Bayport
Platinum
Maboto
Kekundu
Chakubanga
Kibwengo
Nyoronyoro
Utopolo
Hao ni hatariiii kwa uchumi wako
Ukiingia huko utafilisika mpaka ujute
Bora ukope bank au Sacco's ila sio kwenye hao matapeli
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app
Kipindi na Mimi Nina kazi nilikuwa mtu wa kukopa sana ikafika stage ya kukosa hata pesa za kumudu gharama za maisha kwani mshahara wote ulikuwa unaishia kwenye madeni thanks sana Kwa washikaji zangu wa ukanda wa kusini maana walinipa morali ya kulipangua deni lote waliniambia dogo acha upumbavu yaani unakopa mkopo kulipa deni hawa dawa Yao ni kukaa kimya haukatai deni ila una ahidi kuwa utalipa na ulipi.
Sasa nikawa nikipigiwa simu naahidi napeleka afu napiga kimya ikapita miezi 5 bila ya kulipa chochote na kitu kizuri walikuwa hawajui napoishi(hii mentality naishi nayo sio lazima Kila mtu ajue unapoishi) Sasa siku Nina stress zangu nikawa nimejianika kwenye kijiwe fulani jamaa wakanidaka aisee Moja Kwa Moja mpaka ofisini kwao nikawa kama nipo under arrest mikwala kibao.
Sijakaa sawa polisi huyu hapa polisi kuniona na vile kamwili kembamba akaanza we dogo ndio unajifanya msumbufu ngoja nije akaaenda kwenye gari lake kuchukua pingu
Alivyorudi dogo simama twende Mimi nikamuuliza wapi akaniambia kituoni nikamwambia wito wa kunikamata uko wapi akashout wewe dogo msengerema nini matusi kibao mara nimetumwa na mkuu wa kituo licha ya kushout lakini akajua kuwa anaye deal naye darasa lipo kichwani akageuka kuwa mshauri ujue dogo hawa watu wanatusaidia wakati wa matatizo maana hata Mimi uwaga nakopaga Kwa hiyo Fanya ulipe Mimi nikwambia afande lengo sio kutolipa nilikuwa na changomoto zilizopelekea Mimi kutolipa ila I promise end of month nitalipa nusu itakayobaki nitamaliza next month akanipa pen na karatasi kuandika kile nilichaahidi nikafanya hivyo wakaniachia zoezi Zima lilianza tokea saa mbili asubuhi mpaka saa Saba mchana ndio natoka ofisini kwao.
Nikaona hawanijui vizuri it's was not over yet kesho yake asubuhi nikadress kicorporate mpaka makao makuu ya takukuru mkoa husika nikaomba appointment na Mkuu wa takukuru nikamweleza mkasa mzima reason ya Mimi kukopa na why nilisimama kulipa, mkuu akaniambia short and clear kama wanakudai waambie wakupeleke mahakamani na siku wakikupeleka police nipigie simu.
Nilivyotoka tu nikamvutia waya jamaa aliyekuwa akinidai Kwa sauti yenye base with a lot of confidence nikamwambia nimeenda Takukuru wameniambia kama una nidai nipeleke mahakamani nikaona jamaa sauti imebadilika ghafla akapata na kigumizi mara ohh mi Jana nimekuonea huruma mara sijui wamekudanganya mwisho ananiambia kama umeamua hivyo ngoja tuonee.
Mpaka leo nasubiri kuona.