Niko Njia Panda... Msaada Please

Niko Njia Panda... Msaada Please

mapenzi hayahitaji ushauri...fuata moyo wako..hapa watu wanajaribu kukudadavulia tu principles according to their experiences ila ujue kuwa sio suluhisho la kudumu, mwenye uchaguzi na suluhisho la swala hili ni WEWE TU!! sali sana na kaa chini uungalie kwa undani hawa jamaa yupi anayekufaa..Kumbuka..ni WEWE TU!!
 
Haya haya haya........... Kongosho where are you @? Kura ya tatu na ya mwisho ya Veto ishamuangukuia Pita. We utakuwa matron kwa harusi ya Da Asia. Mi ntaukwaa ubestman wakati babu mwenzangu DC atakuwa mshenga. Ikumbukwe kuwa sauti ya DC ni sauti ya mungu mdogo.

Leo saa 11 jioni tukutane Fyatanga kwa ajili ya kikao cha maandalizi. Ukizingatia kuwa Da Asia ni bikira, harusi lazima ifanyikie Ikulu ndogo.

Mzee mwenzangu Asprin,

Hawa wajukuu sijui tuwaelezeje...Nimeona mahali eti RR anajaribu kutafuta tafsiri ya ndoa.....Hili jambo liko wazi.

Mwenza wa kufa na kuzikana siyo lazima awe na mapenzi ya egoli egoli au bongo movies...Haya huwa hayadumu hata kidogo.

Kama kuna mtu anabisha, basi anambie anaweza kula pilau mara ngapi kwa mwezi? Ila ugali na maharage au kauzu tunakula mwaka mzima...na hatuchoki. Binti awe makini kama hataki kuishia kwenye vikao vya usuluhishi kila siku..!!

Halafu The Boss kampa ushauri mzuri sana...Peter anaweza kuendelea kumpa raha na matumaini ya kuishi duniani. Ila siyo mume hata kidogo!!.....Vinginevyo, apige wote chini na kuazan safari upya!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Mzee mwenzangu Asprin,

Hawa wajukuu sijui tuwaelezeje...Nimeona mahali eti RR anajaribu kutafuta tafsiri ya ndoa.....Hili jambo liko wazi.

Mwenza wa kufa na kuzikana siyo lazima awe na mapenzi ya egoli egoli au bongo movies...Haya huwa hayadumu hata kidogo.

Kama kuna mtu anabisha, basi anambie anaweza kula pilau mara ngapi kwa mwezi? Ila ugali na maharage au kauzu tunakula mwaka mzima...na hatuchoki. Binti awe makini kama hataki kuishia kwenye vikao vya usuluhishi kila siku..!!

Halafu The Boss kampa ushauri mzuri sana...Peter anaweza kuendelea kumpa raha na matumaini ya kuishi duniani. Ila siyo mume hata kidogo!!.....Vinginevyo, apige wote chini na kuazan safari upya!

Babu DC!!
Mkongwe Dark City mzee mwenzangu umenena vema...

Hilo la kupiga chini aanze moja kwa hali halisi itakuwa ngumu. Kwanza ukizingatia umri unakimbia na ni vigumu mwanamke kutongoza. Maadam ameshatokewa na wawili na inavyoonyesha tatizo lake ni uchaguzi wa kati yao.

Ndo maana sisi wenye busara zetu, tunamwambia..... Go For Johnnie!!
 
Last edited by a moderator:
Ile sauti uisikiayo moyoni ndo njia ya kweli

Punguzeni kujidanganya,

Hata wanoolewa na vibaka au serial killers huwa wanadai waliwapenda sana...

Unapofikia point ya kuchagua mume au mke, hutakiwi kusikiliza kiungo kimoja..Kinyume cha hapo ni kujitafutia kiama!!

Babu DC!!!
 
Well,Da asia ushauri wangu kwako ni 'FOLLOW UR HEART' coz huwezi amua kuishi na mtu just bcoz anakupenda 2 bt wewe huna 'appetite nae' huna stim,not compatible,not same hobby,interests,zenyewe haziendani m-baba....hutakuwa unaitendea nafsi yako haki...huwezi nunua 'amani,furaha ya moyo wako na maisha' kwa pesa...co money at times iz not everything...we mwenyewe unazo za kwako...kaa chini na peter mwelimishe mpange maisha...that's all...
 
Nyumba kubwa kukufafanulia tu ni kuwa wote wana watoto. John anaishi na watoto wake. Peter nae ana watoto lakini wanaishi na mama yao. kwa sasa yeye anaishi mwenyewe ila anasomesha watoto wake wakiwa kwa mama yao, pamoja na matumizi anatoa.

Kwani umekwenda umri sana maana ndoa sio mchezo wa kuigiza...unaweza kuwa mzigo usiobebeka wakati mwingine.
 
Yaani mpaka sasa John anaongoza kwa kura nyingi.

Afu tayari ana kura turufu ya kwako na ya kwangu. Imebaki moja tu ya Babu mwenzangu Dark City.

Vote For John... (Nimekumbuka mshiko wangu Superman kanirusha, au adhawaiz fellow tablet klorokwini atakuwa katuuzia kibudu kwenye kiroba.... Do something Kongosho asali ya ODM)

Mkuu Asprin; nimeshatia timu DSM. Ni-PM Mkuu kupata mshiko wako. Au toa maelekezo nini cha kufanya.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nisubiri na mie kura ya Babu DC.

Hivi watu wanadhani chakula kitawekwa mezani na penzi?

Peter mwenyewe misheni town, hapo hapo atataka na ndugu zake wasaidiwe, afu hajatulia ndo maana labda waliachana mwanzo.

Heri nusu shari kuliko shari kamili, Votye for John.

Kuhusu Superman, namwendea Sumbawanga mwezi ujao, atakuja hapa hana sehemu inayomtambulisha yeye kama superMAN au superWoMAN.

Mkuu Kongosho, huna haja ya kwenda Sumbawanga, nimeshatia timu Bongo. Tuwasiliane na Winners wote!
 
Last edited by a moderator:
Love is not finding someone to live with; it’s finding someone you can't live without...Da Asia hebu tulizana, kama huyo m-baba ameweza kumpenda mkewe na kumuoa na kuzaa naye watoto kabla yako atashindwa vipi kufanya na kwako pia kipindi hicho ikiwa umechoka na yeye akiwa ameona vibinti vibichi vingine??? mpende akupendaye, jaribu kumsaidia huyo Peter awe vile utakavyo wewe...muwezeshe na kumuelimisha ili ajiajiri, awe na maisha mazuri muishi pamoja. Kwa nijuavyo mimi...mwanamke au mwanaume mwenye mpenzi zaidi ya mmoja ni MALAYA... vunja mtandao..tulizana.

Maneno yako yametulia sana...Mie binafsi siwezi kuwa na mtu ambaye yeye ananipenda sana lakini moyoni mwangu hayuko hata chembe. Sina hata raha tunapokuwa pamoja au kumkosa pale ambapo hatuko pamoja. Naona kama nitakuwa napoteza muda wangu. Mapenzi ukiyapata pale ambapo wewe unapenda na kujua unapendwa yanaleta furaha kubwa sana. Umesema Peter ana elimu sasa mshawishi atafute kazi ya kuajiriwa na huku aendelee na mishe mishe...hata kama mishe mishe zikikwama bado atakuwa na kazi yake ambayo inawaingizia kipato cha kuweza kumudu gharama za maisha...Kwa hiyo ushauri wangu mpe nafasi nyingine Peter. Kila la heri


 
Last edited by a moderator:
Maneno yako yametulia sana...Mie binafsi siwezi kuwa na mtu ambaye yeye ananipenda sana lakini moyoni mwangu hayuko hata chembe. Sina hata raha tunapokuwa pamoja au kumkosa pale ambapo hatuko pamoja. Naona kama nitakuwa napoteza muda wangu. Mapenzi ukiyapata pale ambapo wewe unapenda na kujua unapendwa yanaleta furaha kubwa sana. Umesema Peter ana elimu sasa mshawishi atafute kazi ya kuajiriwa na huku aendelee na mishe mishe...hata kama mishe mishe zikikwama bado atakuwa na kazi yake ambayo inawaingizia kipato cha kuweza kumudu gharama za maisha...Kwa hiyo ushauri wangu mpe nafasi nyingine Peter. Kila la heri




Mi najua akitulia na kumsahau peter ataweza kumpenda john na ikiwa john hatampa makhashikashi ila akimpa upendo atampenda sana hata yeyd atashangaa ni yeye ajaamua tu kumpa moyo
 
Last edited by a moderator:
Ningekuwa mimi ningekwenda kwa Peter whwre my love lies. Pesa hutafutwa. Kwa John huwezi jua ipo siku pesa yaweza yeyuka. Kwangu mimi siwezi kabisa hata kukubali kushikwa mkono na lijitu nisilolipenda, sasa sijui kwenda nae kitandani inakuwaje? Halafu for the rest of your life. Gor for Peter please.

Naam pesa hutafutwa...na mkiweka nia na kujituma basi hazitawapiga chenga....kwenda kujilazimisha kuolewa na mtu ambaye huna hata chembe ya mapenzi naye ni adhabu ya aina yake baada ya muda ndani ya ndoa utamtafuta Peter na kumwambia huna raha ndani ya ndoa umefanya makosa makubwa sana kuolewa na John, Peter naye si ajabu ana mke mwingine....mnabaki kukutana nje ya ndoa zenu na kuwasaliti wenzenu.



 
Last edited by a moderator:
bado una mtihani wa kimaisha mahana hapa upo njia panda ila ushauri wangu kama utojali ni vema ukamkubali unaye mpenda kuliko kujiingiza kwenye maisha ambayo ktk maisha yako hutaishi kwa amani itakuwa ni ndoa ndoano hambayo yawezekana ikawa na kila kitu ila ukajiona huna dhamaini ktk maisha yako kwa kawaida usiangalie uwezo angalia upendo wa thati upo upande upi japo ni ngumu kufanya mahamuzi ya haraka kuliko ujiingize kwenye jambo ambalo hutalifurahia ktk maisha yako yote ya ndoa
 
Naamini kuwa unawafahamu vema sana watu hao........Jaribu kufuata moyo wako pamoja na ushauri uloupata kutoka kwa wajumbe wengine
 
Hali zenu wana JF...
Naomba ushauri wenu tafadhali maana niko njia panda.

kuna huyu m-baba, sitamuita kaka maana ni mtu mzima. tulifahamiana miaka kama 7 iliyopita. Alinipenda sana, mpaka sasa naamini ananipenda kupita maelezo. Mimi binafsi hajawahi kuniingia moyoni. anajua simdondokei, lakini anaamini kuna siku nitabadili mawazo. Wakati huo naanza kufahamiana nae alikua na mke. ana bidii kwa kweli ya kuniweka sawa, lakini mimi wapi. kuna wakati anachoka na kukata mawasiliano, lakini vile mimi sina time nae, wala hainikeri. Mwaka unakatika anarudi tena, lakini mambo ni yale yale kwa upande wangu. Ana matatizo yake huyo kaka, sitapenda kuyaeleza ila kwa kifupi we are not compatible, nionavyo mimi we cant be togather.
Miezi kama mitatu iliyopita, karudi tena kwa nguvu mpya, na this time ni divorcee. nimeamua kua mpole fulani, japo still roho inakataa. ana kazi nzuri, ana watoto wake anaishi nao, anataka ndoa, anadai nafsi yake imeelekezwa kwangu, pamoja na kuwa namuudhi siku zote, lakini bado he thinks we can have a good life togather. Huyu nitamuita John.

Kuna mwingine, huyu namuita Peter. Peter yeye, tuliwahi kua na mahusiano miaka kama mitano iliyopita ambayo yalidumu kama miaka miwili na kiasi fulani. Tulipendana sana mpaka tulipewa majina mji huu. tukatofautiana kidogo sana na kitu cha kijinga mno, sababu ya kila mmoja kua na hasira na mwenzie, tuka break-up. niliumia na yeye naamini aliumia sana. Peter hana ajira inayoeleweka zaidi ya mission town niseme japo ana elimu. ni wale watu ambao they think hawawezi kuajiriwa.
From nowhere Peter nae anataka kurudisha majeshi, kwa nguvu zote. kibaya ni kwamba kaja wakati mmoja na John.
Peter nafsi yangu inampenda sana, na yeye naamini ananipenda, tuna match kwenye kila kitu, very compatible, interests na hobby zetu ni moja. maongezi yanalandana, namzidi kidogo umri, lakini kwangu sio issue.

Niko njia panda. John ananipenda sana na anataka ndoa, maisha yake mazuri, nikiolewa nae najua sitabahitisha kuishi, nina uhakika wa maisha bora, pesa yangu najua nitaotoa kwa kusaidia tu, lakini si lazima. Tatizo bado hayuko moyoni mwangu.

Peter, tunapendana sana, naamini hivyo, lakini hana ajira, maisha ni mishe mishe mjini mradi kunakwenda. aliwahi kuoa nae akaachana na mkewe. kwa sasa nae ni single. nikiwa nae ina maana maisha ni ku share au mimi niwajibike zaidi pale mission zinapokataa.

Mimi mwenyewe nina maisha yangu, I cant complain, najiweza, hata nisipopata msaada wa mtu maisha yangu yanakwenda vizuri bila kukuna kichwa.

Wana JF, ushauri na nasaha zenu ni muhimu. Kina dada, kama ni wewe utaenda kwa Peter au John...

What is Love to you?

Nashauri pamoja na hisia zako za kimapenzi waweke wote katika mizania ya vigezo vyote ulivyonavyo vya mume unayemtaka.

Ila kumbuka kuwa Mapenzi ni zaidi ya feelings. katika ndoa inafika mahali feelings na hata mapenzi ama yanapungua au yanakwisha. ask yourself utabaki na nini katika ndoa hali hiyo itakapotokea? Pia kumbuka wakati mwingine unaweza kujifunza kumpenda mtu kwa kumfanyia mambo mazuri hadi unampenda kweli.
 
Back
Top Bottom