Nilianza kuwa na ukakasi dhidi ya AI pale mmoja wa wahasisi wa AI alivyoacha kazi google na kuonya dunia dhidi ya AI na maendeleo yake

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715

Geofrey Hinton anajulikana kama "GODFATHER OF AI" anatakumbusha swali la msingi, je tuko tayari kisawa sawa kwa ajili ya AI?

Sijui kama Aliacha kazi kama protest au hofu ya ukuu wa AI ambao unakuwa kwa kasi sana ila all in all hata mimi sioni mazuri mbeleni.

Mwamba anasema AI inaweza hivi karibuni kushindana au kuzidi akili ya binadamu katika nyanja mbalimbali. itafika wakati kuwa AI itagundua namna ya kuua mtu

Hinton ameonya kwamba kadri AI inavyokuwa na uwezo zaidi, inaweza kushinda udhibiti wa binadamu, na hivyo kusababisha hali ambapo binadamu atakuwa hana umuhimu.

Mwamba pia anasema AI itajenga akili kubwa ambayo tunaweza kushindwa kui-stopisha na pia itaweza kukuwa kwa kiasi tunaweza kutapelika na AI bila sisi kujijua.
 
Kuna mambo kama sio jicho la tatu mfano kuna movie ambazo zinaeleza kuhusu itafika sisi wanadamu tutakuwa watumwa wa marobot sababu watakuwa wamesoma mengi na mkuu wao hatakuwa Ai mwenye elimu kubwana ambaye atawezakutengeneza chochote bila sisi binadamu kumpinga.Kunamovie zipo nyingi sema zinavyoeleza kama sio muelewa unaweza kuona kiburudisho.
 
Yanini kuhofia watoto uliowazaa wewe mwenyewe kama unawalea vizuri?
 
Movie za marekani hasa za sci-fi ni za kuangalia kwa makini maana asilimia ndogo mno zinakuwa kwa ajili ya burudani na asilimia kubwa ni kwa ajili ya aidha kuna kitu wanajua hivyo wana toa ujumbe au hints kwenye movie zao au wanataka ku mislead watu
 
Mi nionavyo AI ni kama silaha,hivyo yategemea mtumiaji na muundaji anaitumiaje na ana lengo gani,kuna matumizi chanya na hasi,ikitumika kiuchanya utapata tija, kinyume chake ni hasara na majanga kwako.
 
Kwenye hiyo picha nimeshimdwa kuelewa hiyo mikono/viganja vya huyo God father ni vyake au ni picha tu???
 
Umeshawahi fanya interaction with AI?

Najiuliza experts wetu na users wanaifahamu Ai kiundani kabla ya kuitumia... Inakusanya data Gani and for what purpose...
 
Naye yule mnyama 666 akapewa uweza wa kulipulizia sanamu pumzi (AI) hadi lile sanamu likanena ...nalo likanena makufuru
 
Mkuu hili ni janga kubwa sana hapo baadae, hata waweke udhibiti kiasi gani bado kuna watu watakua na uwezo wa ku-ufeed mfumo taarifa haramu na hatari kwa usalama wa wanadamu,

Linaweza likaibuka genge la wahuni kama tunavyoona magaidi maharamia yakaunda AI yao inayohusika na uharifu au wakaunda mfumo unaoingilia mifumo halal ilioidhinishwa na kuaminiwa na mashirika ya kidunia ili kutumikia katika shughuli mbalimbali kama vile hospital jeshini usafilishaji etc kwahiyo mfumo ile algorithm yake I kachezewa na ku miss behave kama ambavyo computer viruses wanavyocurrupt computer kulingana na intent ya mdukuzi.

Pia tunaambiwa kuwa kuna dark Web ambako kuna harakati zinazoendelea huko ni hatari sana, sasa je vipi kama hizi AI zikapata access ya hizo data nini kitatokea, hasa ukizingatia huko mbeleni shughuli nyingi zitakua computerised na automated na hizi AI algorithms.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…