Nikumbusheni kama bado tuna 'Diplomasia'

Nikumbusheni kama bado tuna 'Diplomasia'

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Wote tuliokulia miaka ya 60, 70, 80 tunajua vyema, wakati huo Tanzania ilikuwa 'jogoo' katika ulinge wa Kimataifa. Hivi kwamba, katika mahafali ya Kimataifa Tanzania ikimwunga mkono mtu, nchi hivyo hivyo mataifa duniani yatafuata na kumpitisha.

Sina haja ya kuelezea mapambano ya Tanzania dhidi ya Marekani na vibaraka wake hadi Jamhuri ya Watu wa China ikakubaliwa kupewa kiti katika Umoja wa Mataifa badala ya Jamhuri ya China, Taiwan (Formosa).

Fast Forward.....hadi leo tumafikia hali hii ambapo Rwanda (kama Mkoa wa Tanga tu) inatajwa zaidi duniani kuliko sisi! Kidogo rais Magufuli alivutia kutajwa-tajwa, lakini kwa vile si kwa maudhui bali mtu mmoja na kazi yake.....utajo huo haukuendelea. Na hata angekuwepo, sidhani kama angeendelea kushabikiwa.

Utajo wa Kimataifa unataka nchi iwe na msimamo, malengo na dira. Hivi iwe inavifuata 'consistently'. Tena iwe jasiri kugombea misimamo yake hiyo hata ikiwakasirisha wakubwa.

Pia ichukue fursa zinazotokea na kuwa 'vuvuzela' katika mambo muhimu yanayoendelea ima duniani au barani.

Nasema hivi huku nikijiuliza viongozi wetu wa diplomaia hivi hawayaoni haya matukio makubwa yanayoendelea barani Afrika, kiasi wamefumba macho tu mwanaharamu apite?

Vita vya Msumbiji na Ethiopia! Angalia watu wanaofikiria mbali na kutwaa fursa, Kagame na Uhuru. Wote wamejitosa sana katika matukio haya, kwa kutembelea, kutoa statements n.k.

Ni dhahiri kwamba nchi hizo zilizofikwa na majanga, pindi zitakapomalizana, zitamjua nani ni rafiki yao wa kweli: "akufaaye katika dhiki ndiye rafiki' Ila sisi Tanzania hatuna hili wala lile.

Hali hii ya kujifungia chumbani ni mbaya sana. Tukifikwa na lolote. Wengine pia watakaushia!
 
Sisi kazi yetu ni kupiga picha na wazungu kwa sasa.
 
Back
Top Bottom