Smith Rowe
JF-Expert Member
- Sep 18, 2018
- 4,319
- 9,003
PambanaSijawahi kuikubali Arusha kwa lolote lile, panaboa sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
PambanaSijawahi kuikubali Arusha kwa lolote lile, panaboa sana
WabobevuMasahihisho: Arusha hawana daladala bali wana vifodi.
Vifodi ni miaka ya tisini, neno tunalotumia wazawa mara nyingi hiaceMasahihisho: Arusha hawana daladala bali wana vifodi.
Mkuu simu kwenye kibegi tena!!Hao vibaka wa arusha ni wazembe sana uwa wanajifanya nao ni abiria wakishaiba ndani ya hiace wanashukia njiani, mi kuna kipindi 2018 nilipanda nao kwa mrombo-kilombero wakanipiga tecno y3 yangu wakataka kushukia corner ya mbauda nikastuka kucheck kwenye kibag sina simu nilishuka nao wakatoa simu[emoji23][emoji23]wengine pia wanafahamiana na drivers na kondactors.
Madingi sio poa huwa wanashirikiana na machalii kupiga sho8Kilichoniuma ni mzee kupigwa makofi na konda bila kuangalia umri wake
Ndio maana gesi haikuishi mkuu..Mimi roho yangu nyepesi mno,siwezi shuhudia mwizi akipigwa.
Hii huruma yangu iko siku itaniponza kama huyo mzee.
Nilishawahi pigwa tukio back town baada ya kula masanga sasa na mimi siku hiyo mitaa ya idara ya maji nikakuta mwizi anashushiwa kichapo kwa kweli nilimalizia hasira zangu paleChunga sana kutembea usiku maeneo ambayo wewe sio mwenyeji. Pia kuwa makini sana ikishafika usiku hiyo njia kuanzia Kilombero mpaka mbele kidogo ya Soko Mjinga (Embassy Garage) hiyo njia hapo ina wahuni wa Ngarenaro ukijichanganya tu hata ukiwa kwenye gari unapigwa tukio fresh tu.
Nimekaa sana hapo Back Town (Ngarenaro) watu wanapigwa matukio hata mchana kweupe kwenye magari yani kibaka anakuwa kama anavuka road ukiwe kioo kipo wazi na unachat au unaongea na simu inatembea au hata pochi. Na ubaya wa hapo Ngarenaro mpaka Soko Mjinga yani ukivula tu lami upande wa chini hatua tano ushaingia vichocho so mwizi akikwapua tu hatua tano humuoni ni machocho yakufa mtu huko huingii kama sio mwenyeji hata kama ni mchana.
Usiku ukipita kwa mguu imekula kwako. Ukipata breakdown hayo maeneo imekula. Machalii wa Matejoo na Ngarna ndio kituo chao cha kazi hiyo road kuanzia mida ya saa moja usiku.
Kuhusu wizi kwenye vi hiace (vifodi) au coaster (baadhi ya sehemu zipo coaster) hilo sio kwa Morombo tu au Olasiti kama ulivyosema mleta mada. Hilo ni suala la nchi nzima popote pale ukikaa kiree hasa kwenye haya mausafiri ya kunabanana lazima wahuni wakuoshe.