chime pinchi
Member
- Aug 13, 2022
- 9
- 38
Habari za muda huu ndugu msomaji wa makala hii.
Napenda kukukaribisha kusoma simulizi hii fupi yenye uhalisia Kwa namna Moja ama nyingine. Tukiwa na umri wa miaka kumi Mimi na rafiki yangu aitwae Mido tulikuwa ni watoto wa mfano sana kijijini kwetu tulipokulia, wazazi wangu na wazazi wa Mido walikuwa ni wafanyabiashara ndogo ndogo katika Kijiji chetu cha Bungu mkoani Tanga wilaya ya korogwe vijijini, ubaya ni kwamba hakuna hata mzazi mmoja kati ya wazazi wetu ambaye alipitia shule.
Tulipokuwa darasa la Tano, tulipenda sana kwenda kuwasaidia wazazi hususan baada ya kutoka shuleni. ulifika muda tukaweza kufanya biashara ndogo ndogo na tuliweza kushindana namna ya kusevu kiasi Cha pesa tulichopata na kila mmoja alimtambia mwenzie wakati wa sikukuu kwa kuvunja vibubu vyetu tulivyoweka kiasi Cha sarafu tulizopata. baada ya kuhitimu darasa la saba wote tulifanikiwa kufaulu kuendelea na masomo ya shule ya sekondari, lakini rafiki yangu Mido alikataa, na kumsihi mzazi wake kuwa anataka kuendelea na biashara. Ilipofika muda wa kujiunga na shule ya sekondari ilinilazimu kutembea umbali usiopungua kilomita kumi kwenda ilipokuepo shule ya sekondari.
Niliteseka sana, sikuwa hata na pesa ya kununulia baiskeli, wazazi walinishauri kuachana na mateso hayo na kunitolea mfano kwa rafiki yangu Mido kuwa maisha yake yanaenda vizuri, amepanga chumba na anakaribia kuoa. Niliumizwa sana na jibu hilo maana hata umuhimu wa elimu haukuonekana kutoka Kwa familia yangu maana walinisisitiza kuwa hawana pesa ya kunisomesha.
Niliendelea kusoma na ilifika kipindi nikawa naishi katika nyumba ya wazazi wa mwanafunzi mwenzangu tuliojenga urafiki na utamaduni wa kusoma pamoja. nilimaliza kidato cha nne na kufauru katika shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Tabora.
Hakuna kipindi kigumu kama wakati wa kusubiri matokeo ya kidato cha nne ambapo nilikaa nyumbani na kuonekana kijana mvivu na niliochoka kwani sikuwa na pesa wala mahusiano, nilikonda na wala sikuwa na nguo nzuri za kuvaa. Wapo waliozani nimechanganyikiwa kwa kupenda kusoma. Niliunga nauli na ada na kwenda kujiunga na wenzangu wa kidato cha tano kwa kuchelewa sana. Nilifanikiwa kuhitimu kidato Cha sita na kujiunga chuo kikuu cha Mlimani kwa ufadhiri wa serikali.
Baada ya hapo nikafanikiwa kuhitimu shahada yangu ya kwanza katika fani ya uhandisi.
Nilirudi nyumbani kwa wazazi na kuanza kufanya mchakato wa kutafuta kazi. Niliangaika kutuma barua katika makampuni mbalimbali kupitia mitandao na kwa njia ya posta. Nilifanya usaihili katika makampuni yasiopungua mia mbili pasipo mafanikio yoyote. Siku moja nilifika kipindi nikakata tamaa nikiwa mtaani, nikaanza kujihusisha na shughuli ndogo ndogo za kuendesha boda boda. nilijikaza japo njilijisikia vibaya kwa kunyooshewa vidole na watu. nilikuwa mfano mbaya sana kwa watu wakinihusisha kuwa kusoma hakuna maana, kwa maana nimepoteza muda mwingi pasipo mafanikio na kuangukia katika fani ya kuendesha boda boda.
Mbali ya yote niliopita sikuacha kusoma majarida mbali mbali yahusuyo fani yangu ya uhandisi pamoja na njia mbali mbali za uwekezaji.
siku moja tajiri alionipa bodaboda alikuja kuninyang'anya boda Boda yake kwa kutoweza kutimiza masharti ya mkataba.
Niliumia sana na kwenda kwa rafiki yangu mido ili aweze kunisaidia.
Mido aliumizwa sana na suala langu, akanishauri anipe msingi na Mimi nifanye biashara.
yeye alikuwa na duka kubwa sana pale kinijini ambalo amedumu nalo kwa muda mrefu pasipo kufilisika.
Akanishauri namna ya kuanza biashara akanikopesha mtaji. Kiukweli sikuwa na wazo lolote juu ya biashara japo nilikua na maarifa ya shuleni juu ya kuwekeza na ujasiliamali. Sikumoja nilipita katika mtandao nikaona namna ya jinsi unavyoweza kujiajiri kama mhandisi. niliangalia mafunzo mbali mbali kupitia mtandao. ikafika wakati nikaona uwezo wa kufanya Ile biashara ni mdogo sana kwani niliandamwa na mikopo midogo midogo na nilishindwa kuendeleza biashara. Siku Moja nikaamua kutoka kijijini na kwenda jijini Dar es salaam, nikaomba kujitolea katika kampuni ndogo Sana ya kufanya marekebisho ya majenereta na magari. nilifanya kazi kwa weredi na bidii pasipo kuwa na mshahara wa maana. Sikuangalia pesa, sikuwa na pesa japo niliangalia kupata ujuzi.
Ilipofika miaka kazaa nilipata uzoefu sana katika fani yangu ya uhandisi. watu walifika na kuniulizia Mimi, nisipokuepo walikataa kazi zao zisifanyike mpaka nitie mkono wangu. Bosi wangu siku moja akaniita ofisini kwake, akaniambia juu ya kusaini mkataba wa kudumu na kuniahidi donge nono la mshahara, kiukweli nilikataa mshahara wake, na kumueleza Nia yangu ya kufungua biashara yangu binafsi. Bosi alisikitika sana lakini alinipa moyo.
Leo nimefungua kampuni yangu kubwa na nimeajiri watu wasiopungua ishirini. Nina uwezo wa kutengeneza kiasi Cha shilingi milioni kumi na sita kwa mwezi nimejenga na Nina maisha mazuri.
Siku Moja nilipata ugeni kutoka kwa rafiki yangu Mido ambaye nimempokea na akanieleza juu ya kufiliswa kwake na bank kutokana na mikopo ya muda mrefu, yeye aliwekeza katika ujenzi nyumba yake na familia pasipo kuweka misingi ya marejesho ya bishara. nimemuajiri Mido kama afisa masoko katika kampuni yangu, lakini Mido akanifuata na kuniomba ushauri nimsapoti Ili aende kujiendeleza katika masomo.
Hoja;
Mimi niliwekeza katika elimu Kisha katika fani.
Mido aliwekeza katika biashara.
Cha kutambua ni kwamba biashara sio fani, japo fani inaweza kuwa biashara. watu wengi sana wamekuwa wakikimbilia kufanya biashara pasipokuwa na fani inayoweza kufanya kuwa biashara, japo kuwekeza katika fani ni kitu ambacho unatakiwa uwekeze muda na akili na uvumilivu ndipo ujue kuwa fani Yako unaweza kuifanya kuwa biashara na kujiajiri. asikuambie mtu ukifanya biashara inayoendana na fani yako lazima utoboe!
Wito;
Napenda kutoa wito kwa serikali yetu kupitia vyuo vikuu na vyuo vya ufundi, kuwezesha wanafunzi kupata elimu itayojenga fani, na tafiti zenye tija kwa maendeleo yetu , sio tu kuwekeza katika elimu ya kukalili na kujibu mitihani. najua elimu ni pana sana lakini ikitolewa kwa uwezo wa kujenga mwanafunzi kujiajili itajenga uwezo wa wasomi wetu kujiamini na kujua thamani Yao na sio kutembea na bahasha na kuomba ajira pasipokuwa na ujuzi wowote.
Rai;
Mfumo wa elimu yetu pendwa unatakiwa marekebisho na kujenga ufanisi kwa wanafunzi wasome kwa vitendo na kujenga ujuzi imara, Ili tuwe na jamii zinazoweza kutatua matatizo yake na kuleta maendeleo chanya katika taifa letu. sio TU tafiti za maprofesa bali tafiti ziwekwe kuanzia ngazi ya sekondari na wanafunzi wapewe elimu ya kutosha kuchagua ni fani gani itaendana na talanta zao, pasipo kupanga kulingana na ufaulu TU wa matokeo.

Upvote
8