Wana JF,
Mkoa wa Kigoma unawakilisha jamii ya WTZ ambao wameathirika sana na tawala zilizopita. Kama wanaJF, hakuna haja ya kuanza kubeza mkoa wa kigoma bali tueleze ukweli ili tawala zilizopo zielekeze nguvu za ziada katika mkoa wa kigoma na mikoa mingine inayofanana nayo. Mhe. Jk, alipoingia madarakani, yeye aliahidi kuinua mikoa ambayo aliita mikoa ya 'PEMBEZONI', maana yake mikoa iliyosahaulika kimaendeleo. Sasa sijui kama kweli Jk anafanya kama alivyoahidi.
Kwa wanaobeza kwamba kigoma iko nyuma kimaendeleo, isingepaswa kuwa nyuma. kigoma inautajiri wa kutisha: ni mkoa unaolima michikichi, wote mnajua products za michikichi ikiwemo korie tunayolingia hapa Dsm ambayo tunaagiza kutoka Malaysia badala ya kuhimiza viwanda kujengwa kigoma. Kigoma nyanda za juu wanalima Kahawa, migomba na ni wafugaji wakubwa wa mifugo kama ng'ombe n.k. Kigoma wanalima mpunga kiasi kwamba nchi jirani zinaitegemea chakula kutoka kigoma. Kigoma ina mbuga za wanyama adimu kama sokwe, jambo la ajabu mbuga zinazoongelewa ni nyinigne sio 'gombe wala Mahale. Kuna samaki wa kipekee migebuka na dagaa na pia kuna samaki wa mapambo ambaye duniani anapatikana kigoma na Brazil (watalaam mtanisaidia hapa). kuna utafiti unaoendelea kufanyika na inasemekana bonde la ziwa tanganyika kuna reserve kubwa ya mafuta.
Kijiografia, kigoma imependelewa, ni njia ya kufika Burundi, Congo DRC, Zambia, Rwanda pia ni rahisi kufika. Sasa opportunities zote hizo hazikutumika na hazitumiwi na tawala zote zilizopita na ile iliyopo. Sasa kwa nini kigoma isiwe nyuma? is like a sleeping giant, but, as we go on, Kigoma deserves a lot interms of socio-economical development.