Siasa Basi
JF-Expert Member
- Jul 10, 2016
- 1,493
- 4,281
We umeyataja ya nini?Soma points achana na majina ya watu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We umeyataja ya nini?Soma points achana na majina ya watu.
Bangi tupu,ulipotaja jina la Tunda tu nikaona huyu mleta uzi atakuwa yupo na stimu za ganja kichwani.Habari wapendwa
Nami leo nimeona niandike machache kuhusu nilichojifunza kupitia sakata la Mr Kuku. Nimepata msukumo zaidi baada ya kuona lawama ni nyingi zaidi hasa kwa Serikali (DPP) na wengine kwenda mbali kwa kukilaumu Chama Cha Mapinduzi. Niseme tu kwamba serikali hii ya Mh Dr John Magufuli chini ya CCM ni serikali inayojali na kutaka wananchi wake wapige hatua kimaendeleo. Ilani ya uchaguzi ya chama imeweka wazi. TUJIKUMBUSHE kuibuka vijana mamilionea kwenye awamu hii kama Diamond Platinumz, Fred Vunjabei, Lemutuz Superbrand, Edo Kumwembe, Shilole, Frank Knows, Diper Rato, Tunda Capuccino na wengine wengi.
Mr Kuku alikuwa na nia nzuri lakini utekelezaji mbovu. Mabeberu husema "the end justifies the means" kwamba ile tamati ndo huhalalisha mbinu zilizotumika kufika. Kama mwisho ukawa mbaya basi mbinu zilikuwa mbaya. Kwangu mimi Mr Kuku ni kijana mbunifu, mwenye akili nyingi na ushawishi wa hali ya juu. Ni wa kipekee. Tatizo lake alitumia njia za ovyo kwenye kutimiza ndoto zake. Je kwanini mbinu zake ziwe ovyo?
Kwanza yawezekana alikuwa na wazo ila mikakati ya kutekeleza alikuwa hana. Au alikuwa na wazo na mikakati lakini watu wa kumsaidia kutekeleza wakawa hawapo. Au alikuwa na wazo, mikakati, watu akawa hana uwezo wa kuongoza timu. Tukirudi nyuma kidogo tujikumbushe kuwa Mr Kuku ni kijana sana ambaye hajatoka familia tajiri kwahiyo kuna uwezekano alianza kushangilia ushindi mapema wakati ndo ilitakiwa akaze zaidi. Mr Kuku kwa umri wake bado ana nafasi ya kuwa zaidi ya pale mwanzo kama atatulia na kujipanga. Namwombea kwa Mungu apate ujasiri pia wa kumalizana na wanaomdai, kama serikali haijamnyang'anya mabanda ya kuku na mali zake zingine akae na waliowekeza kuona jinsi gani kwa pamoja wanaweza wakaendeleza walipoishia.
Machozi yanitiririka ninapoona vijana wengi waliotoka familia maskini kusoma kwa tabu kisha kuishia kwenye majanga kama haya. Vijana wengi toka familia maskini kwa sasa hupata mafanikio makubwa lakini hushindwa kuyamiliki haya mafanikio na kuishia kwenye matatizo. Baraka zinageuka laana. Tukiangalia kwenye sanaa kuna vijana wengi hupata umaarufu lakini hudumu kwa muda mfupi. Je tatizo ni nini? Wazazi tufundishe watoto kuwa mafanikio kwa njia za halali inawezekana. Tuache upumbavu wa kuwajaza akili mbovu kwamba mtoto soma uje upate kazi BOT au TRA kuna marupurupu kumbe bila kujua tunatengeneza mafisadi wa baadae. Wazazi wengine pia acheni zile kauli kwa vijana wenu kwamba wamezubaa sio kama mtoto wa fulani. Waacheni vijana wenu wafanye wanachofanya ili mradi hawavunji sheria za Mungu na za jamhuri. DPP pia awafilisi baadhi ya Motivational Speakers. Wana mchango wao kuwajaza vijana ndoto zisizowezekana.
nimesoma nkaishia hapohapo kwa edu na tunda kuwa nimamilionaire.Point yako nn umeongea pumba tu kina edo kumwembe ni mamilionea kina limutuz Uzi wa hovyo kabisa
Nimeona mpka Tunda yupo...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Jamaa itakuwa ana matatizo ya akiliPoint yako nn umeongea pumba tu kina edo kumwembe ni mamilionea kina limutuz Uzi wa hovyo kabisa
Tatizo hadi Forbes watoe list ndo muamini. Msiamini kila kitu cha mabeberu.Nimeona mpka Tunda yupo...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Jamaa itakuwa ana matatizo ya akili
TUJIKUMBUSHE kuibuka vijana mamilionea kwenye awamu hii kama Diamond Platinumz, Fred Vunjabei, Lemutuz Superbrand, Edo Kumwembe, Shilole, Frank Knows, Diper Rato, Tunda Capuccino na wengine wengi.
Jamaa kaandika pumba la kiwango kikubwa sana, kwanza nilihisi analeta utani nikaja kugundua yuko serious sana.Point yako nn umeongea pumba tu kina edo kumwembe ni mamilionea kina limutuz Uzi wa hovyo kabisa
Usifanye maisha magumu kiasi hicho... vijana huwa tunaitana Kiongozi, mkuu, boss nk huku hatuna uongozi wala uboss. Relax.. zingatia points zilizopoSasa naanza kujua ni kwanini tunashauriwa kuandika kwa aya,Aya ya kwanza imeharibu bandiko lote.Unataja taja watu kuwa ni mamilionaire hujui ni kesi hiyo? Unamtaja mtu wakati ata TRA hawamtambui kama ni mlipa kodi
Utakuwa umepigwa kimango kirefu mzee sio kwa hii comment yenye ugwadu mkali 😁😁😁!We unaandika nadharia tu, sisi ndo tunajua ufedhuli wake kwa sababu hizo 5.4 bil ni sehemu ya fedha zetu na wala hahitaji kutetewa. Alifanya akijua alichofanya, kwa vile sheria ipo hivyo ila adhabu na uharibifu alifanya haviendani. Hizo 5.4bil ni mali za watu alizozulumu kwa makusudi kabisa.
Alichofanya kinasababisha vijana kutoaminiwa hata km watakuwa na lengo zuri, lakini kinarudisha nyuma dhana ya uwekezaji wa ndani kwa njia ya ushirika.
[emoji23][emoji23] [emoji1787][emoji1787]U
Utakuwa umepigwa kimango kirefu mzee sio kwa hii comment yenye ugwadu mkali [emoji16][emoji16][emoji16]!
Usisahau kuwekeza kwenye bitcoin mpya ile naona kuna kenge kashaanza kuipromote majukwaani hapa JF.
Nakumbuka waliambiwa humu, kuna bwege mmoja akaja na concept ya crowd farming, ooh wabongo washamba sana hii ni crowd farming model inatumika sana Nigeria 😂😂😂 na lengo ni kumobilize resources kwa wasio na mitaji mikubwa ili kushea sijui na blaa blaah nikasema hiii! Wacha movie iendelee[emoji23][emoji23] [emoji1787][emoji1787]
Naona watu wana hasira sana na mtoa mada utafikiri yeye ndiyo Mr Kuku! Na wapigwe tu maana wajinga hatujawahi kuisha duniani!
Habari zinasema watu zaidi ya 50 wamelizwa na Mr Kuku.Wengi waliomshambulia mtoa mada bila shaka walishapigwa na huyo Mr Kuku! Siyo bure!
Maana haiwezekani comments karibu zote zinaongelea hiyo list ya majina ya millionaires tu na kuacha hata hiyo aya ya mwisho ambayo angalau ina ujumbe unaoeleweka! Pathetic!
Habari zinasema watu zaidi ya 50 wamelizwa na Mr KukuWengi waliomshambulia mtoa mada bila shaka walishapigwa na huyo Mr Kuku! Siyo bure!
Maana haiwezekani comments karibu zote zinaongelea hiyo list ya majina ya millionaires tu na kuacha hata hiyo aya ya mwisho ambayo angalau ina ujumbe unaoeleweka! Pathetic!
Hahaahah.. kweli nakumbuka nilisomaga hiyo comment. Nimejifunza hawa wafanyabiashara wanaoenda kwenye Media na kujitangaza mambo yao ya ndani huwa mwisho unakuwa mbovu hasa vijana. Kwa mfano yule Patric Ngowi wa Solar, Shamim wa kibubu na wengine wa aina hiyo. Sasa hivi kuna Vunjabei... kimsingi vijana watulie mafanikio yatajitangaza tu yenyewe hakuna haja ya kwenda kwenye media na kusema nina utajiri wa 4billion.Nakumbuka waliambiwa humu, kuna bwege mmoja akaja na concept ya crowd farming, ooh wabongo washamba sana hii ni crowd farming model inatumika sana Nigeria 😂😂😂 na lengo ni kumobilize resources kwa wasio na mitaji mikubwa ili kushea sijui na blaa blaah nikasema hiii! Wacha movie iendelee
Nilikua najiuliza hilo swaliWe jamaa sio mzima wewe asee. LeMutuz na Tunda na Shilole ni mamilionea?
Yaani mifano yako imeuondolea credibility uzi wako wote
Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app