Nilichokisikia kuhusu mkakati wa kummaliza kimuziki Belle 9

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
4,854
Reaction score
1,129
Jana nilikuwa napiga story mbili tatu na mdau mmoja wa muziki kuhusu kifo cha Mangwea pia zinazoitwa tuzo za KILI...Ni mengi tuliongea, ila lililonifanya nije na hii post ni kuhusu msanii Belle 9, ni habari iliyonishtua kidogo nikaona si mbaya nikija kushare hapa ili ukweli ujulikane, na hata kama ni story za kupika basi iwe wazi!!

Takribani miaka kama minne iliyopita inasemekana Belle 9 alienda kuonana na uongozi wa Clouds katika kuomba support juu ya kipaji chake, ila cha kusikitisha Ruge pamoja na wenzake wakamwambia dogo hawezi kuimba.

Belle aliondoka na akaenda RocaTz Records na kwa mara ya kwanza akarekodi "Sumu ya Penzi", ngoma ambayo ilipenya masikioni mwa wengi...
Katika kuonesha kwamba hakubahatisha, Belle 9 alikuja na "Masogange" ngoma ambayo ilisumbua vilivyo hali ilipolekea Clouds kumwita tena na kutaka kufanya naye kazi!!! Kilichotokea ni kwamba dogo alikataa na aliwaambia kuwa walisema hawezi kuimba na leo imekuwaje tena...Belle 9 alizidi kupewa msimamo na Afande Sele wa kuendelea kuwatosa Ruge na wenzake...
Baada ya hili sakata, ndipo Ruge na wenzake wakaapa kummaliza kimuziki Belle 9..
Mikakati ikawa kuwabeba kwa nguvu zote wasanii walioonekana kuzidiwa au kuwa sawa na naye!!

Ndiyo maana ukiwaangalia wasanii kama Ben Pol na Diamond huwez sema wana uwezo kumzidi Belle 9 ila ndiyo wanaopata airtime ya kutosha na kupewa tuzo. Cha kushangaza Belle 9 hatokei hata kwenye category ya hizo tuzo zao.

Kama umeusikiliza wimbo unaoitwa "listen" ni takribani miezi mitatu toka utoke, lakini sasa upo kapuni!!

Kila mtu anajiuliza kulikoni, wengine wanasema hana nyota, ila kilichopo kwake ni huo mkakati ambao kwa mujibu wa wapangaji wake...wameapa kwamba Belle 9 hawezi kumaliza hata mwaka toka sasa katika huu muziki!!!

@@@******@@@@
 
duh kama tetesi ni kweli basi wafu fm ni balaa

honestly namkubali belle9 lakin huwaga nashangaa kila mwaka
anatoka kapa tuzo za kili kichwani huwa najiuliza hivi
huyu kijana ni nyota yake haingai ama vipi ama hajui kuimba ama!!!!! ama!!!!

by the way hao sio mungu kama walimkatalia kumpa support
na akatoka without them basi he will continue to shine
 

huu ni umbeya hakuna kitu kibaya kama mwanaume mtu mzima kukaa chini na kupika umbeya na uzushi, unataka kuimbia dunia tuzo za ktma zinaratibiwa na cloudz fm??? mbona wasanii kibao tuu wanaoipinga cloudz fm akiwemo jide komando wamepata tuzo za ktma??? inahitaji moyo kweli kutunga stori za kimbeya
 

hivi ukienda kuomba sapoti mahali kumbe ni lazima upewe sapoti?? nilifikiri sapoti ni ombi tuu na si lazima mtu unayemuomba lazima akupe! Heaven on earth
 
Last edited by a moderator:
hivi ukienda kuomba sapoti mahali kumbe ni lazima upewe sapoti?? nilifikiri sapoti ni ombi tuu na si lazima mtu unayemuomba lazima akupe! Heaven on earth

yeah ni kweli kuna kukubaliwa na kukataliwa
ila kama ulinikataa mwanzo na kuniona siwezi je kuna umuhim wa kunifata
na kutaka niwe chini ya label yenu........

kama ilivyo ukiombwa kuna kukubaliwa na kukataliwa je kuna haja ya kutaka
kunishusha kimuziki kisa nilikataa kuwa chini yenu.....

naomba uclouds uuweke pembeni @be real
 

mkuu hizi ni tetesi kumbuka!!!
 
Kila muimbaji uchwara kapata excuse sasa kuwa nae ni miongoni wa wanaobaniwa na Clouds

Mara mseme Ruge hana uwezo wa kuzuwia soko mara mseme hamng'ari kisa Ruge

Hamueleweki
 
Yesuuu Wangu!!
Belle9 ni zaidi ya Diamond na Ben Pol???!
Kama hujui music, usiongelee music.
huo mfano wako umeharibu kabisa ujumbe uliokusudia.
Jesus!
 
Kila muimbaji uchwara kapata excuse sasa kuwa nae ni miongoni wa wanaobaniwa na Clouds

Mara mseme Ruge hana uwezo wa kuzuwia soko mara mseme hamng'ari kisa Ruge

Hamueleweki

Cha kushangaza wanasema tunzo za Kili zinaratibiwa na Clouds lakini wasanii wenye ugomvi na Clouds wakashinda, kama Jd na Rama dee ( Huyu yupo Anti virus).
Kama Belle aliwakataa Clouds inakuwaje karibu show zote za Fiesta ambazo zipo chini ya Clouds yupo kwenye list!
Kwa nini wasanii wakishaanza kupotea wanawasingizia Clouds? kwa hili nitakuwa wa kwanza kutokuwa upande wa Clouds kama hizi tuhuma watazitoa wasanii ambao wapo kwenye "Peak" kama wakina Diamond, Stamina, Fid nk.
 
Yesuuu Wangu!!
Belle9 ni zaidi ya Diamond na Ben Pol???!
Kama hujui music, usiongelee music.
huo mfano wako umeharibu kabisa ujumbe uliokusudia.
Jesus!

Hivi kwa akili yako huyo Diamond anaimba vitu gani kwenye nyimbo zake zaidi ya kuwataja akina Wema na Jokate..

Kwa kukusaidia tafuta wimbo unaitwa "Anaishi naye"...wamefanya Belle na Benpol, utaona nani kafunikwa!!
 
Hivi huyu Ruge ana ushawishi wa kiasi gani???mpaka kila mdau wa muziki asikilize mawazo yake pekee???Yaan huko BASATA hakuna anayefikiri vizuri...kila mtu anamlilia njaa yeye tuu???SIDHANI.....
 
Kila nnapokuona wewe unawatetea Clouds, na wala si kujenga hoja, kwani wewe ni mmoja kati ya Mashoga wa Clouds?

unajua maana ya kutetea? naomba mtu anayesema clouds inaua vipaji atoe tangible evidence kwamba wanaua vipaji kivipi?? sio kubwaja bwaja tuu, redio zipo nyingi sana hapa nchini je kuna ulazima kwa msanii kupeleka nyimbo zake clouds?? huyo bele 9 anayesema ananyonywa kila show ya fiesta hakosi kwani amelazimishwa?? wasanii kibao nchini huwa wanaomba kila mwaka wajumuishwe kwenye show za fiesta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…