veyra
Member
- Aug 31, 2025
- 19
- 29
Kiungo wa kimataifa kutoka Uganda, Khalid Aucho, amethibitisha rasmi kuwa ataichezea klabu ya Singida Black Stars, licha ya awali kutangaza hatacheza tena kwa timu yoyote ndani ya Tanzania.
Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aucho amesema amebadilisha msimamo wake baada ya kuona mwelekeo wa mradi wa Singida Black Stars na kueleza kuwa ni timu yenye ushindani mkubwa.
"Ni kweli niliwahi kusema sitacheza tena kwa timu yoyote Tanzania, lakini baada ya kuona project ya @singidablackstars nilibadilisha mawazo. Mimi ni mpenzi wa ushindani, na Singida ni timu yenye ushindani mkubwa," alisema Aucho.
Aidha, kiungo huyo ameweka wazi kuwa urafiki na heshima aliyonayo kwa kocha Miguel Ángel Gamondi imechangia kwa kiasi kikubwa kufanya uamuzi huo.
"Namfahamu Kocha Gamondi, ambaye naye ni kocha anayeishi kwa ushindani. Hiyo ndiyo sababu nyingine kubwa iliyonifanya nikubali kujiunga na Singida Black Stars," aliongeza.
Singida Black Stars imeendelea kuvutia nyota mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, na usajili wa Aucho unaongeza nguvu kubwa kwenye kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.