Karikenye
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 564
- 280
Nimeona niombe Ushauri wenu wa dhati kuhusu hili;
Nina Mpenzi wangu ambaye anajua nampenda sana nami vilevile nampenda sana.
Kisa ni Hiki kifuatacho:-
Siku moja ndani ya Mwezi wa June, Mpenzi wangu alinipigia simu usiku na kwa bahati mbaya sikupokea simu yake kwa sababu nilikuwa nimelala hivyo baada ya muda mfupi akatuma sms iliyokuwa na maswali kibao na magumu ambayo sikuweza kupata majibu ya haraka haraka kama alivyotaka nimjibu na hili ndo limenipelekea kuomba ushauri toka kwenu. Message hiyo ilisomeka kama ifuatavyo:-
Naomba unijibu kwa ufasaha kutoka moyoni mwako
Meseji hii ilileta shida na mpaka sasa tuko katika mgogoro mkali sana maana mimi nilireact kwa Nini asiniulize nini kimesababisha nisipokee simu yake yeye akaniuliza maswali ambayo majibu yake anayo???
- Je uko tayari na umeridhika kuwa nami kama mkeo Mtarajiwa?
- Unanipenda kweli?
- Uko tayari kunioa?
- Haunidanganyi?
- Umenipenda jinsi nilivyo pamoja na udhaifu nilio nao? Please naomba majibu
Nawaombeni mnisaidie ili tuondoe kutokuelewana tulikonako.
Kwani ungemjibu ndio ungepungukiwa nini? In short hivyo ndivyo wanawake walivyo awe graduate au darasa la saba hiyo inaitwa FEMINISM it is genentically coded they are so by default!!