Nikki wa Pili ayape heshima mavazi ya kitaaluma. Achague kuwa PhD holder ama abaki na swagger zake za kisela

Wa Arusha huwa hakosei Mkuuu, Subir povu la Mabilionea wa Arusha mpaka utashangaa.
 
Hawezi kurudi hapa huyo kijana
 
Kama Mwakmango ana PhD unashangaa nini?
 
Unamchukuliaje mtu kama Magufuli mwenye PhD anaekaa meza moja na Prof Kabudi, na maDr wengine halafu unamkuta akipanga mikakati ya nchi na kina Musukuma, Kibajaji, Makonda?
Kwa maana nyingine mleta uzi asi-complicate maisha..siku zote elimu ya darasani inategemea zaidi elimu ya mtaani kwa kuwa hata usome vipi mwisho wa siku utakaowahudumia ni hao hao wananchi wa kawaida na masela pia
 
mavazi na phd vinaundugu gani ? tuanzie hapo.

Then kati ya prof lipumba mweny degree nying na king msukuma mbunge aliyeishia darassa la saba nani mweny impact kwa Jamii.
 
... kwa vile mtu ana PhD lakini anamiliki karakana ya kutegenegza magari, eti asivae ovaroli yenge madoadoa ya grisi na oil wakati wa shughuli za karakana yake.....Duh!!
 
PhD IPO kichwani sio kwenye mavazi.
Kwanini wanakataza Kata K mashuleni, na mpaka kuna nguo wanakataza kuvaa vyuoni kwa sasa. Why doing that kama elimu ipoo kichwani tuu?
 
kwani kwako PHD ni nini mkuu?
OGOPA SANA KUTAFSIRIKA KWA USICHOKUWA NACHO WAKATI UNAOGA!

magari
elimu
nyumba
pesa
mke/mume
watoto
HAWAKUFANYI UWE WEWE!
kama huna identity ambayo haikamiliki bila kubebwa na nilivyotaja hapo juu ,UMEKUFA mzee baba!
 
Mbona sawa tu mana yy hatumiii elimu kama mwavuli bali kama torch ya maendeleo sasa mm sioni shida hapo mavazi ni phinotipical things na PHD ni genotipical so these are two separate things which can be done together.
 
Hivi ukiwa na PHD unatakiwa ufanyaje labda au ugombee ubunge tu ha ha ha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…