Nikisafisha picha kwa Tsh 2000 itanilipa?

Nikisafisha picha kwa Tsh 2000 itanilipa?

Nimenunua epson printer L800 na hapa mjini studio zinasafisha picha kwa tsh 200 picha ya size 4 kwa 6, je mimi nikisafisha kwa 200 nitapata faida? Msaada wadau
inalipa tu , mimi ninayo natumia kuprintia karibu kila siku. Tatizo ni speed ndogo lakini ni mashine safi sana
 
inalipa tu , mimi ninayo natumia kuprintia karibu kila siku. Tatizo ni speed ndogo lakini ni mashine safi sana

mkuu ushawahi ku print cd au dvd? na kama ndio kila cd unayoprint kwa kutumia printer hii una charge sh. ngapi?
 
Msaada wakuu nadandia mada...Mimi nina epson xp 600 inatumia cartrig tano sasa moja photo black 26xl imekwsha nmejaribu kurifill imegundua wno syo genuine. Naomba msaada wa kiufundi nifanye nn na npate wap refillable cartrig za hii printer!
 
mkuu ushawahi ku print cd au dvd? na kama ndio kila cd unayoprint kwa kutumia printer hii una charge sh. ngapi?
huwa na charge 500 kwa printing yoyote ile, printer nimenunua kwa matumizi yangu binafsi so bei hiyo siyo ya ushindani unaweza fanya utafiti zaidi ujue bei wanayo printia mtaani
 
Msaada wakuu nadandia mada...Mimi nina epson xp 600 inatumia cartrig tano sasa moja photo black 26xl imekwsha nmejaribu kurifill imegundua wno syo genuine. Naomba msaada wa kiufundi nifanye nn na npate wap refillable cartrig za hii printer!
hebu search google how to refill px600, kuna jinsi ya kufanya ikakubali kufanya kazi, nyingine kuna code za kuingiza, kuna kureset by using software, ila ukisearch vizuri unapata jibu
 
  • Faida utapata tena kubwa tu
  • Sababu cost za uendeshaji ni ndogo sana
  • Ninapo zungumzia cost za uendeshaji hapa nazungumzia ghalama ya ununuzi wa wino na ghalama ya ununuzi wa karatasi
  • Tazama hii picha kwanza
postjfjan19.jpg

Karatasi za Picha
  • Utapata kwa tsh 3'000 au 4'000 kwa dar es salaam
  • Huwa zinakuwa karatasi 20
  • Karatasi moja utatoa picha nne (4) za 4 x 6
  • Hivyo idadi ya picha ni 4 x 20 = Picha 80
  • Upande wa Fedha utakayopata 80 x tsh 200 = tsh 16'000 [ Hapo faida ni tsh 12'000 ]
Wino
  • Ni tsh 6'000 kwa chupa ndogo ya ml 70
  • Na ni tsh 10'000 - 16'000 kwa chupa ya ml 250
  • Kwa kazi ya printing picha kwa kila siku wastani wa picha 240 wino utajaza mara moja kwa kila miezi mitatu hadi minne (4)
Itafikia mahala - baada ya biashara kuchanganya mahesabu itakuwa ni karatasi tu, sababu sifa kubwa ya hii printer epson L800 ni kutotumia wino sana, hivyo hutofikiria unuaji wa wino.

Kwa kifupi - umenunua printer sahihi kwa kazi ya kusafisha picha za aina zote - HONGERA
Vipi kwa L850 Mkuu?
 
Back
Top Bottom