Wote humu tuna ID na hatujuani ukiachilia mbali wale wanaojulikana yaani verified.. Nasemea ID za kujificha kama zetu hizi
Lakini mtaani haipiti siku tunaiongelea JF. Tabu ni kwamba kila tunapoongea mtaani hakuna anayeonyesha dalili kwamba yeye ni member.
Hivyo unaweza kujibizana na mtu humu kumbe mnakunywa naye beer kila jioni.
Nawapa stori moja.
Mtoto wa mjomba wangu mwaka 2011 niliona computer yake ina matatizo na nikamsaidia. Sasa ilikuwa wazi mno akajisahau akawa anatuma post humu JF, siisemi ID yake na nikaiona.
Hakujua nimeona ID yake na siku hiyo alikuwa anatuma kuonyesha matatizo ya chuoni kwake nacho sikitaji.
Basi nikaikariri ID yake nikawa nafuatilia post zake humu JF.
Kimsingi alifaulu sana kukisumbua kile chuo kupitia JF. Maana madai yao yalielezwa vizuri humu JF hadi watawala wa chuo wakanywea na Tanzania nzima ikajua matatizo ya chuo hicho.
Sasa baada ya mwaka mmoja nikamtumia message kwenye simu kumtania kwa kumuita kw ajina la ID yake ya humu JF.
Mfano, kama ID yake ni Chungasana, nikamwita "vipi Chungasana unasemaje?"
Eeeh bwana akaruka, akanijibu "Chungasana ndiye nani".
Sikutaka tena kumuuliza nikajua kuwa hata ndug yako akiwa na ID ya JF hataki umjue.
Je, wenzagu mlishawahi kumjua mwenzenu wa JF hata kwa kuhisia?