Niliandamana Tarehe 29 na nitaandamana tena ikibidi

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa Watu waliotoka tarehe 29/10/2025.Kwanza kabisa nikiri kuwa nilitoka asubuhi sana na bango langu lakini hakukua na mtu barabarani.

Baadae nikarudi pembeni, nikakuka wengi tu wamekaa pembeni, kumbe code ilikua maandamano yalipaswa kuanza saa 4.

Najivunia kuwa saa nne maandamamo yalianza na nakiri kuwa watu walitoka sana, sijawahi ona watu wengi vile.

Wananchi tulikua na sababu milioni za kuandamana, kama nchi tulikua tumefika pabaya sio kiuchumi sio kijamii sio kisiasa!! Ilifika wakati hata mtu kuhoji tu unapotea, ilifika mahali watu wanajilia nchi tu watakavyo ilifika mahali sasa watawala wakakaribia kuwatia wananchi "madole" kwa kua hakuna wa kufanya kitu.

Sasahivi watatuheshimu pakubwa mno, maana walitaka Show na tumewaonyesha show....Watawala walituona sisi ni waoga na hatujui haki zetu lakini tarehe 29 tuliwaonyesha kuwa sisi sio waoga tena na kikubwa ni kuwa tayari tumezika rasmi dhambi ya Uoga tarehe 29 sahivi hakuna mtu anaogopa chochote....Tunaheshimiana mtaani.

Sote tunafahamu mateso tunayopitia kama nchi, hatuna media hata moja, jamiiforum yetu pendwa yenyewe imepigwa ban, hapa wote tunaingia humu kwa Vpn hata wale wachache wasiofika watano ambao hadi leo still ni chawa promax wa SSH regime..

Msg kwa Samia ni kuwa sisi bado hatujamalizana na wewe!! Utawala wako umeua ndugu zetu kibao, hapa nina hasira natetemeka najikaza tu kuandika kwa staha, na asilimia kubwa ya waliouwawa wameuliwa majumbani kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha na maafisa wa serikali walokua wanapita nyumba kwa nyumba kushoot watu hovyo hovyo.

Kuna mama kavamiwa nyumbani kwake na hawa watu alikua anaangalia tv ndani wakavunja mlango na kummiminia risasi yeye na vichanga wake mapacha wa miezi 6 nyie[emoji24].

Nina shuhuda nyingi sana, naomba niishie hapa ila naapa hili halijaisha halitapita hivi hivi bila majibu sahihi.

Nina hasira mno wakuu tokea jana sijalala....
 
Hongera sana.
 
Kusema kweli maandamano yameweka ufa mkubwa kwenye utawala wa Samia. Maandamano yalitulia sababu raia walikosa pakununua chakula na petrol wala si kwa sababu ya askari wenye bunduki. Pindi watu watakapokuwa na stock ya chakula na petrol ya kutumia kwa wiki 2 nchi itabadilika.
 
Tuombe sana mungu aisaidie Tanzania yetu maana ni maombi tu hamna lingine
 
Haya maandamano yamepanda mbegu kali sana!

Siku yakiibuka mengine yatakuwa "Maandamano Aggressive" in every aspect.

yatakua maadamano ya kumalizana kabisa maana wameona mfano ukifanya mistake unakufa kwa raia watajinga haswa kweli kweli maana wanajua ni kufa hama kupona sasa hiyo itakua mbaya raia wakipata mzuka wote
 
Kusema kweli maandamano yameweka ufa mkubwa kwenye utawala wa Samia. Maandamano yalitulia sababu raia walikosa pakununua chakula na petrol wala si kwa sababu ya askari wenye bunduki. Pindi watu watakapokuwa na stock ya chakula na petrol ya kutumia kwa wiki 2 nchi itabadilika.
Sure
 
Back
Top Bottom