Niliibiwa simu, wezi wamekopa kwenye line yangu. Hii inawezekana vipi wakuu?

Niliibiwa simu, wezi wamekopa kwenye line yangu. Hii inawezekana vipi wakuu?

Jackson996

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2019
Posts
773
Reaction score
1,355
Wakuu habari za January naiman wote n wazima wa afya...niende kwenye mada moja kwa moja

Tarehe 25/12/2024 saa 9 Kasoro usiku wa kuamkia Boxing Day nilikabwa kwenye bajaji

Tukio lilikuwa hivi

Nilikuwa nimetoka mizunguko ya kuizunguka dar na washkaji ilikuwa usiku wa kuamkia tarehe 26.. nilikuwa na washkaji tuko na private car wao wanaelekea tabata Mimi naenda kimara ikabid was drop ubungo mataa mida kama ya saa 9 kasoro iv .

Nikajaribu ku request bolt ila bolt nying zilikuwa ziko bize nikawa nimesimama kituo cha ubungo upande wa kwenda mbezi nikiendelea ku request bolt. Ikapita bajaji moja ikielekea kimara dereva akasema “kimara mwisho buku bado abiria mmoja” pale stend tulikuwa kama abiria wanne au watano iv
Sababu nilikuwa naenda Kimara baruti nikaona ngoja nipande umu umu then nifike baruti nitachukua tu boda

Basi bwana nikasogea kwenye bajaji nikakuta inaabiria wawili wanaume wamekaa nyuma pale . Nilivyotaka kupanda moja wa abiria akaniambia yeye anashuka mbele tu apo mi nipite Kati
Sikuina shida nikampisha akakaa pemben then Mimi nikaka katkati

Tukaanza safari adi tulipo fika kimara corner bajaji ikasimama nikajua labda ndio yule abiria mwingine anashuka Asa sikuwa makini nao sana . Asa nikaona w wa bajaji kashuka akaja upande wa kimlango kile then wakatoa visu wakaanza kuniibia

Walinichukulia simu hela zilikuwa kwenye wallet saa na vitu vingine vidogo vidogo vilikuwa mifukoni (kilikuwa ni kitendo cha sekunde chache sana) wakanuvuta wakanisukuma uko nje ya barabara wakachukua walet wakanitupia baada ya kuona imebak na vitamburisho tu

Basi wakawasha bajaji wakazima mataa wakakimbia (nilijaribu kusoma pret number nikakuta wameikunja so sikuweza kuijua ile plet number)

Basi kama baada ya dakika moja ikapita pikipiki nikamsimamisha chap nikamuelezea nikapanda tujaribu kwenda mbele tuone kama tunaweza kuiona bajaji ila sikufanikiwa basi yule bodaboda nikaendanae ad hom nikampa pesa yake ye akasepa

Nikatoka nikamgongea jirani yangu mmoja akanipa sim yake nikampigia mwanangu mmoja anauza sim Ig.. akaniambia kuna sim alitoka nazo shop yupo nazo kwake niende nikazichek

Sikutaka ata pakuche nikaanza safari time iyo iyo (ilikuwa kama 11 au 12 kasoro iv) nikafika kwa jamaa nikazichek sim nikachukua moja kati ya zile then nikampa jamaa kiasi cha pesa nyingine tukakubariana kummalizia. Nikatoka apo direct nikaenda ku rudisha line yangu kwenye kibanda cha mshkaji nafahamiana nae (mpaka saa mbili nilikuwa na sim teyari Niko hewan kama kawaida )

Asa leo nimeshangaa kuna pesa imekata kwenye line yangu sh 104000 laki moja na elfu nne inaonekana nilikopa tarehe 26/12/2025 saa 12:41 asubuhi (hii Kwa mujibu wa computer zao) ila kwenye taharifa za simu yangu inaonesha Mimi mara ya Mwisho kukopa ni march 2023 na pesa ikapipwa ndani ya siku Saba

Asa hii kitu nashindwa kuielewa kabisa wakuu hii kitu inawezekana vip
 
Ukasherehekea xmas mpk ukaibiwa, pole sana mkuu..!!

Ila wezi itakuwa wanakufahamu vizuri au katika vitu walivyokwapua kuna kimoja kimetoa taarifa zako zote..!!
Jikaze ulipe tu.!!
 
Kama kulikua na picha ya kitambulisho kwenye simu mtu anaweza tumia hizo details kubadili/Kujua password na kukopa ama kutumia mobile pesa.
Ni kwel Nilikuwa na picha ya kitamburisho kwenye simu ila ni ngumu sana wao kuiona maana nilikuwa ninapicha zaid ya 5000+ Ni ngumu sana wao kuiona picha moja ya kitambulisho
 
Ni kwel Nilikuwa na picha ya kitamburisho kwenye simu ila ni ngumu sana wao kuiona maana nilikuwa ninapicha zaid ya 5000+ Ni ngumu sana wao kuiona picha moja ya kitambulisho
Ukitafuta wewe sawa ila AI za siku hizi nafkiri Google photo ina option ya kusort hizo picha na kuweka za vitambulisho pamoja.

Ingia Google photo search identity document uone.
 
Ukasherehekea xmas mpk ukaibiwa, pole sana mkuu..!!

Ila wezi itakuwa wanakufahamu vizuri au katika vitu walivyokwapua kuna kimoja kimetoa taarifa zako zote..!!
Jikaze ulipe tu.!!
Shukran mkuu

Labda itakuwa ...lakin wallet waliniamchia

Yan nashindwa kuelewa kabisa mpaka naweza kubadirisha line
 
Mwiz alishawahi kufanya kazi kwenye uwakala, au kuwa karibu na mtoa huduma.Ngoja tusubiri maoni ya watuwenye uelewa zaidi.
Sikuwahi kufikiria itakuwa rahisi hivyo kupita na kuomba mkopo na kuchomoa kibunda hivyo
 
Back
Top Bottom