Nilichojifunza kuhusu maisha

Nilichojifunza kuhusu maisha

magumbugu

Senior Member
Joined
Sep 27, 2017
Posts
143
Reaction score
266
Unaweza kuzungukwa na watu 1000 na katika watu hao asiwepo hata mmoja ambae atakuwa rafiki na mtu wa kweli, tumezungukwa na watu wengi na wapo kwenye maisha yetu kwa sababu wanajua kupitia wewe utamvusha na kumfikisha anapotaka na hatajali kuanguka au kusimama kwako, watakuchekea na kukuweka karibu yao ila ukweli ni kwamba unatumika tuu kwa muda

Wakati wa dhiki, kukosa , wakati ambao utakosa kabisa, wakati ambao utapata matatizo ndipo utakapowajua kwa tabia zao. Wapo watakaokubeza, watakao kusema, watakao kucheka , watakao kupiga picha na kusambaza kwa watu waone jinsi gani maisha yamekuchapa, watazua stori mbalimbali kuhusu wewe, wataelezea namna gani ulikua unayafurahia maisha wakidhani wewe ni mzembe, wapo utakaowapigia simu watakuona kero, msumbufu, wapo watakaokublock na watasahau namna ulifanyika daraja kuvuka.

Binadamu tunabadilika sana, binadamu hua tunasahau tulipotolewa na watu, akitokea mtu akakubeba wakati wa dhiki yako, akakusitiri kipindi ambacho wengine wanakucheka, akafunika aibu yako mbele za watu mtu huyo usimuache Mungu atakapokuinua tena. Kushuka kwenye maisha sio mwisho wa maisha bali kuinuka tena ndipo ushindi ulipo.
 
Nazn kwenye cmu nina number 1000 maximum,

Tuseme active number 100 (ambao n ndugu,jamaa na marafk ambao tulijuan by physical) lakn katk watu mia nikiwa na shida nawez kuw na watu chin ya 5 wanaowez nisaidia lakn pia 2 ndio wanawez nisaidia kwa wakat

Maisha 95% ni wew ukipata mtu ambae anawe kukutumia ata 1000 la vocha huyo n mtu ,
Stay humble
 
Back
Top Bottom