Pole sana. Kula denda kunahitaji uhakika wa usafi wa kinywa wa hali ya juu, mdomo wa mtu huhifadhi uchafu mwingi na bakteria wengi huzagaa kwenye fizi ulimi na meno, sasa kuvamia mtu usiyemjua umakini wake katika usafi wa kinywa ni kujiingiza kwenye maambukizo, kwa wapenzi ni vizuri kujiandaa kwa usafi wa kinywa pamoja na sehemu mbalimbali zitakazohusika kabla ya kumkabili mwenzio, kuna mtu hajui hata kupiga mswaki unaanzaje kumla denda?. Wakati fulani niliwahi kuona mtu aliyeoza mdomo kwa kile kilichoelezwa kuwa amepata maambukizo baada ya kunyonya sehemu za siri la mpenzi wake. Ni vizuri kujihadhari na mapenzi yasio ratibiwa ili kujiepusha na maradhi mbalimbali.