Nikiwa mtaani nitamjuaje mtu kuwa huyu ni member wa JF. Naombeni dalili!

SubiriJibu

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2009
Posts
1,805
Reaction score
1,876
Wote humu tuna ID na hatujuani ukiachilia mbali wale wanaojulikana yaani verified.. Nasemea ID za kujificha kama zetu hizi

Lakini mtaani haipiti siku tunaiongelea JF. Tabu ni kwamba kila tunapoongea mtaani hakuna anayeonyesha dalili kwamba yeye ni member.

Hivyo unaweza kujibizana na mtu humu kumbe mnakunywa naye beer kila jioni.

Nawapa stori moja.

Mtoto wa mjomba wangu mwaka 2011 niliona computer yake ina matatizo na nikamsaidia. Sasa ilikuwa wazi mno akajisahau akawa anatuma post humu JF, siisemi ID yake na nikaiona.

Hakujua nimeona ID yake na siku hiyo alikuwa anatuma kuonyesha matatizo ya chuoni kwake nacho sikitaji.

Basi nikaikariri ID yake nikawa nafuatilia post zake humu JF.

Kimsingi alifaulu sana kukisumbua kile chuo kupitia JF. Maana madai yao yalielezwa vizuri humu JF hadi watawala wa chuo wakanywea na Tanzania nzima ikajua matatizo ya chuo hicho.

Sasa baada ya mwaka mmoja nikamtumia message kwenye simu kumtania kwa kumuita kw ajina la ID yake ya humu JF.

Mfano, kama ID yake ni Chungasana, nikamwita "vipi Chungasana unasemaje?"

Eeeh bwana akaruka, akanijibu "Chungasana ndiye nani".

Sikutaka tena kumuuliza nikajua kuwa hata ndug yako akiwa na ID ya JF hataki umjue.

Je, wenzagu mlishawahi kumjua mwenzenu wa JF hata kwa kuhisia?
 
Nakumbuka kuna mama mmoja makao makuu TTCL, ndo alianzamaana kuniweka mawazo ya Jf then
 
Mimi na marafiki kibao humu ndani japokuwa sitaki kuwataja wengine kila siku tunaonana nao
Marafiki wa ubungo gonga like hapa Kama unanijua
Marafiki wa tabata gonga like hapa Kama unanijua
Marafiki wa kimara gonga like hapa
Marafiki wa kkoo
Nadhani mnajijua gongeni like hapa
 
Kabla ya kuwa na ID hii ya Sigara Kali,nilikua na ID fulani ambayo mwisho iligundulika na college mate wangu wa chuo baada ya siku moja kuniita a.k.a yangu ya chuo ,nikaona huyu jamaa anataka kuniletea mazoea,nikabadili ID
 
Mmetangaziwa leo!
Wana JF wooote mtakao kamatwa mtaenda kufungiwa kwenye uwanja wa Karume Arusha... 😛 😀 😳
 

Ita tu mkuu akigeuka ujue anatumia jf mbane akupe id yake
 
Wagonge like wajulikane?[emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Kabla ya kuwa na ID hii ya Sigara Kali,nilikua na ID fulani ambayo mwisho iligundulika na college mate wangu wa chuo baada ya siku moja kuniita a.k.a yangu ya chuo ,nikaona huyu jamaa anataka kuniletea mazoea,nikabadili ID
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mimi mwenyewe nimebadili jina tu ,kuna mtu niliona analetea ujuaji .Huku jamvini anaye jua nilibadili jina ni mwanamke mmoja hivi tu wa Geita.

Sitaki mtu anifahamu kwa sasa ,Mtu akinifahamu ,naunda ID nyingine .

Labda mtu anifahamu kwa kupenda kwangu.
 
sio rahisi kufahamu mpaka uwe mtu wa karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…