Nilicho jifunza kutoka Rwanda

Tanzania ni sawa na mtu mwenye kichwa kikubwa kisichokuwa na akili.
 
Kwa hiyo alichagua matajiri wachache nakuacha wachache?
Wewe binafsi alikupora Bilioni ngapi?
Wewe unajadili hii ishu kwa hisia badala ya facts...

BTW, hoja yako nini hasa hapa..?

Je, unataka kutuambia kuwa utawala wa hayati Magufuli haukupora watu (matajiri) wasio wa itikadi sawa na yake fedha kibabe..?

M/kiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe ni mmoja wa walioporwa na alisema hili hadharani yeye mwenyewe mbele ya TV cameras...

Najua utasema, huyo alikuwa mwizi wa pesa za ruzuku za CHADEMA (maana ndio wimbo wa uVCCM). Na kama unadhani hivyo, basi nasikitika kukusema kuwa, wewe utakuwa MJINGA kwelikweli kwa sababu umvivu wa kutafuta facts bali unapenda udaku..!

Again, kwani wezi hupelekwa wapi? Si mahakamani? Kama aliowapora fedha wangekuwa wezi, kwanini hawa kupelekwa mahakamani, washitakiwe na kisha serikali ichukue kihalali kilichoibwa..?
 
Nimeona blah blah na neno Mbowe sijui uVCCM hakuna ulichoandika.
Ukiwa na hela zako clean hakuna atakayekugusa. ( hii ndio hoja yangu, kama bado unataka kujua nachotetea ni nini).
Hayo mengine hayanihusu mimi.
 
Ndiyo maana OP kasema kuwe na madarsana hata ya jioni ya kujifunza lugha. Mwisho kabisa OP kasema LUGHA NI AJIRA
Ndio, kwa upande wa kufundisha lugha WANYARWANDA huwa wapo vizuri sana na mimi BINAFSI nilishawahi kukutana na WANYARWANDA wanaotumia zaidi ya LUGHA NNE za KIMATAIFA.

Pale KIGALI, nilikutana na jamaa mmoja alikuwa anaongea kwa ufasaha LUGHA ya KISWAHILI, KINYARWANDA, KIINGEREZA, KIFARANSA na KILINGALA.
 
Nimeona blah blah na neno Mbowe sijui uVCCM hakuna ulichoandika.
Ukiwa na hela zako clean hakuna atakayekugusa. ( hii ndio hoja yangu, kama bado unataka kujua nachotetea ni nini).
Hayo mengine hayanihusu mimi.
Mr. Illmatic, You a problem to yourself...

Jitendee haki mwenyewe. Acha kujitweza kwa kujitoa ufahamu kiasi cha kushindwa kujenga hoja kwa kinachojadiliwa hapa...

Anyway, it doesn't matter because may be, you are mental capibilty to think and digest things perfectly is weak...

All in all, my argument is very simple. Sijui kwanini hujaelewa kiasi cha kupotezea kwa kuandika maandishi matupu yasiyo na substance yoyote...

Nimesema Kwamba, kama mtu ana hizo ulizoziita "hela chafu", ndo Magufuli apole kwa nguvu bila kufuata utaratibu wa kisheria...? Really?

I know, you understand that, nchi hii ina taratibu na kisheria za kushughulikia uhalifu wa mtu yeyote wakiwemo wenye hizo ulizoziita "hela chafu"...

Sasa unaweza kusema neno ni kwanini baba yenu Magufuli hakufuata utaratibu huu..?

I will appreciate kama utaacha utoto na badala yake ujadili ishu hii kwa hoja. Na ukiwa huna neno, pia utakuwa na akili sana ukinyamaza kimya tu. Hakuna atakayekuona mjinga...!
 
Kwa hali hii itatuchukua karne nyingi kutoka hapa tulipo kusonga mbele. Shida viongozi walio wengi wanatokana na system ya uongozi kwa maana ya kwamba kama kuna mtu wa kukushika mkono kwenye siasa za nchi hii basi kuna siku utaukwaa uongozi. Tumeshuhudia kipindi fulani uongozi ulikuwa ni takrima, kulipa fadhila kiasi kwamba kuchonga mdomo na kujikomba kumezalisha viongozi wa aina yake.
Hakutakuwa na tija kwenye uongozi wa kuzawadia mtu na hakutakuwa uwezo wa kujenga hoja iwapo mambo yatakuwa hayaendi sawa mahali fulani kwa uoga wa kutengwa na system. Hata kama uongozi wa juu utakuwa na mipango mizuri watendaji wa kujikomba wataharibu tu. Kama tunaka kwenda tenganisha siasa na utendaji.
 
Viongozi wameendelea kuacha sheria mbovu kuendelea kutumika ( mfano tukubali kuwa na sheria kuwa kiongozi ajue kusoma na kuandika,sheria ya uchaguzi yenye kipengele "mshindi ni aliyetangazwa na sio aliyepata kura nyingi").

Viongozi wa kisiasa kupatikana kutokana na sheria,kanuni na utaratibu mbovu imechangia kuwa na viongozi wasio kubalika na wasio na utashi wa kumletea mwananchi maendeleo(kama kiongozi aliiba kura,ataacha kuiba rasilimali,au ataweza kuwa na uchungu na rasilimali za taifa?!)

Nia ya maendeleo haipo miongoni mwa viongozi wanao wakilisha wananchi (kutokuwa tayari kurekebisha sheria zilizopitwa na wakati, na wakati mwingine kukubali kupitisha sheria mbovu zenye kudhulumu na kukandamiza).

Inaonakana,inajulikana na inaendelea na wananchi wanaona;Kila mwenye uwezo anampeleka mtoto shule za "english medium",lakini viongozi wanaendelea kusema kiswahili kifundishwe masomo yote hadi chuo kikuu. Hivi kubadili mfumo wa elimu ni gharama kiasi gani?

Inaonakana,inajulikana na inaendelea na wananchi wanaona viongozi tena wa ngazi za juu wanafanya makosa hadharani kwa kukiuka sheria na taratibu kwa kuingilia kazi za kitaalamu kwa kutoa matamko katika maeneo ambayo hawana weledi na bila mashauriano na wataalamu.Viongozi wanashindwa nini kujadili ya kitaalamu katika vikao ndani na mambo nanayohusu siasa ndio yaende kwenye mikutano ya hadhara?

Tunasema tunataka kuimarisha na kukuza uchumi, kweli Mji Dar es salaam barabara zinaboreshwa kupunguza msongamano, lakini kwa nini barabara haipanuliwi hadi Chalinze ili kupuguza msongamano wa magari yaendayo mikoani na nchi jirani?
 
Wanajitambua
 
Population yao pia inachangia

Ova
 
Kagame mwanaume aliyefunga makanisa na misikitu elfu sita.. Akiwataka maustadhi na wachungaji kuwa na degree ya theology .. pia waache kucheza na imani za watu KWA kuwafanya vitega Uchumi vyao...
Anaendelea KWA kusema Rwanda ilishabarikiwa kitambo.
 
wanasema Rwanda inaiba rasilimali za Congo ndo maana uchumi wake pamoja na nchi inakimbia kimaendeleo,wakati huo Rais Samia anasema Tanzania tuna madini mengi mpaka mengine hatujui yanaitwaje na bado tupo tupo tu yani.
Kwa hiyo Rwanda wanazidi Tanzania mafanikio sio
 
wanasema Rwanda inaiba rasilimali za Congo ndo maana uchumi wake pamoja na nchi inakimbia kimaendeleo,wakati huo Rais Samia anasema Tanzania tuna madini mengi mpaka mengine hatujui yanaitwaje na bado tupo tupo tu yani.
Rwanda wana GDP ya 12 bilioni

Uku Tanzania 65
Wanani wana maendeleo zaidi

Sema Rwanda unaona ina maendeleo kwasababu ni ndogo saana na population yake ni ndogo zaidi ya Tanzania
 
Rwanda wana GDP ya 12 bilioni

Uku Tanzania 65
Wanani wana maendeleo zaidi

Sema Rwanda unaona ina maendeleo kwasababu ni ndogo saana na population yake ni ndogo zaidi ya Tanzania
unasema Rwanda inamaendeleo kwasababu ni ndogo sana,udogo sio sababu mkuu zipo nchi nyingi ndogo lakini hazina maendeleo ukilinganisha na ustawi wa nchi ndogo ya Rawanda.
 
Hata nyumbani baba akiwa mkali ili alete maendeleo anaitwa dictator, inatakiwa u-dictate ili mambo yaende bila kuangalia makunyanzi. Siamini ila nasikia kapiga marufuku yale makelele ya msikitini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…