Nikimzalia mtoto atanioa

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Nimekutana na Mabinti wengi ambao Wana akili na mtazamo wa aina hii kuwa wakiwa kwenye mahusiano na mtu na wakafanikiwa kuzaa basi wataolewa.

Mmoja akaniambia kuwa amepata mwanaume mzuri anayejali anataka ampe Zawadi ya "KUMZALIA MTOTO",

Hivi nyie Mabinti Huwa hamuoni, hamsikii na pia Huwa hamuulizi hata kwa watu walau??

Alafu kwanini mna akili mgando ya kukubali kumpa mwanaume mwili wako kabla ya Ndoa?
Unadhani ngono inatosha kumshawishi mwanaume akuoe?

Mnajitafutia u single mother kwa nguvu alafu baadae mnaanza kusema wanaume wote mbwa.

Wengine mna na mifano kuwa fulani alikuwa single mother akaolewa so hakuna shida....
oohπŸ€” jaribu na wewe, hautaamini macho Yako yatakayokupata....Mimi Niko palee

Tatizo siku hizi hao mnaoita Role models wenu ni watu wa hovyo... maisha ya mtandaoni changanya na zakoπŸ“Œ

Iko hivi...

Wanaume Huwa Wanajua kabisa kuwa huyu ni mke na huyu ni sagula-sagula, watakutumia na kukuacha Kisha utabaki na uchungu na maumivu makali yasiyoisha na mtoto wako.

Kama huyo mwanaume anakupenda na anataka umzalie afuate utaratibu, HAKUNA TENDO LA NDOA mpaka alipe mahari kwenu, mwende kanisani mfunge Ndoa alafu nenda ukazae hata Dozen ya Watoto (kama unadhani ni rahisi hivyo)

Mabinti ....
Zinaa kabla ya ndoa itakugharimu... Punguza masifa, tuliza komwe subiri mume wako mwamini mungu kwaajili ya ndoa nzuri kisha jitunze!!..

Pastor Lilian David Mbembela
 
Mapenzi Hayana Fadhila, mapenzi mauza uza, We unaoa wenzako wanakula Bure, hata mia hawatoi...
Mwanamke Kiumbe noma, akikunyima wewe haimaanishi kua awapi wengine, Anabana kwako anaachia kwa wengine.
 
Wewe unaweza kuvumilia kutofanya ngono mpaka ndoa?

Wanawake tunafanya ngono sababu tunasikia hamu na sio sababu ya kuwaridhisha tu wanaume.
Fanya pita kuleeeeee hiii mchezo hauitaji Hasira, mtu akiileta we tafuna imeishaaa hiyooooo
 
Wewe unaweza kuvumilia kutofanya ngono mpaka ndoa?

Wanawake tunafanya ngono sababu tunasikia hamu na sio sababu ya kuwaridhisha tu wanaume.
Wale wanaojitunza hadi kufikia kuolewa wao hawana hamu?

Mwanamke ameumbiwa uvumilivu ndiyo maana utakuta mwanamke anaweza kukaa miaka hajashiriki tendo na maisha yanasonga kama kawa.
 
Wale wanaojitunza hadi kufikia kuolewa wao hawana hamu?

Mwanamke ameumbiwa uvumilivu ndiyo maana utakuta mwanamke anaweza kukaa miaka hajashiriki tendo na maisha yanasonga kama kawa.
Mtu akitumia K yake wewe unaumia wapi?
Mtu ashindwe kufanya vitu vinavyompa raha eti kisa watu wamsifie yeye ni bikra! Uliona wapi?
 
Simple tu tuna wasomi ila hawana akili : kama kupima uzazi wako mbona mnaweza kwenda wote kama wenza mkapima uzazi mpaka magonjwa mengine then mkafunga ndoa kwa amani kabisa.
 
Mtu akitumia K yake wewe unaumia wapi?
Mtu ashindwe kufanya vitu vinavyompa raha eti kisa watu wamsifie yeye ni bikra! Uliona wapi?
Sawa sawa. Hongera kwa kutumia k yako ipasavyo naona wahun wanajipigia kisela maana sio kwa hamu zako hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…