................JK anaharibu kuanza kushambulia watu ambao walisimama kidete kuamsha umma wa watanzania na wabunge juu ya Richmond...angekaa kimya ingetosha pia kuwa kampeni ya CCM, kuanza kutangaza huku wengi tunaingiwa na mashaka juu ya maamuzi yake..................
MI NILISTUKA NILIPOWASHA TV NIKAKUTA WAZEE WA SISIEM NDIO WAMEJAA DIAMOND NIKAWEKA STAR TV NAKO KUKAWA KAMA TVT.HIV HAWA WANATUTAFUTA NINI JAMANI.tATAKIRUDIA SAA TANO USIKU STAR TV TUONE WALISEMA NINI WALIOTANGULIA.Tena hii ta kuongea na wazee ilikuwa iwe saa tisa ghafla wakachange nwa walijua kabisa akina zito ndio wataanza kuongea jamni umechoka kuburuzwa mengi tusaide rusha na wewe live hili bungeNow JK akiri kwamba alitaka kufanya mabadiliko ya baraza . Long LIVE JF tulisema mapema akawa ana buy muda kwamba hadi Bush aondoke .Lakini siku zote alisema ni uvumi leo amekiri LIVE.Hongera JF kwa nyeti .
Ni kwamba muungana hajui kama watu huwa tunapoteza muda kufuatilia bunge kwa masaa kibao na kuacha shughuli nyingine.sisi tunakumbuka hoja hii ilitolewa na wapinzani na kilangu alipotaka kujua zaidi akafungwa mdomo.hii inanifurahisha kuona mkuu wetu anajichanganya kwa kiasi hiki,inataka kufanana na bot mana wamejifaya walianza uchunguzi mapema so hoja ni yao.sisi hatujali iwe yao iwe ya slaa tunataka watu wawajibishwe kwa kulisababishia taifa hasarahapo umenena ndg yangu Chuma................haswaaa, hakukuwa na haja ya yeye JK kushambulia akina Dk. Slaa.....................kwani statement kama hizo hazina impact/mvuto wowote kwa wananchi na hasa baada ya wananchi kusikia/kuwekewa wazi issue nzima ya Richmond na kamati teule iliyoongozwa na Dr. Mwakyembe
JK aingia ushabiki atangaza kwamba CCM ndiyo wenye issue ya Richmond na kwamba ni CCM ndiyo wanafanya kazi .Amponda Dr.Slaa na kusema anataka sifa binafsi na si mkweli kabisa .Kawataja wana CCM kwenye kamati na kuonyesha kwamba ni Shelukindo kaanza issue .
Kuna siri kubwa kati ya hawa wakuu yaani RA, EL na JK .Kaeni macho watanzania .
mkuu bado sijakufahamu hivi umetoka dar sasa ushafika dom? au una nanasa kwenye radio?
mkuu hebu tuwekee wazi tukuelewe mkuu wetu
Now JK akiri kwamba alitaka kufanya mabadiliko ya baraza . Long LIVE JF tulisema mapema akawa ana buy muda kwamba hadi Bush aondoke .Lakini siku zote alisema ni uvumi leo amekiri LIVE.Hongera JF kwa nyeti .
JK asema Lowasa ni safi sana .Ni mzalendo na mtu ambaye anaipenda Tanzania na kaisukuma mbele sana Ilani ya CCM. JK anasema kwamba Lowasa kaondoka lakini kaacha alama kubwa .
Ki-Protocol Rais anastahili kupewa vyombo kuliko Bunge. Hii kwa katiba ya sasa. may be tukibadilisha . Isije kuwa ile issue ya Adam Malima Vs Mengi ktk vyombo vyake vya Habari...nafikiri hii kesi yafahamika.
JK anaharibu kuanza kushambulia watu ambao walisimama kidete kuamsha umma wa watanzania na wabunge juu ya Richmond...angekaa kimya ingetosha pia kuwa kampeni ya CCM, kuanza kutangaza huku wengi tunaingiwa na mashaka juu ya maamuzi yake.
Kwanza Baraza lenyewe BOMU...may be kikao cha bungeni kiwe kidedea kuutokomeza ufisadi...
Kwa mshangao mkubwa na mtisiko TVT sasa wameacha kutupa habari za Dodoma ambazo zina mambo ya kugusa Taifa .Mjadala wa Richmond sina hakika kama Watanzania wanaweza kuusikia labda iwe recorded.Sasa JK anaongea na wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam .CCM again kwa mara nyingine inakuwa ya kwanza na issue za Taifa zinakuwa za mwisho .
I am confused lakini niko LIVE hapa Dar
Zitto anasisitiza kuwa mikataba sio siri kwani wao kama wajumbe wa kamati ya madini wamepewa mikataba bila hata ya kiapo kwa nini wabunge wasipewe mikataba hiyo?
Anasisitiza kuwa kuna haja ya mikataba kudaiwa na wabunge na kama serikali ikikataa wabunge wa kila kamati waanzishe kamati kama ya mwakyembe ili kudai mikataba husika .
Mbunge wa CCM anasisitiza kuwa Daniel Yona na Rostam Azizi waletwe na waseme kwa nini wamekaidi amri ya bunge ya kwenda kuhojiwa na kamati ya bunge na kwanini wanalidharau bunge .
Anasisitiza pia kuwa lazima viongozi wote waliohusika kwenye richmond basi wawekwe rumande ili kuruhusu uchunguzi wa haki na wafunguliwe mashtaka mara moja.
JK asema Lowasa ni safi sana .Ni mzalendo na mtu ambaye anaipenda Tanzania na kaisukuma mbele sana Ilani ya CCM. JK anasema kwamba Lowasa kaondoka lakini kaacha alama kubwa .
Kwa mara nyingine tena JK anazima mjadala wa bunge kumhusu Lowassa. Mapema leo mbunge wa Sikonge alikuja juu na kudai chama kiwashughulikie. Sasa wabunge hawa wakijua baadaye kuwa JK amemtetea Lowassa kesho mjadala utaanza kubadilika na watetezi wake wataanza kujitokeza. Wabunge wa CCM ambao wataendelea kulilia 'kichwa cha Lowassa' kwenye sahani wataonekana wanaenda kinyume na Rais.
Nimekuwa na wasiwasi mkubwa sana na mkuu wa kaya yetu, inaelekea anamuogopa sana sana EL na RA kwani anadiriki kujitetea kuwa haukuwa uamuzi wake ila ni uamuzi wa kamati ya wabunge wa CCM kuwaajibisha wote waliotajwa kuhusika na sakata la Richmond. Pili anasema kama mambo fulani yangefanyika tusingefika hapa, yaani kujiuzuru PM, mbaya zaidi anasema ni mchapa kazi ameisukuma mbele ilani ya CCM. Ina maana haoni hali za waTZ zinavyozidi kuwa duni? Hakuona jinsi mafisadi walivyolitia hasara taifa hili? Hajaongea na Salva akamwelezea jinsi alivyofanya kazi na Richmond? Alivyoongea Viongozi wa CCM wanamwangusha siku ile ya miaka 31 ya CCM kule Pemba alimaanisha nini? Mbona Muungwana simuelewi? Je ni kweli ana nia ya dhati kabisa ya kutufikisha tunakopataka. Nafikiri tunahitaji Mtu wa kuthubutu, mwanamapinduzi, Jasiri kama Nyerere, Sokoine na Mwakyembe. Nilizima redio kabisa. sikufurahia. Ufisadi unapakwa mafuta!!!!! Haiwezekani. Rais umekosea,Usiwaogope hawa wana mtandao, tupo nyuma yako waTZ wote. Tupo tayari kupambana na hao wana Mtandao, najua EL ananguvu na ushawishi mkubwa ndani ya chama, lakini kwa hili hatukubali na tunakuomba uchukue msimamo thabiti ussitetereke na kuanza kutoa speech nyepesi.
Mtu wa Pwani.
Umesahau huyu huwa anaruka kwa ungo?