Mabula marko
Member
- Jul 18, 2022
- 44
- 38
Habari za wakati huu ndugu
Kulikuwa na kijana mdogo aliyeitwa kaswahili, mzaliwa wa kijiji kidogo kutokea katika nchi ya Tanzania, kijana huyu alitamani sana kuiona Tanzania ikiwa nchi bora Zaidi kwa kila mtu kwani kaswahili alichoshwa sana na malalmiko ya wazazi wake pamoja na wazee wa pale kijijini kwao juu ya vitendo viovu kama ufisadi,rushwa na mengine mengi yaliyokuwa yakiendelea nchini mwake. Kaswahili aliamini kuwa kama kila mtu angefanya kazi kwa bidii na kwa uwajibikaji, Tanzania ingeweza kuwa nchi bora zaidi.
Kaswahili alianza kufikiria jinsi gani ya kuleta mabadiliko katika nchi yake, hatimaye siku moja akiwa amekaa chini ya bustani yao baada ya kumaliza kumwagilizia nyanya ambazo wazazi wake walilima alimwona mototo mdogo na ndege wa kuchezea aliye kuwa ameundwa kwa rangi tatu ambazo ni kijani, njanona bluu, kaswahili alipata wazo zuri la kutumia ndege huyo kama ishara ya uwajibikaji.
Kaswahili aliamua kuanza kufanya kazi kwa bidii sana huku akiwahamasisha na watoto wenzake katika shule aliyokuwa akisoma na katika kijiji chake kwa ujumla kufanya kazi, kaswahili alitumia huyo ndege mwenye rangi tatu kama ishara na huku kila rangi akiipa maana yake rangi ya kijani ilikuwa ishara ya uwajibikaji, rangi ya njano ilikuwa ni ishara ya kujituma na bluu ilikuwa ni ishara ya utawala bora kwa hakika ndege huyo aliwapendeza sana watoto wenzia na hata ikawa rahisi kwakwe kuwafikia na kwani wengi walipenda sana kuchezea ndege huyu wa kuchezea basi alivyoona ndege wanapendwa sana aliamua kutengeneza wengi Zaidi na Zaidi.
Kaswahili aliamua kusambanza ndege hizi kwa watoto katika maeneo ya kijiji chao na vijiji vya jirani hatimae vilitapakaa sehemu ya mbali na hata kila mahali pa nchi nzima , kaswahili alianza kuwafundisha watoto kutumia ndege hizi kama ishara ya utawala bora , kujituma na uwajibikaji kupitia rangi tatu za ndege kwa kuwa watoto walipenda sana wale ndege walipendezwa pia yale ambayo kaswahili aliwafundisha.
Baada ya muda, watoto hawa walikuwa wakizungumza na wazazi wao na kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kwa uwajibikaji. watoto hawa walikuwa wakionyesha ndege hizi kwa wazazi wao na kuwafundisha maana yake. Watu wengi walivutiwa sana na wazo hili na walianza kufanya kazi kwa bidii na kwa uwajibikaji.
Kaswahili alifurahi sana kuona jinsi watu walivyokuwa wakifanya kazi kwa bidii na kwa kuwajibika. Aliamini watoto kuelewa imekuwa chachu kuleta mabadiliko makubwa katika nchi yake kwani kila mtu alifanya kazi kwa bidii na kujituma pia utawala bora na uwajibikaji
HITIMISHO
Waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, methali hii inatukumbusha yale ambayo kaswahili aliyafanya katika udogo wake ambapo aliwafundisha watoto alafu watoto wakawafundisha watu wazima kumbe inatupaswa kama taifa kufundisha utawala bora na uwajibikaji kwa watoto wadogo ambayo ndiyo taifa la kesho, kwa mfano kama serikali ambavyo imekuwa ikija na miradi mbali mbali kwa vijana basi ije na mradi unao lenga kuwahusisha watoto hasa kwa ngazi ya shule ya msingi na sekondari kuwafundisha uwajibikaji na utawala bora, tumekuwa tukishuhudia katika nchi za wenzetu wakiwekeza sana katika watoto wakiamini mtoto akilelewa akiwa mzalendo na mwenye kuwajibika basi sio rahisi kubadilika kupoteza dhana ya uzalendo katika maisha yake.

Upvote
6