Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,814
- 2,738
Mwaka 2017 nilipeana rasmi mkono wa kwaheri na mwajiri wangu Simba Technology ,Posta Dar es slaam. Maagano ya ya kirafiki na bashasha kila mmoja akimtakia mwenziye kila la kheri.Hapo nilikuwa nimetumia miaka 3 kudeal na biashara ya sabuni asilia kwa muda wa ziada wa ajira ,iwe usiku,weekend hadi likizo ya mwisho wa mwaka.Biashara ilianguka na kusimama mara zaidi ya 3, Na safari hii niliapa ‘imma shahada waimma naswra’yaani ni iwe ushindi au iwe kifo naenda kusimama kwa miguu yangu (kujiajiri)
Cha kwanza nikabadili makazi ya bei kubwa nikaja makazi ya bei nafuu ili nyumba iwe ni ofisi pia ya kuzalisha bidhaa na kuuza sabuni online. Nikapata Mpakani na Dar , yaani Maili moja –Kibaha.
Kwa kuwa naanza sina timu ya uzalishaji wala mauzo , nikajigawa.Usiku nazalisha sabuni, asubuh nashinda internet café kusaka wateja online.
Wateja unawagroup kwenye whatsapp kuwapa elimu ya madhara ya vipodozi kemikali, nao wakipona wanawaambia wenzao(One bring one). Likijaa group au wakifika mia mbili unaunda group lingine ili kujibu kwa urahisi maswali yao.
Tulianza kuwauzia sabuni tu, wakapendekeza pia lotion zao licha ya kununua bei kubwa ,zinazeesha ngozi kila wakistop kuzitumia )Ni kama zimeandaliwa wawe addicted nazo) ,hiyo ni pamoja na watumia tyubu za pharmacy.
Hapo ikabidi tufanye kozi za SIDO za uandaaji lotion, Pia tufanye kozi Muhimbili kitengo cha tiba asili na mimea(MUHAS) na kuanza kuwahudumia
Baadaye wakapendekeza vipodozi wapendavyo ila tuviweke kwenye mimea. Safari hii sasa ilibidi tufanye kozi nje ya nchi kabisa.Mwanzo Dubai mwaka 2022. Kisha Guangzhou –China mwaka 2023.
Uwekeza huu wa ziara za nje ulituletea matunda mengi ikiwa ni pmoja kufungua akili na kujua uaandaaji a bidhaa zote za ngozi ka kutumi amimea ikiwemo sunscreen, serum, toner,cleanser,Moisturise, scrub.Pia Wakaja na ushauri pia wamechoka kuvaa mawigi ,nywele zao zimeharibiwa na madawa ya saluni na kukaa kwenye draya. Ikabidi tukafanye mafunzo tena ya uaandaaji bidhaa za nywele asilia kama hair oil,steaming ,conditioner na shampoo. Hapo tukawa full package tumeelewa ulimwengu wa vipodozi asilia.
Hitimisho , Chagua biashara ikiwa na vitu vitatu
Scalable – Chagua biashara inatanuka siku baada ya siku. Mteja mmoja ataongeza kiasi cha huduma au bidhaa anazochukua siku bada ya siku.Mteja wa sabuni mwaka 2017 ,leo 2025 anaagiza bidhaa 10. Hapo kabla hajamwambia rafiki yake.
Mass Market- Lenga tabaka la chini ndiyo wengi. Bidhaa za bei elf 20 , elf 15 au elf 10 za vipodozi zinauzika kiurahisi.Na biashara inayotengeneza faida kidogo per unit, ila mauzo makubwa ,ndiyo biashara ya kufanya.
Technology Update- Nikiwa nimeajiriwa niliamini kuwekeza mafunzo ya mara kwa mara na kutumia technology ni gharama. Ila baada ya kujaribu na kuona matunda yake, naamini ingawa mafunzo na technology ni gharama,lakini biashara ya kimazoea bila update za mafunzo na technology ni gharamza zaidi.
Mwisho kwa sasa furaha yetu ni mafunzo kwa wengine mtu mmoja mmoja,Familia, vikundi, VICOBA, Ofisi n.k ili tuhudumie watanzania milioni 60 kwa vipodozi asilia.Kwani mimi ni binadamu nina mwisho, nimeona bora nirithishe ujuzi kwa watanzania wenzangu .Karibuni nyooooote.
Dr.Zaganza
Kibaha
0713 039 875