze upya sana akaamua ajiite kizz daniel

Ila case ya harmonize na kizz ni tofauti sana maana kizz aliimarika kwa muda mfupi tu baada ya kutofautiana na uongozi wake wa zamani akaamua kuanzisha kampuni yake 'Fly Boy Inc' sasa harmo yeye itakuwa ngumu maana WCB ina mizizi mirefu mno tofauti na G-Worldwide (label ya zamani ya kiss)
 
Back
Top Bottom