CCM wana pesa
Wana pesa za kuwalipa mamluki wakaja huku na kutuchafua kwa hoja zao za kipuuzi, zisizo na nguvu wala msingi. Nawaita "agent provocateurs"!
Wana pesa za kuzilipa NGO "feki", kama REDET, kutoa ripoti za utafiti "hewa", kuonesha kwamba JK anakubalika, huku wakiujua ukweli!
Wana pesa za kukodisha mabasi na malori, ya kuwapeleka "wapiga debe na washangiliaji" kwenye mikutano ya kampeni za JK!
Wana pesa za kuwalipa vijana wasio na kazi kushika mapanga, sime na mawe, kwenda kuwashambulia wagombea ubunge wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani.
Wana pesa za kuweka mabango huku na kule, kila upitapo, barabarani, hata kwenye kuta za nyumba zetu.
CCM wana pesa.
Lakini CCM hawana vitu hivi:
Hawana mapenzi ya watu, wanaofurika kwa mamia na maelfu, kwenye mikutano ya Dr. Slaa na wagombea wengine wa CHADEMA!
Hawana utashi wa watu walioamua, kufa na kupona, kumpigia kura Dk. Slaa, na KUZILINDA kura hizo zisichanganywe na zile feki, usiku, wakati wa kuhesabu kura kwenye vituo.
Hawana uamuzi wa watu walioamua kuichangia na kuisaidia CHADEMA, kwa hali na mali.
Hawana kauli ya watu wanaolalama, huku na kule, wakiilaani Serikali (ya CCM) na kiongozi wak (JK), kwa kuwapuuza, kuwanyanyasa na kuwadhihaki, miaka nenda rudi, wakitoa ahadi zisizotekelezwa na zisizotekelezeka.
Hawana kionambali cha watu wanaotaka mabadiliko, baada ya kushinda juani kutwa, wakilala sakafuni usiku, miaka nenda rudi, na baada ya utawala wa miaka 50, wamesema, SASA NI ZAMU YETU!
Tanzania itarudi mikononi mwa Watanzania, CCM walikubali hili... vinginevyo, kitachachotokea WATAKUWA LAWAMANI!
-> Mwana wa Haki