Niko dillema, mchumba wangu ni mchawi!!!

Mtoto wa nyoka ni nyoka, LAKINI MTOTO WA TAJIRI ANAWEZA KUWA MASKINI WA KUTUPWA! Listen brother, kama huyo binti ni mchawi, utagundua tu, na pia kama si mchawi utajua tu. Believe me, unaweza kuwa safe sana na mtu aliyetoka kwa wachawi lakini yeye ana negative attitude na uchawi!
 
Hivi wewe unajua uchawi??? angekuroga hata hapa usingekuja kuuliza swali kama hili, na kama kweli mchawi basi sasa hivi keshapata alarm fulani unamteta humu, na ole wako ukutane nae leo utakoma......hahahahaha hakuna kitu kama hicho
mamaaa, ila siogopi hawezi kuwa na hisia yeyote, uchawi wa huko kwao bado unadaiwa ni ule wa kutembea na fisi.
 
Fanya utafiti wa kina kuhusiana na taarifa ulizozipokea baada ya kuzithibitisha achana naye lkni kwa muda huu usioneshe ishara zozote mbaya kwa huyo dada kwani huna hakika kwa shut uma ulizozisikia
asante bosi.
 
thank you broda
 
Hizi mada zingine bana!
E bana we sharo kuna mwenzio anaitwa hand some kule anatafuta mchumba naona we mtaendana
 
Hizi mada zingine bana!E bana we sharo kuna mwenzio anaitwa hand some kule anatafuta mchumba naona we mtaendana
hapana bana, we mbona unataka kunifanisha na watu wanajisifia wenyewe? Yule mara aseme eti anaitwa hendsum na wanaume wenzie mara sijui nini, so we huoni kama niko tofauti, mi nimeingia pabaya bwana, niambie namna ya kutoka humu.
 
Dah! Suali gumu. So we unataka niendelee nae kisa yeye asije akakosa mpenz au?

Akose mpenzi kwani mwanaume umebaki wewe peke yako duniani?Atapata watakayeendana kisera!

Nashangaa mpaka sasa bado unahoji,umesikiliza ushauri wa watu wengi humu,masuala ya uchawi unajua ni ya kufikirika zaidi.Tuliza akili yako,tafakari uliyoshauriwa kisha chukua hatua.

Kama uko serious unatafuta mwenza wa maisha.........acha mzaha...........inaelekea umeleweshwa na urembo wa bibie,ukithibitisha hizi tuhuma jinasue haraka sana kaka.
 
dah, umeongea kwa jazba sana. Mtoto kiukweli kanizimisha, mhhhh! Ngoja nijaribu naamini kama ananipenda hataniroga hata kama angekuwa mchawi.
 
Kama anakupenda we hofu yako ni nini? Shukuru utapata mtoto mchawi hahahahaha!
 
Kama anakupenda we hofu yako ni nini? Shukuru utapata mtoto mchawi hahahahaha!

Mpaka huyo mtoto aje kuzaliwa,na baba yake atakuwa mchawi tayari!................si unajua kupenda kukipitiliza..............kila kitu ..........yes babe!
 
Mpaka huyo mtoto aje kuzaliwa,na baba yake atakuwa mchawi tayari!................si unajua kupenda kukipitiliza..............kila kitu ..........yes babe!
sidhani, kama ikitokea ni mchawi kweli na tukaishi wote pamoja, sidhani kama anaweza kuniteka hadi mawazo kiasi kwamba niitikie kila kitu yeh! Nitaishi kwa machale.
 
Nahisi umempa ushauri mzuri sana uliotakiwa apewe!Hofu aondoe ajichukulie jiko lake kama kweli anauhitaji
 
sidhani, kama ikitokea ni mchawi kweli na tukaishi wote pamoja, sidhani kama anaweza kuniteka hadi mawazo kiasi kwamba niitikie kila kitu yeh! Nitaishi kwa machale.

Kumbe hata kama ni mchawi kweli unaweza kuishi naye eeh?..............................................teh teh teh................joking

Sasa wewe unachohofia hasa ni yeye kuwa mchawi au mama yake kuwa mchawi....au vyote?
 
Weka picha kwanza
 
Kwani mpaka sasa bado watu wanaamini kuna uchawi? Jamani mtu akifa inakua mkataba wake wa hapa duniani umekwisha mengine yote sababu2,usiache kupenda umpendae kisa mchawi mulize ivi Eti wangu wewe mchawi manake watu wanasema hivyo, atakupa jibu
uchawi upo na unaua,sangoma pia ipo kama huamini ipo siku utaamin,mm namshauri azingatie pia maneno ya watu afanye evaluation,ukipuuza utaumia,utaamia Gamboshi soon..
 
Kumbe hata kama ni mchawi kweli unaweza kuishi naye eeh?..............................................teh teh teh................jokingSasa wewe unachohofia hasa ni yeye kuwa mchawi au mama yake kuwa mchawi....au vyote?
wasiwasi wangu ni kwamba anaweza kupewa urithi na mama yake afu aje anifanye kama alivyofanywa babaake kutokana na za mtaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…