GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Katika hizo Nyimbo za Masuwa na Ndombolo ndipo Watu waliujua Uwezo mkubwa wa Kughani au Kurapu ( Wakongo wanaita Atalaku ) aliokuwa kuwa nao Mwalimu wa Marepa ( Atalaku ) wa Kizazi cha Pili aitwae Tutu Calugi ( jina Kamili Yombo Lumbu ) kwani alizinogesha vilivyo hizi Nyimbo.1. Masuwa
2. I love you
3. Ndombolo
4. Cavalier Solitaire
Hizi nyimbo kusema na ukweli hata kama sina fedha hua nahisi nina pesa,pindi ninapoanza kuzisikia!
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Nimefurahi mno Mkuu kujua kuwa nawe ni mwana Wenge BCBG yake JB Mpiana. Nataka niwajue na JF Members wengine waipendao hii Bendi kama Sisi.
Ndiyo maana Congo DR nzima wanakuambia hii si Bendi tu bali ni Mashine ya Muziki kabisa Mkuu.Ngoma zake zikipigwa ukiwa bar bia hunoga zaidi
Mpaka leo bado sijaona Wimbo wa Kuupiku uitwao Kine Bouger ( yaani Kinshasa inatingishika ) ambapo Mghani au Rapa ( Atalaku ) Mwandamizi aitwae Roberto Wunda Enkokota aliutendea vyema kabla ya kumuachia Jukumu la 'Kurapu' Mwalimu Tutu Calugi na Yeye ( Roberto ) kwenda Ufaransa kutibiwa Koo lake ambalo ndiyo lilizima kabisa Safari yake ya kuwa Rapa ( Atalaku ) wa Wenge BCBG yetu hii Mkuu.BCBG for life, taja nyimbo zote lakini Kama hakuna Kalayi Boeing hiyo siyo Wenge ni Mawenge.
Nipe tofauti ya Wenge Musica na Wenge BCBGTafadhali naomba ukiwa kama mwana Wenge BCBG yake JB Mpiana uniambie ni kwanini Nyimbo hizi Nne zifuatazo haziishi Utamu na wala hazichuji miaka nenda rudi?
1. Champion Kapangala ( Sebene )
2. Omba ( Rhumba )
3. Wallah Danico ( Sebene )
4. Sans te Toucher ( Rhumba )
Kama una 'updates' zozote za kuihusu Bendi hii yetu pendwa ya Wenge BCBG yake JB Mpiana tafadhali karibu utupatie kwani hii Bendi ambayo Mbinguni kwa Mungu Baba inapendwa na imebarikiwa kabisa.
Wenge BCBG ni Mashine ya Muziki hasa!
Ndiyo Wimbo bora wa Rhumba ( Mziki wa taratibu ) ambao umemfanya JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG Kupendwa, Kukubalika na kuwa Tishio Congo DR nzima na huku Kwingineko.Mimi sijui ata kwa nini nikiusikia ule wimbo uitwao OMBA nasuuzika mno moyo mkuu
Hiyo namba 4 aliyepiga gitaa peponi moja kwa moja! Sijui ni Allan Makaba!?1. Masuwa
2. I love you
3. Ndombolo
4. Cavalier Solitaire
Hizi nyimbo kusema na ukweli hata kama sina fedha hua nahisi nina pesa,pindi ninapoanza kuzisikia!
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Japo kuna kina Suzuki 4×4, Bill clinton n.k Huyo Roberto Ekokota sijui kama kuna rapa yeyote anagusa hapoMpaka leo bado sijaona Wimbo wa Kuupiku uitwao Kine Bouger ( yaani Kinshasa inatingishika ) ambapo Mghani au Rapa ( Atalaku ) Mwandamizi aitwae Roberto Wunda Enkokota aliutendea vyema kabla ya kumuachia Jukumu la 'Kurapu' Mwalimu Tutu Calugi na Yeye ( Roberto ) kwenda Ufaransa kutibiwa Koo lake ambalo ndiyo lilizima kabisa Safari yake ya kuwa Rapa ( Atalaku ) wa Wenge BCBG yetu hii Mkuu.
Itutu Caluji na mpiga gitaa walikuwa nyota Wa mchezo! Lile gitaa linapelekwa huku linarudishwa huku hatariiiTitanic na Kuna Ile kaimba na marehemu papa Wemba aiseeh Ile ngoma sijawahi kuichoka sauti zilipangwa zikapangika..
Huo Wimbo aliouimba na Papa Wemba unaitwa Cavalier Solitaire.Titanic na Kuna Ile kaimba na marehemu papa Wemba aiseeh Ile ngoma sijawahi kuichoka sauti zilipangwa zikapangika..
Ni kweli katika Wimbo huo Lead Guitar la Solo alipiga Alain Makaba 'Prense' na Second Guitar alipiga Burkinafaso Mbokaliya.Hiyo namba 4 aliyepiga gitaa peponi moja kwa moja! Sijui ni Allan Makaba!?
Alikuwa akiitwa Roberto Wunda Enkokota ila sasa anaumwa Saratani ( Cancer ) ya Koo na yuko nchini Ufaransa.Hivi rapa Wa Kallai Boeing ile OG ni nani!? Huwa natamani ningekuwa studio nimuone wakati anaghani
Rapa aliye Tishio kwa sasa ni GENTAMYCINE ( Pitshou Lisimo ) wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana japo hata akina Bill Clinton ( Mukeba Kalondji ) pamoja na Gesac aliyekuwa akirapu kwa Felix Wazekwa kabla hajahamia kwa Koffi Olomide na Bendi yake ya Quarter Latin ambapo alifanya Kazi kubwa katika Album ya Monde Arabe hasa ule Wimbo mtamu wa Respect.Japo kuna kina Suzuki 4×4, Bill clinton n.k Huyo Roberto Ekokota sijui kama kuna rapa yeyote anagusa hapo