Nikipenda tena nigeuke nguruwe

Nikipenda tena nigeuke nguruwe

daaa! nimeumia si kidogo, ila haya mambo ya kuchunguza chunguza nayo si mazuri.

we kausha muwekee vikwazo (hahahaha tafuta uzi flani wa jamaa alimuwekea vikwazo demu wake). pokonya kimtaji taratibuuu alafu lala mbele.

Umenifundisha jambo nalifanyia kazi nijikopeshe mtaji kidogo kidogo then ndio nimuache
 
Chunguza kwanza
Unamaanisha nini mkuu.....

Yaani unamshauri jamaa apande ndege kwenda kuchunguza huko China......[emoji15]

Ama haujasoma na kuelewa kilicho andikwa...... [emoji45]

Hivi unatarajia hadi umkute anahemewa kifuani ndipo utaamini......[emoji47]
 
Pole sana mkuu. Unaambiwa mwanamke ni mdhaifu hujui usemi huu una maana gani, hawa viumbe hata uwafanyie nini wape kila kitu hata mpe Dunia hii yote mwambie yako. Atadanganywa na kitu kidogo tu. Atasahau vyote.
Hawa viumbe, haijawahi kujulikana wanataka nini ama wanaridhika kwa lipi......
 
Nilimpenda sana mke wangu sababu ya tabia zake na upole wake juu yangu kumbe nilikuwa sijajua yeye ni nyoka.

Nimemkuta yuko na maisha ya chini sana nimesaidia yeye na ukoo wake nikasema nimpe mtaji kaanza biashara sasa nyota imemwakia China kila leo.

Mungu sio Lemutuz juzi nampigia simu kwenye mtandao wa We chat mtu hapokei. Kwakuwa nilijua yuko hotel gani nikagoogle hotel nikapata number eeeh nikapiga reception kuomba waniunganishe nae kapokea mwanaume nilivyosikia sauti ya mwanaume nikaongea kama mchina can I talk to ..... ;nikamtajia jina. Mke kapewa simu kusikia sauti yangu kakata simu.

Roho inaniuma sana sina nguvu maumivu haya ni mazito ukitoa msiba wa mamangu hakuna naweza fananisha na maumivu haya siku nikipenda tena nigeuke nguruwe nimeweka nadhiri.
Weka akiba ya maneno ndg yangu! Kwanj ulipopenda mwanzoni ulikua kunguni?nyumbu?kongoni? Au??

Kupenda ni hisia na huja automatic ni maumbile tuliyoumbiwa na Mungu.

Ni vema tukajifunza kuwa imara tunapokabiliana na changamoto kisha tunatoka salama.

Natamani ningekufunga king'smuzi bse huna muda utakua na mtu
 
pole sana chief,
ila hiyo nadhiri fanya ufanyavyo utajua mwenyewe ui vunje ita kuCost big time,

kumbuka kupenda sio akili inayoamua bali ni moyo + nafsi ss ww usije kujidanganha hutapenda, trust me utapenda tu tena this time utapenda zaidi ya ulivyompenda huyo,

japo utakuwa unajiaminisha hupendi maana ubongo na moyo wakat mwingine wanapingana ila uhalisia unabaki pale pale kwamba Moyo unapenda.

mnaambiwa kila siku msichukue maamuzi mnapokuwa na furaha sana au huzuni sana hamuelewi....ona ss umejitia kitanzi.

Vunja nadhiri hiyo before its too late chief, maisha haya.

ww sio wakwanza na hautakuwa wa mwisho kufanyiwa hivyo....be strong.

adios.
 
Msamehe tu mkuu, nature ndio inasumbua. Akirudi bado ni mkeo mkae chini mzungumze myajenge
 
Back
Top Bottom