Kinyonyoke
JF-Expert Member
- Oct 4, 2016
- 3,498
- 13,138
Mimi ni kijana mgeni hapa mtaani.Jana nikiwa nimekaa napiga story na mangi,mara ghafla akaja demu mmoja mzuri kweli kweli.Umbo namba nane,miguu ya bia, kisura cha kitoto kilichopambwa na vishimo fulani hivi mashavuni (dimples),ana nywele ndefu mpaka mgongoni,mwendo wake wa madaha ulinidatisha zaidi,nikajiapiza lazma nimfahamu,alipoondoka dukani,nilimuuliza mangi jina la yule msichana akanambia anaitwa Judith.Nilimfuata kuongea naye lakini hakunipa ushirikiano wowote,nikapga moyo konde nikaendelea kumfuata mpaka alipojitoma katika geti lao akapitiliza mpaka ndani nami bila ajizi nikaingia nikaangaza kulia na kushoto,lahaula! uso kwa uso na wazazi wake.Niliwasabahi,wakaniuliza nilihitaji nini wanisaidie,huku nikibabaika nikawaeleza namuulizia rafiki yangu wa kike anayeitwa Judith.Sijui kama walinisoma vile kwani Judith alipoenda kuitwa aliambatana na kopi yake!.Aisee! kumbe walikuw mapacha..Wazazi wakaniambia nimchukue Judith ambaye nilidai ni rafiki yangu.NILIBAKI NIMEPIGWA NA BUTWAA AMA KWELI NILIUVAA MKENGE.