Nikiulizwa Magufuli ameacha nini kikubwa, nitasema kuwa Magufuli ameacha hofu kwa Watanzania

Nikiulizwa Magufuli ameacha nini kikubwa, nitasema kuwa Magufuli ameacha hofu kwa Watanzania

Uko sahihi.
Kuu zaidi watu wengi sana wameona umuhimu mkubwa na wa haraka wa nchi kuwa na KATIBA MPYA.
Mbowe anasema ukidai Katiba Mpya ni siasa zisizo za kistaarabu.

Ameamua kufanya siasa za kistaarabu baada ya kunywa chai ikulu na kupewa bahasha ya khaki. 😁
 
😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁
 
Habari!

Kwakuwa jf ni huru sidhani kama uzi huu uliojaa mawazo huru usio na kejeli wala matusi sitarajii kwamba utafutwa.

Nikiulizwa Magufuli ameacha nini kwa Watanzania, pasi kupapasa nitajibu kuwa "Magufuli ameacha hofu kwa Watanzania, itachukua miaka mingi sana kuipndoa".

Watanzania katika serikali za awamu ya 1, 2,3 na 4 kidogo walikuwa watu wanaozifahamu haki zao na wakati mwingine walithubutu kuzidai kwa nguvu walipoona zinacheleweshwa na wenye mamlaka.

Ila tangu Magufuli aingie madarakani ile style yake ya kuwaminya waliojaribu kuinunua shingo zao imeleta athari kubwa kwa Watanzania.

Sasa hakuna mtu tena wa kuweza kuipinga serikali kwa vitendo.
Watanzania wamepandikizwa woga.

Nakumbuka mkwara aliowapigia wanafunzi wa UDSM endapo wataandamana, naukumbuka mkwara aliopigwa Majaliwa endapo ndugu zake wataandamana.

Na kumbuka pale alipokuwa akitumia neno fyokofyoko akimaanisha uchochezi.
Watumishi walikuwa wapole kwa miaka yote 6 huku wakisubiri Mungu aongee na Rais juu ya hatma yao.

Hii hofu haitafutika hivi karibuni. Si mmeona tozo zilivyoingizwa kikatili ila wananchi wakaishia kulia mitandaoni tu.
Alipoamrisha Tundu Lissu apigwe risasi akiwa kwenye kikao bungeni ndipo niliamini kuwa kiwango cha kichaa cha Magufuli kiko juu sana na alistahil kuwa Wodini Mirembe Hospital
 
Hayo ni yako mtoa mada.. Kwangu mimi Hayati JPM anaishi.. Na Nabii aliyekuja kwetu kutufumbua macho na kutuonyesha kuwa watanzania tunaweza kuendeleza nchi yetu bila utegemezi wa nchi za magharibi.. Ni nabii aliyekuja kutufundisha umuhimu wa kufanya kazi na kuipenda nchi yetu.. Ni Nabii aliyekuja kwetu kutuonyesha kuwa watu wanaoishi kwa wizi wa ujanja ujanja wanadhibitika.. Ni Nabii aliyekuja kwetu kutufundisha jinsi Taasisi ya Urais inavyotakiwa kufanya kazi.. Na kama ilivyo ada, manabii wengi huwa hawaishi muda mrefu na jamii zao.. Kaongoza kipindi kimoja akitamani kumalizia kipindi cha pili, lakini mMwenyezi Mungu akamwambia kijana wangu inatosha.. Njoo upumzike.. Nasi tuliomuelewa tutamkumbuka daima.. Na jina lake litaishi vizazi hata vizazi...
It is totally INSANE kumshabikia mtu anaiba kura zote za Serikali za Mitaa mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020 na anaweka wabunge anaowataka yeye. Bado misukule yake kama St. Paka Mweusi inatujazia pumba humu.

Mtu MWONGO amayesema anajenga kwa kodi za ndani wakati anakopa, mtu anaysema hawezi kupeleka maendeleo kwenye majimbo yenye wabunge wa upinzani. Anayetumia raslimali za Taifa kujenga miundombinu mikubwa kama Airport kijijini kwake. Mwizi na muuaji ndiyo taswira ya Magufuli itakayobaki
 
Mbowe anasema ukidai Katiba Mpya ni siasa zisizo za kistaarabu.

Ameamua kufanya siasa za kistaarabu baada ya kunywa chai ikulu na kupewa bahasha ya khaki. [emoji16]
Mbowe ni mmoja tu katika Watanzania milioni 60, katiba mpya ni kwa ajili yetu wote tunaotaka nchi bora zaidi kesho kuliko hii ilivyo leo ni kwa ajili ya faida ya watoto na vizazi vyetu vingi vijavyo pia.
 
Back
Top Bottom