Niko dillema, mchumba wangu ni mchawi!!!

Niko dillema, mchumba wangu ni mchawi!!!

wasalaam MMU!

kama ni kuchanganyikiwa ndo nahisi nachanganyikiwa!!
Katika pitapita zangu na kujituma kwangu kumsaka mchumba ambae ni mzuri nilibahatisha kumpata mtoto wa makabila mmojawa maarufu sana ktk mkoa wetu wa Arusha.
Mtoto mwenyewe si haba, mtoto mweupeee!!
Mtoto wezereee!!
Mtoto unywele!!
Mtoto smile!!
Mtoto meno meupeee!!
Mtoto mguu!!
Dahhhh!!

na kiukweli nilikuwa nikipita nae kila mahali masela nilihisi kama kuna ka uhasama mfali, kina dada walininunia bila sababu kisa kuwaambia ukweli kuwa my hny yre(wayre nilipenda kumwita hivo) kauteka moyo wangu na naahidi kumpenda kwa dhati!!!

Looo! Kuna taarifa ambazo nimeanza kuzipa kutoka kwa marafiki zangu wa mtaani kwao kwamba ile familia ni issue, mama wao aliwahi kumuua mumewe na 7bu zingine kibao zikiwa ni pamoja na kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume majirani zao!!

Sasa mi nitafanyeje? Kama hizi taarifa ni kweli nikijifanya naendelea nae nitaishia wapi?

Naombeni ushauri wenu wapenzi wenzangu wa jf hasa MMU.

ahsanteni.
Hii nilichelewa kuiona yote uliyozungumza ni kuhusu mama sijaona kosa la kisura wetu Wayre,nakuaminia mkuu hapa vijana wa street wanataka kukupiga bao la kisigino akili kumkichwa mkitembea mkishikana mikono na Wayre.
 
mmh! Tunaanza kupewa vyandarua halafu vyupi. Kompyuta hadi mwaka 3011.
vyandarua vyenyewe vimegundulika kupunguza fertility tumia visivyo na dawa na vyupi si vimepitwa na wakati hahaha!
 
Usimwite mtu usiku huu tutahangaika wenyewe usijali,kwenye taarab wanasema 'ye aweze ana nini,we ushindwe una nini' lol!
akaa babu wewe, taarab ya mabonge mi sio bonge. Hahahaha! Nipo kwenye course ya mipasho, vipi naweza weza eeh?
 
akaa babu wewe, taarab ya mabonge mi sio bonge. Hahahaha! Nipo kwenye course ya mipasho, vipi naweza weza eeh?
ukija dar ntakupeleka ukamwone Mzee yusuf siku hizi anatumbuiza maisha Club jumatano sio uswaz.
 
Back
Top Bottom