Frederick Daudi
New Member
- Jul 11, 2021
- 1
- 1
NIKIONA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YANAELEA KILA MWAKA, NAJUA YAMEUNDWA
Utangulizi
Elimu yetu imekuwa ikipitia katika vipindi tofautitofauti na mabadiliko makubwa ili kuiboresha. Mabadiliko haya huhusisha viongozi, mitaala, mihutasari na hata fomati ya mitihani. Hii ni tafsiri tu kwamba hakuna kinachodumu. Mabadiliko ya marais wa nchi hii, mawaziri wa elimu pamoja, wenyeviti na makatibu watendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) yamekuwa na mchango wa moja kwa moja kwenye matokeo ya mitihani anuai. Hapa tutajikita zaidi katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita (ACSEE).
Hebu turudi nyuma miaka 10 iliyopita
Tangu mwaka 2013 mpaka sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu. Sizungumzii tu mabadiliko ya mawaziri wa elimu kuanzia Dr. Shukuru Kawambwa, Prof. Joyce Ndalichako na Prof. Adolf Mkenda. Wala sina mpango wa kuwakumbusha kwamba kipindi kile Mwenyekiti wa NECTA alikuwa ni Prof. Rwekaza Mkandala na sasa ni Prof. William Anangisye. Pia sina lengo la kuwataja makatibu wakuu wa baraza hilo toka wakati huo kwamba ni Prof. Joyce Ndalichako, Dkt. Charles Msonde na sasa Athuman Amasi kama kaimu katibu mtendaji. La hasha, hilo siyo kusudi la andiko hili.
Je, unaikumbuka BRN? Kama umesahau basi nikukumbushe kwamba kirefu chake ni Big Results Now (Matokeo Makubwa Sasa) - sera ya serikali ya kuleta mabadiliko chanya katika sekta 6 zilizopewa kipaumbele ikiwemo sekta ya elimu. Nakukumbusha tu kwamba mfumo uliotumika kupanga matokeo kipindi hicho ulikuwa ni wa Grade Point Average (GPA). Naam, huohuo mfumo ambao ni mpya kwako mwanachuo sasa hivi, uliwahi kutumika kipindi fulani katika ngazi za sekondari.
Ndiyo, kipindi hicho kuna 'B' na B+. Huo ni wakati wa Distinction, Merit, Credit, Pass na Fail. Sasa hivi mambo yamebadilika. Kila kiongozi ana maono yake na njia zake za kuifikia nchi ya ahadi.
Niko peke yangu nimetulia lakini kuna kelele nyingi kichwani mwangu. Najaribu kuyaangalia matokeo ya kidato cha sita kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2022 napata maswali mengi sana ambayo sina majibu yake na hayupo wa kunijibu hapa nilipo. Wakati 2013 ufaulu ulikuwa asilimia 87.85, mwaka huu ni asilimia 99.87; ufaulu umeongezeka sana.
Lakini tashtiti zangu ni je, ongezeko hilo lina maana gani? Je, masomo yamekuwa rahisi zaidi au wanafunzi wa sasa wana akili zaidi? Natambua kwamba muhtasari (syllabus) wa kila somo umebaki vilevile tangu 2009. Au labda kuna uhusiano wowote kati ya mabadiliko ya fomati za mitihani mwaka 2015 na 2020 na matokeohaya? Lakini ile ya 2020 inajikita kwenye umahiri unaozingatia viwango vya juu vya kufikiri. Au wanafunzi wanafikiri sana ndiyo maana wanafaulu sana?
Binafsi nilitarajia ugumu zaidi kwenye ufaulu kwa kipindi hiki kuliko kipindi cha nyuma. Nilitarajia kwamba umahiri huo unalenga kumpata mwanafunzi atakayepata daraja la kwanza awe amestahili na sio huyu mwenye 'A' kwenye somo la Kiingereza lakini akizungumza sentensi 10 za Kiingereza, nne zina makosa. Sikutarajia kwamba mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza kwenye tahasusi yoyote ile kwa umahiri wa viwango vya juu akifika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ashindwe kuingia mwaka wa tatu.
Hivi inakuaje mwaka 2021 na 2022 ufaulu kwenye somo la Kiswahili ni asilimia 100? Kumbe Kiswahili ni rahisi sana eeh? Hii ina maana kwamba Tanzania nzima hakuna aliyepata 'F'. Je, kipindi cha nyuma ambapo ufaulu ulikuwa haufiki asilimia hizo mitihani ilikuwa migumu zaidi ya sasa? Angalia ufaulu wa kila somo mwaka 2021 na 2022 halafu linganisha na 2013 kwenye majedwali hapa chini.
Chanzo: Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)
Mtanziko na tashwishwi yangu hutokana na utofauti unaokinzana na uhalisia. Yaani kipindi cha Matokeo Makubwa Sasa matokeo yalikuwa madogo kuliko kipindi cha umahiri unaozingatia viwango vya juu vya kufikiri. Au mfumo wa GPA ulileta ugumu kwenye ufaulu?
Nakumbuka wanafunzi waliofanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2012 na matokeo yao kutoka mwaka 2013, mtihani wao ualisahihishwa mara mbili. Au hili pia lilikuwa na mchango kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2013?
Maoni yangu
Kila mtu anafurahia ukuaji. Kila mtu anapenda maendeleo. Serikali, taasisi za elimu, wazazi, wanafunzi na wadau wengine wa elimu wanapenda kuona matokeo mazuri. Sote tunafurahi kuona maendeleo na mabadiliko chanya kwenye elimu. Lakini tahadhari lazima ichukuliwe.
Pamoja na ukweli kwamba nchi inahitaji wasomi wengi, uhalisia ni kwamba nchi inahitaji wasomi bora. Umakini unahitajika katika kufanya maboresho na mabadiliko katika suala la elimu. Si kila kinachoitwa maboresho huboresha. Hii siyo sehemu ya kila kiongozi mwenye dhamana kuleta kitu kipya. Majaribio mengine ni hatari kwa afya ya elimu.
Ufaulu mkubwa wa darasa la saba, ulegezaji wa vigezo vya ufaulu kuingia kidato cha tatu na ukubwa wa matokeo ya kidato cha sita hupelekea wasomi ambao vijana wa siku hizi huita 'wa mchongo". Ndiyo maana baadhi ya watu wenye shahada hawawezi hata kujieleza na kujenga hoja. Tunaandaa wasomi wa kupokea mishahara tu.
Nimeona mara kadhaa sasa, wanafunzi ambao walipata daraja la 4 kidato cha nne wakaenda shule binafsi kusoma kidato cha tano na sita na kupata daraja la kwanza. Wengine walipata sifuri wakarudia mtihani wa kidato cha nne mara 4 lakini walipopata tu 'credit' na kwenda sekondari ya juu, walikuja kufaulu kwa kiwango kikubwa na sasa wako vyuo vikuu. Inaonekana elimu ya kidato cha tano na sita ni rahisi sana!
Hitimisho
Vinavyoelea ni vile vilivyoundwa. Lakini chondechonde, tusiunde matokeo. Tuunde mifumo na sera nzuri ambayo itawaandaa wanafunzi bora wanaoelea kwa ufaulu mzuri kwani wao pia wameundwa. Hata hivyo nawapongeza wadau wote wa elimu kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa udanganyifu kwenye mitihani. Hii inaonesha kwamba wanafunzi wengi wanafanya mitihani peke yao na kupata matokeo halali. Lakini kuna haja ya kupitia tena mitaala, mihutasari, fomati, mifumo ya usahihishaji na utoaji wa matokeo ya kidato cha sita ili kutoa mazao bora. Elimu bora ni kiungo muhimu kwenye sekta zingine zote za kiuchumi na kijamii.
-Fredrick Daudi

Upvote
2