Nikiwakumbuka akina John Guninita, Sukwa Saidi Sukwa, James Mbatia nashindwa Kabisa kuwalinganisha na Vijana wa sasa

Nikiwakumbuka akina John Guninita, Sukwa Saidi Sukwa, James Mbatia nashindwa Kabisa kuwalinganisha na Vijana wa sasa

Kiukweli Siasa za Tanzania zinazidi kufubaa hasa kwa vijana wetu kama utalinganisha na enzi za akina Guninita

Sijui kwanini Vijana wetu wa Leo hawana Uwezo Kabisa wa Kujenga hoja zaidi ya kuropoka ropoka tu

Yaani Leo Lucas na Mchungaji Msigwa ndio tegemeo la CCM, Pambalu na Boni Yai ndio tegemeo la Chadema na yule aliyejiteka mh Nondo ndio tegemeo la ACT Wazalendo

Siasa za Bongo ziko ICU kwa kweli

Baadae Mlale Unono 😀
Wanaogopa kutekwa, kutwaliwa na kupotezwa ama kumwagiwa tindikali. Chaajabu watekaji hujitambulisha wao ni akina nani, na wanakuwa na vifaa vya kutosha walioshiba, (watekaji ni vikosi vilivyo kamilika), hao wote uliowataja wamepitia shuruba mbalimbali ambazo zimewaongezea ujasiri

Kwani wewe huogopi?
 
Upo sahihi kabisa, viwango vya akili vinashuka sana kwa vijana wetu sio kwa wanasiasa tu wa uvccm ni taifa zima across all areas, nafikiri kuna haja ya kufanya utafiti zaidi wa malezi na hasa kwenye chakula, naamini (literary) labda kwa sababu tunakula ugali😎 kama chakula kikuu, tunadumaa sana akili na mwili! Tazama pia physical structures za vijana wa kisasa, utafikiri watoto na kilo zao kama za mbuzi. Linganisha na waganda, wakenya na ukienda mbali zaidi West Africa, utaona watanzania ni kama mbilikimo tu.

Ukitazama trends za performance ya shule zote na vyuo utaona inapanda generally lakini tazama outcome ya elimu kwenye maendeleo ya taifa ndio utajua jinsi tulivyo. Tuna madaktari wenye phd lkn ni machawa, maengineer wasioweza hata kudesign kiosk, tuna madaktari wanaogoogle dawa wawape wagonjwa, tuna 1st class wachumi wanaojua kupandisha thamani ya shilingi ni kukopa na sio kuongeza mauzo nje. Maprof wanaoogopa hoja na hawafanyi tafiti wanasubiri teuzi, hata sijui wanafundisha nini huko vyuoni, matokeo yake jamii butu inayoishi kwa uchawa na kutegemea kuimport maendeleo toka kwa wachina. Kutwa kuwasifia. Pathetic
 
Upo sahihi kabisa, viwango vya akili vinashuka sana kwa vijana wetu, nafikiri kuna haja ya kufanya utafiti zaidi wa malezi na hasa kwenye chakula, naamini (literary) labda kwa sababu tunakula ugali kama chakula kikuu, tunadumaa sana akili na mwili! Tazama pia physical structures za vijana wa kisasa, utafikiri watoto na kilo zao kama za mbuzi. Linganisha na waganda, wakenya na ukienda mbali zaidi West Africa, utaona watanzania ni kama mbilikimo tu.
Tuliandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuhoji linaanza kwenye ngazi ya famlia kuna vitu ukihoji utaambiwa kama umekuwa uondoke, hii tabia ya kukataa kuhojiwa jamii imelichukua na kuishi nalo kwenye ngazi zote za maisha na ndiyo maana mlipo hoji kuhusu tozo mliambiwa muende burundi, tukakaa kimyaaa, (fyata mkia)

Kuhusu washika tonge hawa wakiona una hoja za kuwanyang' anya matonge yao wanakushughulikia, (ostracism), they will deal with you perpendicularly

Kuhusu ushirikishwaji kwenye mambo yanayo husu sera na mengineyo yaani yanayohusu jamiI, wahusika wa mipango hiyo wanaweza kuamua kuwashirikisha wananchi ama kutofanya hivyo na hili nalo naliwekea alama?, maranyingi sera na mipango bila ushirikishwaji wa wadau na wananchi mapokeo yake huwa ni hasi madhara yake ni sera ambazo hazina muelekeo (uncertainty policy)
 
Tuliandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuhoji linaanza kwenye ngazi ya famlia kuna vitu ukihoji utaambiwa kama umekuwa uondoke, hii tabia ya kukataa kuhojiwa jamii imelichukua na kuishi nalo kwenye ngazi zote za maisha na ndiyo maana mlipo hoji kuhusu tozo mliambuwa muende burundi, tukakaa kimyaaa, (fyata mkia)

Kuhusu washika tonge hawa wakiona una hoja za kuwanyang' anya matonge yao wanakushughulikia, (ostracism), they will deal with you perpendicularly

Tena inaanzia kwenye level ya familia kabisa! Hakuna mtu mwenye mamlaka anayekubali kuhojiwa, kaka hataki mdogo ahoji, baba hataki yeyote ndani ya familia ahoji chochote, ikaenda kwa mapadri, maaskofu, mashekhe, viongozi, waalimu maeneo yote, ukihoji unadisco, jamii nzima sasa haitaki kuhojiwa hata kwa majukumu yao, leo ukihoji utendaji wa kiongozi unapoteza kazi, ukahoji polisi ujue maisha yako yanakuwa hatarini ukihoji rais ndio kabisa unashambuliwa kuanzia na machawa hadi vyombo vyote vya dola. Kila mtu anataka kusifiwa sio kuwajibika
 
Daaaa tumetoka mbali sana.....kujua historia nzuri sanaaa.......kweli bijeba vile viko wapi ??Kasapira Guninita Sukwa etc......
 
Sasa hivi vijana wamejawa hasira na matusi akileta hoja yake anataka wote muiunge mkono ukimbana maswali mawili matatu anakuambia wewe umetumwa na ccm mwishowe utaishia kutukanwa, sijui role model wao ni nani? Miaka ya 2000 hadi 2015 angalau kulikuwa na vijana wajenga hoja ila baada ya hapo sijui vyama vya siasa hasa upinzani wamefeli wapi yaani wamekuwa na vijana wenye hasira hasira na matusi sijui wamewaanda kumuongoza nani.
 
Kiukweli Siasa za Tanzania zinazidi kufubaa hasa kwa vijana wetu kama utalinganisha na enzi za akina Guninita

Sijui kwanini Vijana wetu wa Leo hawana Uwezo Kabisa wa Kujenga hoja zaidi ya kuropoka ropoka tu

Yaani Leo Lucas na Mchungaji Msigwa ndio tegemeo la CCM, Pambalu na Boni Yai ndio tegemeo la CHADEMA na yule aliyejiteka mh Nondo ndio tegemeo la ACT Wazalendo

Siasa za Bongo ziko ICU kwa kweli

Baadae Mlale Unono 😀
Guninita anatofauti gani na Msigwa?
 
Kiukweli Siasa za Tanzania zinazidi kufubaa hasa kwa vijana wetu kama utalinganisha na enzi za akina Guninita

Sijui kwanini Vijana wetu wa Leo hawana Uwezo Kabisa wa Kujenga hoja zaidi ya kuropoka ropoka tu

Yaani Leo Lucas na Mchungaji Msigwa ndio tegemeo la CCM, Pambalu na Boni Yai ndio tegemeo la CHADEMA na yule aliyejiteka mh Nondo ndio tegemeo la ACT Wazalendo

Siasa za Bongo ziko ICU kwa kweli

Baadae Mlale Unono 😀

Tofautisha siasa za zamani na za sasa ,siasa za sasa zinahitaji watu kama kina Boni yai,zinahitaji watu kama Sumu ya Nyigu 7x70 Mdude ,siasa za sasa zinahitaji kupiga kwenye mshono hakuna kona kona ,hakuna kurembesha...Watawala wa sasa ni madikteta/watekaji/wauaji siasa nyepesi haziwastui.
 
Back
Top Bottom