Magufuli 05
JF-Expert Member
- May 7, 2023
- 1,990
- 3,824
Hongera Gwajima. Acha wajinga wakushambulie lakini watanzania wenye akili tumekuelewa
Gwajima ameagana na nyonga kabla ya kukimbia. Haikuwa rahisi kujitokeza hadharani kwa desturi ya nchi yetu kwa mbunge tena wa chama tawala kuzungumza jambo linalogusa maisha ya watanzania kwa kiasi kile. Na Gwajima nimjuaye kwa mbali hapo ametekenya tu Bado anakuja. Na itakuwa hatari. Gwajima anayo Siri kubwa na mambo yakienda hivi watanzania jiandaeni kujua msiyoyajua.
Hawa akina Tarimba na Msukuma wanaokuja kupinga na kumshambulia mnawakilisha wananchi Gani? Ni kweli nyie hamna uchungu na watanzania waliotekwa na wanaotekwa? Kisa tu si wanachama wa chama chenu? Wengine akina Muro mnasema utekaji ulikuwepo toka zamani. Je mnataka kuhalalisha utekaji kwa matukio ya nyuma? Kabisa hamuoni kama Kuna Shida mahala.
Pia soma Pre GE2025 - Askofu Gwajima: Wakuu wa Vyombo vya Usalama wasiondolewe kwenye nafasi zao kwa mapenzi ya mwanasiasa aliyewaweka
Nyie mnaopinga hoja za Gwajima ndiyo genge ambalo Gwajima kalisema?
Nilitegemea bunge lijadili kwa kina tena kwa dharura utekaji kama huu, nyie mnatumia Bunge kuhalalisha utekaji. Watanzania mnawaona nyani? Kijana mmoja alichoma picha huko Mbeya kilichompata masikini. Mbona magazeti yenye picha za mwenyekiti tunafungia vitumbua na hamtukamati. Huyu kuchoma tu yakamkuta.
Siandiki sana lakini Gwajima amesukuma kete sasa nyie jaribuni kugusa atawapiga hamsa ni suala la muda. Mnamtisha chama kimchukulie hatua je mnadhani hakuna maisha nje ya CCM.? Alikuwepo nje ya CCM na atakuwepo nje ya CCM.
Tunataka sauti kama hizi za kuwasemea watanzania na matapeli kujificha kwenye kichaka Cha amani kuiba Mali za umma. Tumechoka kusikia kauli za kuwashughulikia watanzania wasio na hatia.