Niko njia panda nahitaji msaada wa haraka sana

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Nina mpenzi wangu ambaye nimekuwa na mahusiano naye kwa muda wa miaka miwili na miezi kadhaa, tulipendana sana nakuheshimiana na kusaidiana katika hali na mali,
Kwa muda wa mwezi sasa alikuwa na tabia ambazo zilikuwa hazieleweki,kwa kuwa yeye anafanya kazi Arusha nilifunga safari mpaka kwenda kule kumsalimia nilikuta kila kitu kimebadilika,alikuwa hanijali tukienda out hanijali hata tukiwa barabarani tunatembea alikuwa anathubutu kuniacha nyuma yeye anakuwa mbele yangu, kuna siku tulienda Club aliniacha peke yangu akaenda kucheza na wasichana wengine akanidanganya kua niwafanyakazi wenzake, lakini nikamwuliza mbona hujanitambulisha? Akawa ananizungusha hakunipa jibu la kueleweka sikumwambia chochote.
Nilirudi zangu Dar esSalaam maisha yakaendelea kusonga mbele niliendelea kumpigia simu kumtumia message na kumtumia zawadi kila mara nilipopata muda wa kufanya hivyo.
Tumeendelea kuwasiliana kila mara na nimeendelea kumwonyesha upendo wangu wa dhati maana sikujua nakufahamu nini kinaendelea. Leo nimempigia simu kumwambia sina pesa nahitaji kama laki tatu, haraka haraka kanitumia, amenipigia simu nyingi sana na ameniandikia sms akinitaka niende arusha kumtembelea amenisihi sana lakini nikamwambia "nilikuja hukunichangamkia wala hukionesha kunijali kweli sijisikii kuja"amenisihi sana lakini nikamwambia kwa sasa sina muda kuna mambo yamebana sana labda Holiday za Xmass na mwaka mpya. Akawa amenielewa tukaongea na mambo mengine.
Baada ya muda akanitumia message ananiambia kuna kitu anataka aniambie ila nisikasirike nikamwambia hamna noma.
Amenitumia ujumbe huu......
Baby sorry najua nitakuumiza please haikuwa dhamira yangukufanya hivyo but nimejikuta tu imetokea nikawa na mahusiano ya kimapenzi namsichana hapa Arusha anaitwa Rachel nilimu approach akanikubalia ingawa sikutaka kuachana na wewe directly but ikatokea nikawa sikupendi kabisa nani kawa najisikia kero hata kupokea simu yako, ingawa nilifikiria kuachana nawewe lakini nikaona sio vizuri sikufanya nae mapenzi zaidi ya romance, na nilichana picha zako zawadi zako zote ulizonitumia nilichoma moto. Lakini juzi nimeachana na. nae nahitaji kuendelea na wewe naomba unisamehe na usichukue hatua mbaya kumbuka tumetoka mbali.
Jamani naomba mnishauri nifanyaje yaani hapa nilipo simu zangu zote nimeziweka kwenye flight mode nanyingine Offline sitaki pokea simu zake, please nahitaji ushauri wenu
 
Huyo mwanaume ni **** sana, ni juu yako kuona kama amejirekebisha kiukweli. Unaweza kumpima kwa kidogo kama kajirekebisha kisha mkapime ile kama utaridhia jamaa aendelee kupiga mambo yetu yale.
 
lola
Endelea nae tu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,kama kashaachana na huyo Rachel, what is the problem then? Granted he was and has been up to no good but rarely you will find men with such honesty! My advise is jimwage nae ila usiache kumpa joto ya jiwe so he can learn that you are not his to use and dump when he pleases to!!!
 
duh!!!! i dnt know wat to say really
on one side this guys has realized that he has done wrong nd has come clean abt it hence shows to be an honest man
on the other he has shown he cn no nolonger be trusted.
sasa mie ushauri wangu ni kwamba mwambie kaka asante sana kwa ukweli wako but this is the end of the realitionship becoz the trust has be broken and hence will also be uneasy with u being all the way there in arusha.

mwisho kabisa dada yangu...long distance realtionship never work...so never try it again!!!
 


anapima uvumilivu wako. kwani angekuwa mjeuri asingepoteza muda kukupa hiyo stori, ukizingatia mlikuwa hamjaachana. na hujawai mjua huyo mtu anaemsema

kwa uzoefu, ni kuwa anamtu mwingine ambae amewekwa kwenye mzani na wewe. na huyo mtu sio huyo aliyemtaja. anawaona wote mnafaa kwa kila namna. hapa anaangalia reaction yako. kama uki react vibaya ujue ndo mwisho. ukimwonyesha uelewa basi it ticks the boxes
 

Thanks my dear
 
sasa kidume kimefunguka na kukueleza ukweli
na kimeomba msamaha....na wewe unauliza ufanyaje?

ukimsamehe si ndo poa?

mnatufanya tushindwe 'kukiri' na kuomba msamaha
kwa sababu mnatumia 'kukiri na kuomba msamaha' kama silaha ya kutuadhibu...

wanaume wengi wakisoma hii post watasema huyo jamaa yako
'alikosea mno' kukueleza ukweli
angejirudisha kimya kimya bila wewe kujua kilichotokea....
 

asnte kaka yangu nitaufanyia kazi ushauri wako
 
Huyo ni ****** hana msimamo ktk mapenzi anatapa tapa ka Zombi. Temana nae ila km unampenda angalia moyo wako ila huyo ni ****.
 

asnte Boss wangu kwa kunifungua, i appreciate you...
 
Kweli kabisa, huyo kaka ni wa kusamehewa manake ameamua kuwa mkweli mwenyewe, mwingine angeamua kunyamaza na maisha yangesonga mbele bila mdada kujua kilichokuwepo nyuma ya pazia. Lola hajawahi kukutana na mwanaume unamfumania live na bado anakataa, hakiri hata kwa mtutu wa bunduki, mie ntamshangaa sana kama atashindwa kumsamehe mwenzi wake!
 

halafu yeye mwenyewe anasema 'anampenda' bf wake
sasa ushauri wa nini tena?
 
Ukweli hujenga uaminifu...... Anayejutia kosa hafikirii kutenda kosa tena.....Mpe nafasi tena ila sio kirahisi rahisi, m'shake kidogo aone umuhimu wako
 

asante kwa kuendelea kuujenga moyo wangu uliokuwa umeanza kupasuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…