Nilichukua maamuzi magumu

Nilichukua maamuzi magumu

Mleta uzi wewe sasa ndio MAN OF SPERM,, Kwa kiswahili ni DUME LA MBEGU.

Usilegeze
 
Mi wala huwa sihangaikagi na kublock.
Naacha tu kiwasiliana nae, status tunaview kama kawa zangu anaview zake akipost naview kiroho safi kabisa.

Mwisho wa siku kila mtu anamove on bila taarifa ya kuachana rasmi kublockiana wala maneno machafu.

Hii ni mbinu ya kibaharia ili uje kupasha kiporo, yani kifupi huwa siachani rasmi na manzi hata akinikosea mi ntamkaushia kiivo tu.
Hujakomaa, yaani ni nusu mvulana
 
Mi wala huwa sihangaikagi na kublock.
Naacha tu kiwasiliana nae, status tunaview kama kawa zangu anaview zake akipost naview kiroho safi kabisa.

Mwisho wa siku kila mtu anamove on bila taarifa ya kuachana rasmi kublockiana wala maneno machafu.

Hii ni mbinu ya kibaharia ili uje kupasha kiporo, yani kifupi huwa siachani rasmi na manzi hata akinikosea mi ntamkaushia kiivo tu.
Hapa tunajadili mambo ya kiume si ya kivulana
 
Hapa tunajadili mambo ya kiume si ya kivulana
Kwahiyo kublock ndo njia ya kiume.

Mapenzi hayako ivo kijana ndio maana mnaumizwa sana kwa kudhani mapenzi ni ukauzu.

Na mtasaidiwa sana hao wapenzi/wake zenu ukauzu wa kijinga.

Fuata ushauri wangu ufurahie dunia, sinaga stress za mapenz mm 😃
 
Hapo kwenye block ndo umezingua mwanaume kumpiga block mtu ni udhaifu we futa namba sepa block wanapiga wanawake.
 
Kabla huu mwaka haujaisha itakuwa umesharudiana naye nakuambia 😅😅😅😅
 
Ndugu zangu, katika maisha kuna wakati tunapitia changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwa pamoja na mapenzi.Nilimpenda dada mmoja kwa dhati kabisa, lakini upendo toka kwake ulikuwa kama wakulazimisha hivi, maana wakati mwingine unamuona online ukimtumia msg hajibu au anachelewa sana ukiona anajibu haraka ujuwe ana lake. Niliendelea nae hivyo hivyo kwa kipindi cha mwaka mzima kwa uhusiano wa kuvuta na kamba.

Mwaka jana mwezi desemba tarehe 23 niliamua kwa dhati kabisa kuachana nae. Hatua ya kwanza niliacha kabisa kumtafuta kwa mwezi mzima huku akichungulia whatsapp status zangu na mimi kwa roho ngumu nikiangalia zake, ilipofika Janauari mwishoni mwaka huu nika m-block kabisa na kudelete number zake.

Feb alinitafuta kupitia namba ya mdogo wake nikapokea kwa vile nilikuwa siijuwi kisha yeye aliongea kwa kuomba msaaada wa kumpeleka mdogo wake Aghakhan Hospl, nilikubali kwa maana niliona siyo vita acha nitoe tu msaada, nilipofika kuwachukua sikuongea nae sana ukiondoa kumpa salaam na kisha kumpeleka huko hospital tulipofika sikuongea chochote kitu ambacho si kawaida yangu mbali ya kuwaacha na mimi kusepa zangu jambo si lakawaida.

Siku iliyofuata nikapokea simu toka kwa rafiki yake kuwa yule dada nae amewekwa mapumziko hospital ya jirani lakini hawaoni ana tatizo gani, nikamwahidi nitampigia kumjulia hali lakni sikufanya hivyo kwani nilihisi ni usongo tuuu wa mawazo hana lolote.

Jana jioni dada kapiga tena simu kupitia namba nyingine kwa sababu ya mdogo wake nayo nime block toka siku ile, na nilivyosikia tu sauti yake nilimwambia nitampgia maana nipo kikaoni, sijapiga na sitompigia maana nikianza kuwasiliana tutarudi kwenye mahusiano ambayo yeye mwenyewe aliyaletea mzaha. Tutanatimiza miezi mitano kuelekea wa sita bila mawasiliano rasmi, nimezuia mawasiliano na nimezuia kuonana naye ili iwe funzo kama mtu anakupenda usifanye mzaha na aweke nidhamu.

Nawakilisha kwenu wapendwa.
Safi mkuu...nakuunga mkono kwa nguvu zote na umefanya jambo moja la maana sana.
 
Inapendeza kwa kuamua kumuachia mambo yake mwenyewe...
 
Mwanangu kama upo karibu njoo nikupe hata nusu kilo ya nyama . Huo ndio uanaume bro once ukishaamua hakuna kugeuka
 
Maamuzi uchukue wewe ila utuandikie sisi ili iweje au fanya hivi nipe namba ya huyo dada kwasababu wewe mwenyewe unaonekana ndio chanzo cha mtu kuchelewa kujibu jichunguze mwenyewe cyo unakuja tu hapa kwamba umeweza unajuaje kama siyo uwongo je kama unajazwa tu acha zako wewe
 
Back
Top Bottom