Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
NITAKAPO KUWA RAIS, SAME ITAKUWA MKOA.
Na, Robert Heriel
Najua haina vigezo, najua wapo watakaonipinga, nafahamu kelele nitakazo pigiwa. Lakini sitajali. Same lazima iwe Mkoa.
Kila Rais akiingia Madarakani afanye Mji wake au wilaya atokayo kuwa Mkoa, ikiwezekana aweke ndio yawe makao ya nchi.
Si ndivyo mnavyotaka. Wala siwapingi wekeni Mkoa ikiwezekana wekeni mpaka makao makuu ya nchi.
Taikon nikiingia na Mimi naipandisha wilaya ya Same kuwa Mkoa, na nitajenga Uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa, hata mlie Kama Mbuzi meee! Sitajali la mtu Mimi.
Na wewe kutoka Lushoto ukichukua Nchi, fanya utakavyoona, Weka Mkoa WA Lushoto.
Wa Mpwapwa weka Mkoa WA Mpwapwa
Wa Kazulamimba sijui Makete pandisha mikoa.
Hata Mimi Nina mapenzi na kwetu.
Hata Mimi nataka kwetu pawe na maghorofa
Hata Mimi nataka kwetu pawe na Uwanja mkubwa wa ndege. Hata Kama hakuna timu kubwa Mimi sijui Hilo, lazima nijenge Uwanja pale.
Najua Same ni pakame Sana lakini nitapeleka Mbuga mbali na Ile hifadhi ya Mkomazi.
Nitapeleka Bandari pale hata Kama hakuna bahari.
Nitaiga yote niliyoyaona Kwa watangulizi wangu.
Wala sitaleta katiba mpya Mimi. Kwani ninyi mnakula katiba. Litakuwa jeshi la mtu mmoja sitaki lakuambiwa Mimi. Si mlinichagua wenyewe.
Same lazima iwe Mkoa labda patokee mabadiliko msinichague.
Lakini hata msiponichagua na Same yangu isipokuwa Mkoa najua Maeneo mengine yatakuwa mikoa.
Rais akitoka Kilolo ataweka Mkoa wa Kilolo.
Akitoka Matombo, ataweka Mkoa wa Matombo
Akitoka Nzega ataweka Mkoa wa Nzega.
Litakuwa Taifa lenye mikoa Buku.
Zàmu Kwa zàmu.
Wenye akili watende Kwa akili, wapumbavu wafanye upumbavu.
Wenye Hekima huiangalia kesho lakini wapumbavu huiona Leo tuu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa MOROGORO