Kaka oa kama mnaendana, usiangalie, mwilini , utadanganyika, angalia uzuri wa ndani , je anamcha MUNGU,? Ana hofu ya MUNGU? Moyoni mwake kimejaa vitu gani? Je ni msafi?
Unajua umasikini ni kujitakia. Lakini duniani MUNGU ametuumba sawa kwamba tuna akili na utashi.
Sasa kila mtu amepewa nafasi ya kuchagua aina ya maisha anayoyataka , kwahiyo unachochagua ndicho unachopewa( unachokiona ndicho unachopewa- Mwanzo 13:14-15).
Hali ya mwonekano wa mtu kwa nje usikudanganye hata kidogo kaka.
Mwanamke anayefaa kuwa mke utamuona tu, kuongea kwake, kuvaa kwake, kutembea kwake, kwa uchaji wake kwa MUNGU na jinsi anavyoishi ni kiuharisia siyo kwa kuigiza.
MUNGU akupe hekima tu ya namna ya kuishi naye umuongoze mjenge maendeleo yenu na familia bora yenye kumcha MUNGU.
Jitambue kuwa nyie ni matajiri kupitia NGUVU zenu wenyewe kila kitu kinatafutwa. Maisha ya kuanza pamoja ni mazuri sana. Hasa wote mkijitambua na kujua lengo lenu ni nini.
Maisha ni kupanga , na kupanga ni kuchagua, muwe akina nani.
Nakutakia kila la heri.
Sent from my KIW-L24 using
JamiiForums mobile app