Nimekuwa na wasiwasi mkubwa sana na mkuu wa kaya yetu, inaelekea anamuogopa sana sana EL na RA kwani anadiriki kujitetea kuwa haukuwa uamuzi wake ila ni uamuzi wa kamati ya wabunge wa CCM kuwaajibisha wote waliotajwa kuhusika na sakata la Richmond. Pili anasema kama mambo fulani yangefanyika tusingefika hapa, yaani kujiuzuru PM, mbaya zaidi anasema ni mchapa kazi ameisukuma mbele ilani ya CCM. Ina maana haoni hali za waTZ zinavyozidi kuwa duni? Hakuona jinsi mafisadi walivyolitia hasara taifa hili? Hajaongea na Salva akamwelezea jinsi alivyofanya kazi na Richmond? Alivyoongea Viongozi wa CCM wanamwangusha siku ile ya miaka 31 ya CCM kule Pemba alimaanisha nini? Mbona Muungwana simuelewi? Je ni kweli ana nia ya dhati kabisa ya kutufikisha tunakopataka. Nafikiri tunahitaji Mtu wa kuthubutu, mwanamapinduzi, Jasiri kama Nyerere, Sokoine na Mwakyembe. Nilizima redio kabisa. sikufurahia. Ufisadi unapakwa mafuta!!!!! Haiwezekani. Rais umekosea,Usiwaogope hawa wana mtandao, tupo nyuma yako waTZ wote. Tupo tayari kupambana na hao wana Mtandao, najua EL ananguvu na ushawishi mkubwa ndani ya chama, lakini kwa hili hatukubali na tunakuomba uchukue msimamo thabiti ussitetereke na kuanza kutoa speech nyepesi.