Nilichokiona kwenye ziara za Paul Makonda

EMACHA

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
771
Reaction score
1,478
Ziara za Komredi Makonda, na hasa anapowapambanisha watumishi wa umma na wananchi, zinadhihirisha udhaifu mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi.
 
Anashindwa kutatua changamoto za watumishi na wananchi.Anatakiwa awapatanishe ili washirikiane kuzikabili changamoto zao.Anawagombanisha ili iweje?Au ana pepo la uchonganishi akidhani ni sifa njema?
 
Wachumia tumbo msiogope. Hao wananchi ndiyo waliowachagua ninyi viongozi.

Kama unapiga kazi vizuri hofu ya nini? Mnabweteka sana ,acheni kijana awafunze na kuwashtua usingizini.
 
Nani alikuambia wafanyakazi wapo usingizini?Aache ujinga.Alisababisha hadi maafa kwa watumishi.
 
Wewe ni % ngapi ya wananchi wote hapa Tanzania?
Watu wanashida zao ,Acha Waone umuhimu wa kupata nafasi ya kusemea shida zao.

DAB PIGA KAZI
 
Nani alikuambia wafanyakazi wapo usingizini?Aache ujinga.Alisababisha hadi maafa kwa watumishi.
Kuna wale Watumishi wa Halimashauri kule Arusha, wamepima Aridhi ya Muhindi wa watu kimakosa,na kisha wakawauzia wananchi hivyo viwanja! Muhindi kwenda mahakamani akashinda kesi, Halmashauri badala wao ndiyo wamplipe mwenye eneo lake kama Mahakama ilivyo elekeza,eti wao zigo la hilo deni la Muhindi wamewatupia tena wale wananchi waliouziwa viwanja vilivyo pimwa! Yaani full uwonevu kwa wananchi wa kawaida!!
 
Anashindwa kutatua changamoto za watumishi na wananchi.Anatakiwa awapatanishe ili washirikiane kuzikabili changamoto zao.Anawagombanisha ili iweje?Au ana pepo la uchonganishi akidhani ni sifa njema?

Hiyo ndiyo kazi yake hasa katika chama.

Political agitation(uchochezi na ufitinishi).

Inaweza isiwe relevant kwa enzi za sasa lakini kumbuka CCM bado inajinasibu kufuata siasa za ujamaa.
 
Kuna wale Watumishi wa Halimashauri kule Arusha, wamepima Aridhi ya Muhindi wa watu kimakosa,na kisha wakawauzia wananchi hivyo viwanja! Muhindi kwenda mahakamani akashinda kesi, Halmashauri badala wao ndiyo wamplipe mwenye eneo lake kama Mahakama ilivyo elekeza,eti wao zigo la hilo deni la Muhindi wamewatupia tena wale wananchi waliouziwa viwanja vilivyo pimwa! Yaani full uwonevu kwa wananchi wa kawaida!!
Hiyo inaitwa "duble-duble"!Wapima wamejiongeza si kwamba walikuwa hawajui. Na wauziwa viwanja ni malofa wasiopenda kuchunguza vitu.Ngoma ngumu.
 
Hiyo ndiyo kazi yake hasa katika chama.

Political agitation(uchochezi na ufitinishi).

Inaweza isiwe relevant kwa enzi za sasa lakini kumbuka CCM bado inajinasibu kufuata siasa za ujamaa.
It's high time now!Akue kiakili.Akijiendekeza hivyo atazeeka akiwa mzee mjinga na mchawi.Ingawa kwao usukumani uchawi ni sifa njema.
 
Back
Top Bottom