Niliapa sintakuja piga mwanamke

Niliapa sintakuja piga mwanamke

Nzurii!, hutamani iishe. Lakini ilipofika inaogopesha, Malcolm asitishe sana jamani.

Nimecheka pa mtoto akilia na yeye anaitwa kubembeleza, alivyoiweka kama vile ni kitu cha ajabu yeye kubembeleza mtoto...lol
Hahaha mbona kubembeleza, but ilisaidia sana kwenye kuform bond, you know how it feels kumbembeleza mtoto hadi alale
 
Jibu lako lile limenikumbusha mhenga aliyewahi kuitawala nchi ya "Bongo land" alipata kusema "Ukitaka kula lazima uliwe". Tigo nao wamemuenzi kwa ile "Jaza ujazwe". (Nimecheka at! )
[emoji23] daah una misemo migumu nimejikuta narudia tena na tena kuelewa nimetoka kapa
 
Wakuu wasalaam,
Bwana mimi huwa sipendi kubishana kabisa na mabinti na hata akinikosea huwa siwezi kumfanya chochote namuangalia na kumwacha tu. Kama ni muelewa huwa namkanya aache kitu fulani lakini nikikuta akili ndiyo zile zile huwa namwacha tu. Kikubwa zaidi haya matatizo ya kubishana na wanawake siyapati kwasababu huwa sijichanganyi nao sana: nakuwa nimejikita sana katika maisha yangu.

Sasa miaka kama 18 hivi imepita nimemaliza shule najiandaa kuingia Chuo nilikuwa nafanya kazi moja sehemu fulani hivi. Sasa nikawa nakutana na dada moja mjamzito mkubwa kwangu kama miaka 10. Nilikuwa namsalimia kila asubuhi na alikuwa ananichangamkia sana kila tulipoonana. Lakini muonekano wake ulikuwa ni wa mtu ambaye maisha yamemtupa mkono. Mara nyingi alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana: nikaja kujua kwamba alikuwa anafanya usafi kwenye nyumba fulani ya Mhindi.

Sasa siku zinazidi kusogea mimba ikawa inakuwa kubwa na mara nyingine nilimkuta akikaa nje kwenye kivuli wakati watu wanaenda kula. Mimi kusoma tu yale mazingira nikajiongeza nikawa nanua vyakula vya watu wawili nampelekea. Mara ya kwanza akawa anagoma lakini akaja kuzoea hiyo hali. Jina lake alikuw anaitwa ********

Hivyo nikawa namuita dada.
Sasa kuna siku moja nimeenda kule kazini naulizia dada fulani yuko wapi wakasema hayupo ameenda kujifungua. Kipindi hicho hata mawasiliano ya simu watu wengi yalikuwa hayapo. Sasa sikutilia maanani sana ile ishu nikasema atakuja ntampa hongera. Kesho kutwa yake naenda pale ofisini nakuta yule Mhindi na watu wengine wamejaa kwenda hivi nakuta mtoto kichanga kwenye kikapu fulani hivi.

Kuuliza wakasema wamekuta analia ametupwa hapo chini. Yule mama muhindi akasema atakuwa ******* huyu maana yule binti alikuwa amaevurugwa sana na maisha. Mimi akili ikanijia kweli yule dada kajifungua: nikasema sasa kwanini atupe mtoto. Baadae watu wa Ustawi wa jamii, Balozi na polisi walikuja lile eneo lakini ikawa inaonekana hakuna suluhu ya lile jambo. Mimi nikaenda kufanya kazi ndani lakini yule mtoto alikuwa analia sana hadi moyo ukanigusa.

Nikaenda tu nje,
Nikamwita yule polisi moja alikuwa ni mwanamke: Nikamuuliza mustakabali wa lile jambo akasema watampeleka yule mtoto kituo cha yatima watu watamlea. Kipindi hicho hata maziwa na diapers hakuna kwa wingi yaani full visepe na nepi. Nikauliza jinsia ya yule mtoto nikaambiwa ni wa kike. Yaani ndiyo huruma ikanizidi mara mbili.

Mengi yalitokea pale,
Wakaondoka na yule mtoto lakini kila nikimkumbuka yule dada na nikimuangalia yule mtoto naona sana huruma. Roho ikaniingia ikasema chukua huyo mtoto, nikaona nawaza ujinga lakini msukumo ule ulikuwa ni mkubwa sana. Huwezi amini nikaenda kwa wale polisi wakasema na watu wa ustawi wakacheka sana wakasema “yani wewe huyu mtoto umpeleke wapi? Wewe mwenyewe bado mdogo hapo halafu isitoshe wewe ni mwanaume”.
Nikawaambia mama yangu atamlea yule mtoto, tulibishana nao sana pale.

Bahati nzuri balozi aliwafahamu wazazi wangu kwasababu kabla ya kuhama ule Mkoa tulikuwa tunakaa kwenye ile nyumba ambayo huyo Mhindi alikuwa anakaa. Basi akaniita akasema mimi wazazi wako nawafahamu ni watu wema sana na baba yako amasomesha watu wengi sana ambao ni ndugu na wasio ndugu naamini hawezishindwa kumlea huyu mtoto. Lakini akashauri kwamba siyo jambo jema nijiamulie mwenyewe tu. Alizungumza na wale polisi na wakaandika kabisa kile kilichotokea pale na mimi nikasaini.

Balozi yule usiku ule aliwaomba watoto wake wakae na yule mtoto huku akiniambia unavyosafiri kurudi kwenu ntakupa binti yangu urudi naye ili akusaidie kukaa na mtoto njiani. Basi akasema atawandikia wazazi wangu barua kuhusiana na tukio lile huku akinisifia kwamba kijana wangu umefanya jambo la kiuanaume sanaaaa. Huu ndiyo ubinadamu wa kitanzania.

Safari imefika nikarudi makwetu,
Kwenye gari kila mtu alikuwa anauliza mtoto huyu mzuri ni wa nani lakini yule dada anasema wa dada yake. Watu wanataka wamshike lakini maswali yakawa mengi sana na baadhi ya watu tuliokuwa tunasafiri nao walikuwa wanafahamiana na familia yetu. Kuna mama moja ni Mchagga rafiki wa mama akauliza wewe MALCOM huyu mtoto mama yake yuko wapi ??

Nikasema amefariki,
Akasema sasa wewe unaenda naye wapi huyo mtoto ???nikajibu nyumbani kwetu. Akauliza wewe kama nani wake ?? Watu wengine wakavutiwa na ule mjadala, huku wamenitolea macho. Basi nami nikakaza macho nikasema mimi ndiyo baba wa huyu mtoto. Akastuka na kuanza kusema: MALCOM umri huu unazaa mtoto ??? Wazazi wako wanajua haya ??? Yule dada mtoto wa balozi akataka kunitetea lakini nikamnyamazisha. Akaanza kuuliza kama yule dada ndiye mama yake mimi naficha.

Mara wamama wengine na watu wakadakia ule mjadala. Wakaanza kuropoka kwamba Watoto wa siku hizi wamebadilika sana, tena mimi ndiyo kwanza nimemaliza sekondari tayari na mtoto,nikifika chuo nitaamua kuoa kabisa wake wengi. Nilishikwa na hasira sana nikamwambia yule mama "Mbona binti zako wote wamezaa nyumbani tena yule mkubwa kazaa na mwalimu wake humuoni kwa hilo ??” akastuka huku wengine wakianza kuropoka maneno kama “huyu Mhaya ana kiburi sana ona maneno anayojibu wakubwa”

Kadiri wanavyosema ndiyo walizidi kunipandisha hasira hadi mama moja akasema “usipoangalia utaugua miwaya wewe mtoto” kipindi hicho ukimwi ndiyo umepamba moto. Nikamjibu “Mbona wewe ulikuwa unatembea na mume wa mtu mzee ***** halafu hujapata hiyo miwaya ??” basi zima kukawa na ukimya utadhani shetani kapita. Yule mama alikuwa mwekundu usoni, akaloa majasho mwili wote.

Wakaacha kunishambulia,
Lakini mimi nilijua kabisa nikianza kuwaambia kwamba huyu mtoto ameokotwa inaweza ikaja kuwa stori ambayo itamuumiza huyu mtoto akikua na hatajihisi ni sehemu ya familia yetu. Maana anaweza akafanya kitu halafu wakasema siyo Mjukuu wa mzee fulani huyu halafu mtoto akaishi kwa shida sana na adharaulike bila sababu. Hilo ndilo lilikuwa wazo langu kubwa.....

Itaendeleaaaaa...............
Duh
 
Back
Top Bottom