Niko tayari kufundisha Kung Fu, Judo, Karate, Taekwondo & Kick boxing muda ukiruhusu

Mmmhh ningekuwa CUF ningelikutafuta! Kuna memba mmoja huyo anaitwa M Sugu anapenda karate

Out of point!!! (nnje ya mada!!!).
Inaonekana ungepewa kazi ya kugawa riziki, wale wapinzani wako wote usingewapa kwa kuwa wanapingana nawe. Tushukuru Mola kazi ya kugawa riziki anaifanya yeye mwenyewe, lau kama angemkabidhi binaadamu kazi hiyo ingekuwa kazi kweli kweliiiiii!!!
 

dah! mbona umelalia sana kwenye kuwezesha watu kupiga wengine?
ni vyema ungesisitiza kwenye kubadili mtu kuwa mwema zaidi katika jamii,
mvumilivu na uwezo wa kujilinda (ambayo ni tofauti na uwezo wa kumgaragaza
mpinzani ndani ya dakika 4)
 

Twamshukuru Allah.
Muda ndi unakaribia so ni maeneo gani?
Hivi Karate hujaeleza ni styles zipi utafundisha...!
Nataka nije niongeze kidogo rank.
Ila nmepata mkanda wa ***** katika Shotokan. Pia Judo.
 


Vipi mkuu huu mpango bado upo? mi nilishaanza mazoezi ya kukimbia ili niwe na Pumzi. I realy love it.
 
Nikikumbuka Ustaadhi Moody wa Msikiti wa jirani alivyokuwa akitufundisha Judo wala sitaki!
 
Aisee hii bonge la idea. I am so interested. Tafadhali naomba utuambie mapema ni lini utaanza haya mafunzo ili tuweze kujipanga na foleni za barabarani na kupanga muda wa kutoka huko tunapotoka hadi kufika panapostahili...!

Napenda sana hii kun fu sema naogopa sana mafunzo yake manake najua kuna kupiga msamba na mazoezi yake ni ya kuumiza sana. Je unauzoefu wa ku train watu ambao ni fresh? ambao hawajawahi hata kurusha teke moja?
 

Japo hajatuambia wapi kutakua school(Dojo)...
Usihofu...bila shaka hata jina lako limetulia...utaweza tu.
 
Dah! Mkuu, unaonekana wewe mkali kushinda hata wale magwiji wa Kung fu na Karate, kina Bruce Lee, Jet Li, Jack Chan, na hata yule mkali wa Thai box Tony Ja umemshinda... Maana hawa magwiji wa Martial art, wao wame-speacilised kwenye aina moja tu ya sanaa ya mapigano, lakini wewe, umekusanya karibu sanaa 5 kama si sita, zikiwemo, kung fu, karate, Judo, kick boxing, taekwondo na hata ile hali ya kutafakari (meditation) wewe unajuwa namnai yake...!

Lakini mkuu hii michezo si tuna-practice for self-perfection and for self-defense and as a sport tu, au kazi yake kuingia mitaani na kudunda watu hata wakikanyaga vivuli vyetu?

Sawa mzee wa Kumite sasa una yudansha ya aina gani mkuu...!?


Lakini juwa kwamba walimu (Masters) wa hii michezo wanafundisha nidhamu ya hali ya juu sana... sensei Funakoshi yeye anasema hivi: "inwardly humble and outwardly gentle." and "indecisiveness is a weakness"
 
Ukifika tujulishe, kuna vitambi uzembe vya akina The Finest na wenzake lazima zitokomee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…