KERO Niko Gerezani dakika 20, hakuna basi la Mwendokasi hata moja

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Aramun

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
461
Reaction score
2,213
Imagine unakaa dakika 20 huoni gari ya kuelekea unakoenda, na unatumia usafiri tuliotangaziwa kwa mbwembwe na bashasha kwamba ndiyo mkombozi wa shida ya usafiri.

Kwa hali hii, serikali iruhusu daladala kama kawaida kwa zile route ilizoondoaga daladala kama Kimara hadi Gerezani na Kivukoni.

Huwezi kukaa kituo chochote cha daladala zaidi ya dakika 3 bila daladala kupita, ila ni rahisi kukaa hata nusu saa kituo cha mwendokasi bila gari hata moja kupita.



 

Attachments

  • IMG_20240403_180306.jpg
    3.3 MB · Views: 2
Kuna siku nilikuwa pale manyanya mwendokasi nilikuwa nawahi kivukoni nilisubiria sana gari bila mafanikio kuna jamaa nilikuwa nae yeye alipanda daladala zetu hizi akanipigia yeye ameshafika anasubiria panton avuke kwenda kigamboni mie bado nipo stand manyanya hapo ndio ilikuwa mara ya mwisho kupanda mwendokasi nadhani inafika miaka 3 sasa kama nina haraka huwa naona Bora nitafute njia nyingine ila sio mwendo kasi
 
Mara ya mwisho kupanda mwendokasi ilisiku siku ya majaribio
 
ukashindwa kujiongeza
mkuu fala kweli wewe 😆 😆
 
Ubaya ni kwamba Morogoro Road waliondoa daladala, kwa hiyo hakuna option nyingine zaidi ya bajaji au pikipiki ambazo ni ghali..

Warudishe tu hizo route za daladala ili tuwe na options nyingi..
 
Serikali inayokimbilia kukusanya mapato kwa kusajili magruop ya WhatsApp unafikiri kuna nini hapo ?
 
Serikali ya wapumbavu na raia wapumbavu
 
Chochote kinachoendeshwa na serikali kimelaaniwa. Hadi pale mifumo yenye kufuata muongozo wenye nidhamu itakapotengenezwa upya
 
Vuteni subra, mwekezaji anakuja kuwakwamua.
 
MAJINA YANAUMBA, USIWE UNASUBIRI BUS GEREZANI MAANA WATAKU-TREAT KAMA MFUNGWA
 
Kwani honda click sh ngapi? Mnapakana majasho na watu mwishowe upate magonjwa ya ngozi
 
Mpigieni waziri ili ampigie simu Kihamia Kama walivyofanya wenzenu kule kivukoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…