Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Sijawahi kuwa na utulivu kiasi hiki hasa nikisoma makala za kisiasa mtandaoni. Mubezi thanks kwa hili. Umekuwa objective...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
This is very informative, the big picture, general but deep, I believe its not too late for our kipeperushi journalist of the year, one and the only Maggid Mjengwa to learn!
Hakika wewe akili zako ni ndogo kama za Makamba au Kikwete. Huu ulimbukeni wa kuelezea kitu kifupi kwa kuweka hadithi ndeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeefu zisizo na kichwa wala miguu ni wa kizamani. Ubongo wako mdogo sana kuandikia gazeti kama raia mwema...
Ndugu yangu,
Ahsante sana,
Makala hiyo imeandikwa na rafiki yangu Godfrey Dilunga ( Raia Mwema)
Pamoja na kuwa ni kazi nzuri, lakini mimi nimekiona pia ambacho labda wengi wenu hamjakiona.
Maana, mtu mzima unaweza hata kujifunza kwa mtoto wa miaka sita. Unachotakiwa ni kuwa na utayari wa kujifunza. Kuna siku mtoto wangu wa miaka sita alinifundisha hili; Niliandaa uji wa ulezi wa asubuhi . Akawa wa kwanza kuamka kabla ya wenzake. Nikamwambia; Nenda mezani, chai tayari!.
Akaenda, baada ya sekunde chache akaniita; Baba njoo!
Nikaenda, akaniangalia usoni na kuniambia; Baba hii sio chai, huu ni uji!
Nikakiri mapungufu. Na mapungufu yale kwangu ni ya kimalezi, wengi tunayo. Tukiwa kuruta JKT enzi zile nakumbuka na usomi wetu wa form six, pale kambini Itende JKT, baada ya mchakamchaka wa alfajiri na usafi tuliambiwa na Afande Paul; Kuruta nendeni mkanywe chai!.
Wote tuliokuwa pale Kambini Itende, wengine tumo nao humu JF ni mashahidi, kuwa pale Itende tulikunywa maji ya moto yaliyochemshwa pamoja na vumbi la kahawa na sukari. Haikuwa chai. Lakini ni nani kati yetu alithubutu kumwambia afande Paul; Hii sio chai, ni kahawa, ingawa si kahawa hasa!
Tatizo hilo la kimalezi linatusumbua wengi wetu mpaka hii leo. Unaona kwa macho kuwa bwana mkubwa anakupa chungwa, halafu anakwambia; "pokea embe hili!" Wewe unakubali!
Mtoto wangu wa miaka sita anatupeleka kwenye kutafakari alichoandika ; Godfrey Dilunga; Nimeona waschotaka kukiona ( Raia Mwema)
Dilunga anaandika;
Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa.
Anaendelea kuandika; Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi. ( Dilunga, Raia Mwema)
Sasa hapa sijamwona aliyehoji na kudadisi uhakika wa anachokiandika Dilunga. Hivi ni kweli pale Ifakara Dilunga aliwaona watu 40, 000? Ifakara sikuwapo, lakini pale Mwembetogwa Iringa nilikuwapo. Watu waliofika pale hawakuzidi 5000. Ukubwa wa uwanja wa Mwembetogwa na maeneo ya jirani hauwezi ukajaa watu zaidi ya 5000 na wakaweza kumsikia anayezungumza achilia mbali kumwona kwa sura.
Ndio tatizo letu, tunapenda kusikia tunavyotaka kusikia, na kuona tunavyotaka kuona. Shilingi ina pande mbili, tuwe na ujasiri wa kuangalia upande wa pili wa shilingi. Ujasiri wa kuangalia tusivyotaka kuangalia, kusikiliza tusivyotaka kusikia. Sina cha kuhofia katika kuandika fikra zangu, maana ni fikra zangu. Fikra huru. Na najua kuwa mimi si malaika, nina mapungufu yangu. Ndio maana tukaitwa wanadamu. Najifunza kila siku, hata ninapokutana na mchoma mahindi pale Kitonga. Kijana aliyeishia darasa la saba, naamini nina nitakachojifunza kutoka kwake. Na kwa mwanadamu, katika yote unayayotakiwa kuyakubali. Usisahau kuukubali ushamba. Nimezaliwa mjini na kukulia mjini, tena Ilala, Dar. Lakini siku zote natanguliza ushamba wangu. Ndivyo nilivyo.
makala, iko kwenye gazeti la RAIA MWEMA, la jumatano, iliypita imeandikwa na GODFREY DILUNGAAhsante sana ndugu Mubezi kwa uchambuzi wako, bila shaka huyo mama ulimlipa ndizi zile.
Key message thanks!!!
Kuna kitu kimoja tu niwaongezee, kwamba although watu hawapendi changes/mageuzi kwenye mambo mbalimbali kiasili. Watu hao hao wanapenda mageuzi kwenye siasa sana!
Mfano ukiangalia jina la chama kinaitwa CCM litakueleza kwamba always in politics people like changes.... but they need realiable change ... not change b'se it is change!!!
Dr. Slaa ni tumaini katika kuona hizo changes, and people listen carefully to ensure reliability of change promised!!! Of course washabiki wanaenda mbali zaidi kuamini tayari wasikilizani wameshakubali!!! well a certain percentage yes, but still majority will need be assured whether promised changes will is reliable and credible.
Mfano wa kuonyesha wananchi wanapenda mageuzi ni wazee walikuwa wamefanya makubwa kwenye majimbo yao kama Mzee SJM, lakini akaondolewa na kijana... walifanya hivyo tu pale walipogundua kijana ana uwezo, na walifanya hivyo sio kwa sababa Mzee SJM hakuwa ana-uwezo no, it was b'se changes in politics is inenvitable.
My take
---> Kukubali kwamba watu wanapenda mabadiliko it is obvious
---> Kuelewa kwamba CHADEMA isipopata 30% ya kura za urais kwamba sio udhaifu wa Dr. Slaa bali ni kwamba people needs to process and assess credibility of changes they want to make.
---> Personally I won't give CHADEMA presidencial vote, b'se they were not serious in picking up the running mate, also they will not able to form government even if Dr. Slaa be a president per our current constitution zaidi ya kwamba watakwamishwa na chama kitakachokuwa na wabunge wengi which is obvious CCM.
--->Kura ya Mbunge na Diwani yes nitawapa wapinzani b'se I need them to build that credibility to be given vote for change.
--->Indeed kuipa CHADEMA urais sasa ni kuamini only one person can run a country... bila kuwa na nguzo nyuma!
makala, iko kwenye gazeti la RAIA MWEMA, la jumatano, iliypita imeandikwa na GODFREY DILUNGA