Nikipona mchepuko anakula kibuti maana haridhiki

Baba yenu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,053
Reaction score
1,418
Nina mchepuko wangu ambao ninausimamia kwa 100% katika kila kitu

Huu mchepuko unanipenda kwa ninavyouona,pia nishauchunguza sana hauchepuki labda kama unafanya kwa siri sana

Tatizo lake haridhiki,anaomba helq kila sekunde hata umpe kiasi gani bado kesho atakuja akuombe

Unaweza mpa pesa nyingi tu ila kesho akarudi kutaka nyingine

Mpaka najiuliza hivi huyu hajui kuwa tuko kipindi cha bwana jpm??

Kilichonikera ni lastweek nimetoka kumlipia kodi yake kwenye nyumba anayokaa pesa nyingi vi mil kadhaa

Sasa cha ajabu jana nimeenda kupumzika kwake nikiwa naumw kweli na anaona hilo ila asubuh alipomka bila kujali naumwa na nimetoka kumlipia kodi juzijuzi tu eti akaniambia anaomba nimnunulie Iphone 7!!!!

Nilimwangalia na kukubali kishingo upnde ila nimepanga nikipona naenda kwa mwenye nyumba na kumweleza nafunga ile nyumba maana mimi ndo mpangaji na sio yeye

Na kwa sababu kila kitu kilichopo ndani ya ile nyumba nimenunua mimi nimepanga nimtolee nguo zake zikiwa kwenye begi na kuziweka nje kisha nibadili vitasa na funguo za milango yote

Akija atakuta vitu nje na mimi ntakuwa nishabadili line zangu kwa siku mbili tatu

Baada ya hapo ntatulia kdg kama wiki au mwezi kisha niibuke vyuoni nione kama ntapata mchepuko mpya uliokosa mkopo unitunze

Nb: nakuwa na mchepuko kwa sababu hatuko katik mahusiano mazuri na wife na isitoshe yuko mkoani

Je niko sahihi?
 
Hapana hauko sahihi ongea vizur na mke wako ili mmalize tofauti zenu kabisa hiyo michepuko haifadhiliki kbs
Ni muda sasa hatuko vizur so tunashirikiana kuhudumia watoto pekee ingawa sina mpango wa kuoa tena
 
Usifanye hivo wala kumdhalilisha kama unamuacha muache kwa amani kwani haina haja ya kufanya hivo Sana na hali ilivo ngumu basi uje kwangu na mie unilipie Kodi
 
Mchepuko sio solution ya matatzo katika ndoa hilo fahamu hebu mkae muyajenge na mkeo labda umbali umesababisha mapenz kupungua mjue mnafanyaje naamini unampenda mkeo fanya hivo matatzo ya kimahusiano hayatakiwi kukaa muda mrefu bila kupata ufumbuzi
 
Unaweza kuta huyu jamaa wife wake hana hata tecno anatumia simu ya tochi...
Hapana ndg ni mtu mkubwa tu anajitosheleza zaid ya kawaida na hiyo ndo sababu ilipelekea dharau zikaanza na kupelekea tutofautiane
 
Mchepuko sio solution ya matatzo katika ndoa hilo fahamu hebu mkae muyajenge na mkeo labda umbali umesababisha mapenz kupungua mjue mnafanyaje naamini unampenda mkeo fanya hivo matatzo ya kimahusiano hayatakiwi kukaa muda mrefu bila kupata ufumbuzi
Hatuwez kusuruhishwa maana kila mmoja anajiona anaweza ishi bila mwenzake na vyeo anavyopanda ndo vinampa kibur zaid acha tuish hivi hivi na sina mpango wa kuoa tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…