Nilichukua maamuzi magumu

Nilichukua maamuzi magumu

Ndugu zangu, katika maisha kuna wakati tunapitia changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwa pamoja na mapenzi.Nilimpenda dada mmoja kwa dhati kabisa, lakini upendo toka kwake ulikuwa kama wakulazimisha hivi, maana wakati mwingine unamuona online ukimtumia msg hajibu au anachelewa sana ukiona anajibu haraka ujuwe ana lake. Niliendelea nae hivyo hivyo kwa kipindi cha mwaka mzima kwa uhusiano wa kuvuta na kamba.

Mwaka jana mwezi desemba tarehe 23 niliamua kwa dhati kabisa kuachana nae. Hatua ya kwanza niliacha kabisa kumtafuta kwa mwezi mzima huku akichungulia whatsapp status zangu na mimi kwa roho ngumu nikiangalia zake, ilipofika Janauari mwishoni mwaka huu nika m-block kabisa na kudelete number zake.

Feb alinitafuta kupitia namba ya mdogo wake nikapokea kwa vile nilikuwa siijuwi kisha yeye aliongea kwa kuomba msaaada wa kumpeleka mdogo wake Aghakhan Hospl, nilikubali kwa maana niliona siyo vita acha nitoe tu msaada, nilipofika kuwachukua sikuongea nae sana ukiondoa kumpa salaam na kisha kumpeleka huko hospital tulipofika sikuongea chochote kitu ambacho si kawaida yangu mbali ya kuwaacha na mimi kusepa zangu jambo si lakawaida.

Siku iliyofuata nikapokea simu toka kwa rafiki yake kuwa yule dada nae amewekwa mapumziko hospital ya jirani lakini hawaoni ana tatizo gani, nikamwahidi nitampigia kumjulia hali lakni sikufanya hivyo kwani nilihisi ni usongo tuuu wa mawazo hana lolote.

Jana jioni dada kapiga tena simu kupitia namba nyingine kwa sababu ya mdogo wake nayo nime block toka siku ile, na nilivyosikia tu sauti yake nilimwambia nitampgia maana nipo kikaoni, sijapiga na sitompigia maana nikianza kuwasiliana tutarudi kwenye mahusiano ambayo yeye mwenyewe aliyaletea mzaha. Tutanatimiza miezi mitano kuelekea wa sita bila mawasiliano rasmi, nimezuia mawasiliano na nimezuia kuonana naye ili iwe funzo kama mtu anakupenda usifanye mzaha na aweke nidhamu.

Nawakilisha kwenu wapendwa.
[emoji1696]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mm idd Amin dada na mobutu seseseko walikuja kwangu kwa nyakati tofauti kupata internship ya ukauzu kwa mambo kama haya

Nikupe hongera ukiona anakusumbua kwa namba nyingne mualike chakula Cha mchana mwekee na sumu afe kabisa
Mimi Ni mdoko wake idd Amin
 
Mi wala huwa sihangaikagi na kublock.
Naacha tu kiwasiliana nae, status tunaview kama kawa zangu anaview zake akipost naview kiroho safi kabisa.

Mwisho wa siku kila mtu anamove on bila taarifa ya kuachana rasmi kublockiana wala maneno machafu.

Hii ni mbinu ya kibaharia ili uje kupasha kiporo, yani kifupi huwa siachani rasmi na manzi hata akinikosea mi ntamkaushia kiivo tu.
 
Ukianza kuact kama Alpha male ndyo utajua mbona ulikuwa wapi mda wote huo yani mizani ya upendo ikiwa sawa wala huoni shida na mnaelewana sana.
 
Haina tofaut na ya kwangu mimi hata miez mi2 haikuisha nikamute mana siez bembeleza mtu asiejielewa
 
Back
Top Bottom