Nikipeleka kuku chotara kijijini nitapata matokeo mazuri?

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Wakuu hivi kwa mazingira ya kijijini ambapo kipato cha wengi ni cha chini, kuku wa chotara wataweza kuboresha maisha ya mwanakijiji?

Na kama sio hao, je ni kuku wa aina gani ni chaguo bora zaidi?
 
Mada yako ni kama haujiongezea nyama nyama sana, mkuu. Unawapeleka kijijini kwaajili ya kufuga au kuwauza? Labda tuanzie hapo ili tuone namna ya kukushauri.
 
Kama Nia ni kuwafuga kienyeji, peleka kuku chotara, watahimili zaidi mazingira ya kujitafutia chakula.
 
Mazingira ya kijijini chukua jogoo kubwa za chotara, tetea za kienyeji, utatoboa. Chotara hawaatamii, hivyo hata wakija taga mayai, hawatozaliana, ila ukiwa na dume la mbegu la chotara basi utafanikiwa.
 
Mada yako ni kama haujiongezea nyama nyama sana, mkuu. Unawapeleka kijijini kwaajili ya kufuga au kuwauza? Labda tuanzie hapo ili tuone namna ya kukushauri.
Kwa ajili ya kufuga
 
Vifaranga 100 vya chotara unaweza nunua kwa 150k
Hao huna uhakika utapata matetea wangapi na majogoo wangapi.

Pia hadi wakupatie vifaranga ni baada ya miezi 7.

Pia kuwatunza hadi waanze kukupatia vifaranga ni gharama pia.

Kwa fedha hiyo utapata matetea 20 ya 5,000/=, na majogoo 2 ya 25,000/=.

Hapo wewe hauhangaiki nao chakula, ni kuhesabu tu vifaranga. Baada ya mwaka banda hazitoshi.
 
  • Thanks
Reactions: PYD

Asante
 
Kwenye ukuaji kuna namna yakuwafanya wakienyeji wakawa wakubwa ndani ya miezi 3 ukauza?msosi upi?
 
Back
Top Bottom